LANGO LA MOTONI CHAPTER 12
SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
CHAPTER 12
Ilipoishia
Aunt amina aliwasili pale baada ya ndege yake kushuka samira alipong'aza aunt amina alirukwa na furaha na kujikuta akimkumbatia na kulia kwa furaha na hakuamini kama kweli alikuwa kapona na anaona tena.Walingia garini na ben akawachukua moja kwa moja mpaka moshono na kwenda kupaki mtaa wa ichenga na kisha wakashuka garini.
Aunt amina alisita kungia ndani na akajikuta akitokwa na machozi na.................
Endelea
Aunt amina alisita kungia ndani na akajikuta akitokwa na machozi na ghafla akawa kama mtu aliyepandwa na kichaa na kuanza kupiga kelele huku akikimbia kuifuata barabara kuu ili arudi mjini.
Iliwachukua zaidi ya saa moja na nusu Ben na Samira kuweza kumtuliza na kumwambia ukweli aunt amina juu ya mmewe kuuawa katika tukio lile, nyumba kuchomwa moto na kila njia aliyoipitia samira mpaka kukutana na ben aliyemsaidia na kuhakikisha kuwa aunt anatibiwa na kurudi salama.
Samira pia akamweleza aunt amina kuwa hajawahi kuona mtu mwenye moyo wa kusaidia kama wa ben na imemshangaza na kuona kumbe kuna binadamu bado wa chembe ya utu hata kama dunia na watu wake wanazidi kuwa vichaa na wanyama wasio wajali wenzao na mapito yao.
" Asante sana mwanangu Ben, Mungu akupe baraka tele na pia awe mlinzi wako katika kila njia ya mafanikio mbele yako. Mimi nitaomba jambo moja tuu"
"Asante, sema tu aunt amina"
"Nitaomba kesho kwenda kuliona kaburi la mme wangu na kuwashukuru majirani na kisha nije kuishi hapa kwa muda kama ulivyosema" Aliongea aunt amina kwa sauti ya unyonge na maumivu.
" usiseme kwa muda aunt amina, mimi naomba ukae tuu na pia nitajitahidi kujaribu kuangalia nini nikupe ukifanye ili uweze pata kipato na Samira arudi shule aendelee maana mwaka huu ni kama hajasoma kutokana ma shida hizi"
" asante sana kaka ben, mungu akubariki" alidakia samira na kumfuta ben na kumnyanyua aunt amina ambaye alimkumbatia ben kama ishara kuonesha kuukubali na kuuthamini mchango wake na kisha akamalizia kwa kusema " mwanangu ni wanaume wachache sana wanaoweza kumsaidia mtu bila ya kutarajia malipo, nakushurukuru kwa kunifanya nione tena"
Ben aliwaacha na kuliwasha gari lake na kisha akaondoka kwenda mjini ambako aliishia kwenye hotel moja na kujipatia chakula cha usiku huku akiwa na fikra nyingi juu ya aunt amina ambaye kiukweli hata kama ungekuwa ni wewe msomaji ungetokwa na machozi kwa jinsi alivyoumia kuona mmewe kaondoka katika tukio la kikatili.
Usiku ule aunt amina aliongea mengi sana na samira na walijadili mengi na kila halipoongea aliishia kulia kwani aliamini kuwa furaha yake na faraja pekee imetoweka, " hebu fikiria unakaa na mwanaume kwa miaka nenda rudi hujabahatika kupata mtoto lakini bado anakupenda kwa dhati na hana hata dalili za kutoka nje ya ndoa au kukusaliti, na hata ndugu wanapojaribu kuwagombanisha bado yuko upande wako, Kweli nimeamini kuwa watu wazuri huwa hawadumu"
Maneno hayo aliyatoa aunt amina bila hata kutarajia na kumfanya samira agundue jambo ambalo alikuwa halijui kwa undani.Samira na aunt amina walikuwa na jambo moja ambalo kwa pamoja walibarikiwa nalo lilikuwa ni kuimba nyimbo kila walipokuwa katika wakati mgumu, muda huu walijikuta wakianza kuimba wimbo wao waupendao ambao taratibu uliwateka na usingizi ukatumia mwanya huo kuwabeba.
Ben alikaa pale hotelini na kuendelea kuagiza vinywaji huku sasa akijikuta kuanza kumfikiria samira kwa mtazamo tofauti na kila alipoongeza funda jipya la kinywaji chake akajikuta akipata ujasiri wa kumpigia samira na kumwambia neno ingawa ujasiri huo kuna wakati ulitoweka na kuamua kuacha.
Alikaa pale kwa muda na akaitoa simu yake na kuiangalia kwa umakini picha ya samira na kila alipotaka kumwambia kitu samira alishindwa akaamua kuandika sms hii, " Nimevumilia kwa muda lakini najikuta nashindwa kuendelea kujifanya sina hisia nawe, naomba kama ikiwa ni kwa mapenzi yako pia bila kuathiri uhusiano wetu basi tufungue ukurasa mpya"
Alishikilia kitufe cha kutumia ujumbe huu kwa muda akitafakari kama atume au asitume. Akiwa katika hali hiyo kuna rafiki yake mmoja alifika pale na kama ilivyo kwa taratibu zao za kusalimiana alimgonga bega ben kwa nyuma na kumsalimia jambo lililomshtua ben kwani alikuwa kwenye dimbwi la mawazo.
Alipokuja kupata fahamu akagundua kumbe ile meseji ilijipekeka alipogongwa bega na yule rafiki, ben alijikuta akitamka kwa sauti kubwa NOOO!!!! NOOO!!! na kutoka nje ili ampigie samira kumwambie sio ujumbe wake.
Alipiga simu ya samira kwa muda ingawa haikupokelewa alipoiangalia saa yake akagundua kuwa ni saa nane kasoro za usiku. akaishiwa nguvu na kuingia hotel kulipa bili yake na kisha kurudi kwenye gari na muda mfupi baadae akawa barabarani.
Wakati anatokeza barabara kuu kuna magari mawili yalikuja kwa kasi moja likitokea nyuma na jingine mbele na kumzingira ben na..........................
KIsa hiki kitaendelea KESHO na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia Telegram wasiliana nasi kwa Telegram namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini
Asante sana mdhamini mkuu wa kisa hiki www.karibumbeya.com ambaye anakupa nafasi ya kutangaza biashara yako bure kwa kujisajili kupitia tovuti yao na pia unaweza kuuza na kununua mahitaji yako ya msingi
KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki
0 comments: