LANGO LA MOTONI CHAPTER 13
SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
CHAPTER 13
Ilipoishia
Alipiga simu ya samira kwa muda ingawa haikupokelewa alipoiangalia saa yake akagundua kuwa ni saa nane kasoro za usiku. akaishiwa nguvu na kuingia hotel kulipa bili yake na kisha kurudi kwenye gari na muda mfupi baadae akawa barabarani.
Wakati anatokeza barabara kuu kuna magari mawili yalikuja kwa kasi moja likitokea nyuma na jingine mbele na kumzingira ben na..........................
Endelea
Wakati anatokeza barabara kuu kuna magari mawili yalikuja kwa kasi moja likitokea nyuma na jingine mbele na kumzingira ben na watu wale wakalivamia gari la lake na kumtoa nje kwa kurupushani huku mmoja wao akiutumia mwanya huo kumchoma sindano moja iliyomfanya ben alegee taratibu na kisha kutupwa kwenye moja kati ya magari yale siti ya nyuma na safari ikaanza huku ben akiwa sasa kalala na hajitambui.
Watu wale walikuwa wamevaa mask ambazo hazikuweza kuruhusu kuzifahamu sauti wala sura zao kutokana na aina ya mask hizo, hivyo ule muda wa purukushani ingekuwa ni ngumu kwa ben kuwatambua .
Mgari yale yalitembea kwa muda wa takribani dakika kama 30 na baadae yaliingia katika jumba moja pembeni ya mji lililoonekana kuwa ni kubwa na pengine mmiliki wake kuwa na kipato cha kutosha. Walimshusha ben aliyekuwa kalala kutokana na ile sindano na kisha watu wale wakamfungia kwenye chumba kimoja na kumwacha.
" Mkuu tumempata mtu uliyetutuma tukamchukue na tumeshamfungia kwenye chumba ulichotuamuru, kuna jingine la kufanya kwa sasa?" alihoji mmoja wa watu wale ambaye kutokana na amri zake kwa wenzake ni dhahiri kuwa alikuwa ndio kiongozi
" Hapana nafikiri mwacheni kama nusu saa kwani kuna kitu nakifanya kisha nitakuja nyie mwongezeni ile sindano ili asizinduke sasa" " Sawa mkuu" alimalizia kijana huyo na kisha kwenda kutekeleza amri.
Saa tisa kasoro za usiku samira alishtuka kutoka usingizini na akawa anajisikia kiu ya maji hivyo akanyanyuka na kwenda jikoni akachukue maji. Baada ya kunywa maji akaona sio mbaya aangalie simu, alishtuka kuona kuna missed calls pamoja na sms kutoka kwa Ben.
" Nimevumilia kwa muda lakini najikuta nashindwa kuendelea kujifanya sina hisia nawe, naomba kama ikiwa ni kwa mapenzi yako pia bila kuathiri uhusiano wetu basi tufungue ukurasa mpya"
Sms hii ilimfanya samira apoteze usingizi wake wote na kujitupa kwenye sofa pale sebuleni na kuanza kuitafakari, " maskini!!!! kumbe muda wote huu ben ana hisia na mimi na akaogopa kuniambia. Au ndio maana kamsaidia aunt amina? Na je nikimkataa inamaana ndio utakuwa mwisho wa msaada wake kwetu au hata kututoa kwenye nyumba?
Je nimwambie aunt amina au nitulie, na je nikimwambia atanichukuliaje? Hapana liwalo na liwe kwa sasa mapenzi hapana, ila nafikiri ni bora nimpigie na kujaribu kumwambia kuwa kutokana na yote yaliyonisibu kwa sasa sina fikra na mambo hayo, ili anipe muda kisha nikihitimu shule tulijadili, je ataelewa lakini?
Hapana nafikiri ngoja nimpigie simu sasa, mmmh!! ila nahisi kama ni usiku sana, nitampigia asubuhi, lakini kwa mtu mwenye kujitoa kama huyu katika maisha yetu, si na mimi natakiwa kumfikiria nae afurahi na kuona pia kuna watu wanamjali?"Samira alijiuliza na kujijibu bila ya jibu sahihi na hatimaye usingizi ukamchukua pale kwenye sofa na kulala usingizi mzito.
Saa tisa na nusu ikielekea saa kumi kasoro za alfajiri mlango wa chumba alichowekwa ben ulifunguliwa na boss wa vijana wale akaanza kuwakaripia wale vijana wake, " jamani mmefanya nini tena? huyu mliyemleta ni nani, mbona simfahamu? Huyu siye angalieni vyema ile picha ya gari niliyowapa"
" samahani boss basi magari yanafanana sana tukajua ndio hili kwani lilikuwa sehemu uliyotuambia tukatege na ni kama lile"
" haya sasa haraka mfungueni na nendeni mkarudishe pale mlikomchukua na hakikisheni hakuna anayewafuatilia, na mara nyingine kuweni makini makosa kama haya hayahitajiki na ni hatari"
"Sawa boss" Aliongea kijana huyo kwa uoga huku akimchukua ben ambaye bado alikuwa hajaamka kutokana na sindano ile.
Muda mfupi baadae vijana wale walifika pale njia panda walikomchukua ben na kumwingiza kwenye gari lake na kisha wao wakatokomea kusikojulikana wakimwacha ben akiwa pale ndani ya gari lake na wakati huo ilikuwa inakaribia kumi na moja kasoro za alfajiri.
Saa moja kasoro za asubuhi ben ali........................... .............................. ...
KIsa hiki kitaendelea KESHO na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia Telegram wasiliana nasi kwa Telegram namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini
Asante sana mdhamini mkuu wa kisa hiki www.karibumbeya.com ambaye anakupa nafasi ya kutangaza biashara yako bure kwa kujisajili kupitia tovuti yao na pia unaweza kuuza na kununua mahitaji yako ya msingi
KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki
0 comments: