WANAUME WANAPENDA KUOA WANAWAKE WENYE TABIA HIZI

20:15:00 Unknown 0 Comments



Mtu anaweza kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na wakati mwingine kwasababu ya kukidhi tamaa ya ngono kisha akabaini kuwa anaona mvuto mkubwa kwa mpenzi huyo. Upande mmoja ama pande zote zaweza kudhani kuwa mvuto huo ndiyo dalili za kuwa na mapenzi ya kudumu jambo ambalo ni kosa na athari zake huonekana baadae.

Sasa tukijite kwenye kitovu cha mada tajwa hapo juu ambapo wanaume wengi wanaojua athari za kukurupuka kuoa wanapofikia hamu ya kuoa si kwamba wanakurupuka bali huwachukua muda mrefu kuchunguza hata kama wataona wanawake wazuri wa sura.

Hapa ni kipindi kigumu sana kwa wanaume na wanawake wengi hujidanganya na kufikiri kuwa kitu kinachoweza kuwashawishi wanaume kuwa nao kwa ndoa ni kujiremba kupindukia hivyo wengi huishia kupoteza muda na gharama kubwa na kusahau kuwa kuolewa ni zaidi ya uzuri wa sura na kujiremba.

Hapo awali mwanamke mwenye umbo zuri na sura nzuri alikuwa na asilimia zaidi ya 90 za kuolewa lakini hali imebadilika ambapo wanawake wenye sura nzuri na maumbo mazuri wamekuwa ni wanawake wa kustarehesha wanaume na kupungukiwa sifa za kuolewa ambapo wanaume wengi wanasema kuwa wakiwaoa ni wasumbufu na wana viburi kutokana na kutongozwa na wanaume wengi hivyo kujiona kuwa soko lake ni kubwa hata akiachika.

1.Mapenzi Mema yenye faraja si makwazo
Lengo kubwa la mwanaune kuoa ni kupata mapenzi ya kweli na faraja kutoka kwa mkewe na hatimaye kupata watoto ambao wataongeza faraja katika familia na hatimaye kujivunia katika jamii mnayoishi.

Kumekuwa na tabia za wanawake wengi kupenda sana matukio kwamfano wengi wao wanapenda kuonekana wameolewa lakini maisha ya ndoa hawayataki na hawa tunawaita wanawake wazugaji na baadhi wanapenda pesa za mwanaume ama kuonekana yupo na Fulani.

Wengi wao hawajui kuwa maisha yanabadilika waweza kuwa nacho leo na kesho ukakosa na kusahau kuwa maisha ya ndoa kila uchwapo yanatakiwa kutawaliwa na upendo.

Niwakumbushe wanawake mambo walau matatu yanayoweza kuboresha mahusiano na maisha ya ndoa ambayo ni neno Samahani, pole na Asante yakizingatia hayo yatakusaidieni.

2. Mwanamke mwenye tabia Njema
Mwanamke ukiwa na tabia njema kwa kujitambua kuwa wewe ni mwanamke tayrai unakuwa umejiweka katika asilimia kubwa ya kuolewa na mwanaume wa ukweli mwenye uhitaji wa kuwa na mke maana tabia njema waswahili wanasema ni silaha.

Hakuna asiyejua umuhimu wa silaha na ndiyo maana wenzetu wazungu walio wengi wanathamini sana wapisgi na walinzi wao maana hao wameshika asilimia Fulani za uhai wao.

Linapokuja suala la kuoa hakuna mtu anayeuliza kuwa mwanamke anayetaka kuolewa ana kimo gani ama umbile likoje bali kitu cha kwanza kuuliza ni tabia watu wanaulizana ama kuambia kuwa je unaijua tabia yake? Na je unaona mtawezana na huyo mbona chakaramu huyo? Huku wengine wakisema aaaaaa.. pale umepata mke ana tabia nzuri sana na anaheshimu mkubwa na mdogo na anamisimamo.

Wapo wanaume walikurupuka kuona wanawake wenye sura na maumbile mazuri lakini baada ya siku chache kilichotokea ni machafuko makubwa na hatimaye ndoa zikavunjika na hawatamani tena hata kuwa na mahusiano ya kawaida na wanawake warembo.

3. Wenye kupenda kutoa ushauri wa kimaendeleo.
Kuna tabia mbili ambazo wanaume wanapenda kuziona kwa wanawake ambao wanatamani kuwaoa. Wanaume wengi kwa sasa hawapendi kuoa mwanamke ambaye hana kazi na vinginevyo mwanamke huyo atakuwa na mawazo chanya ya kimaendeleo.

Mwanamke mwenye fikra za kumshauri mwanaume wake masuala ya kimaendeleo na mwenye kujituma bila manug’uniko na kutoa lawama hata kwa vitu vidogo alivyotendewa na mpenzi wake ana nafasi kubwa ya kuolewa kuliko ambaye ana ajira yake kwasababu mawazo ni dira ya kila jambo.

Hapa sizungumzii mwanamke ambaye anapenda kunyoosha miguu nyumbani na kuagiza ama kupanga mambo ambayo anataka afanyiwe na mtu mwingine, la hasha bali nazungumzia mwanamke ambaye anapenda kumshirikisha mwenzi wake jambo ambalo wanaweza kulifanya kwa pamoja ama kupanga kwa ajili ya maendeleo yao na jamii inayowazunguka ikiwemo kutoa misaada kwa wahitaji ama kutembelea wagonjwa Hospitalini.

Mwanaume hapendi kuwa na mwanamke ambaye anapenda makuu, si unajua kuna wanawake si vijijini wala mijini wao makuu kwao ndo maisha, na hapa nitoe dawa inayoitwalimbwata, limbwata linalotakiwa hapa ni kwamba wanaume kama watoto wanapenda sana kunyenyekewa na hilo ni limbwata baaab kubwa hivyo mwanamke haupaswi kupenda makuu ni moja ya dalili inayokukosesha kuolewa ama kuaminika katika jamii unayoishi na kama upo kwenye ndoa tambua mwanaume wako anaporudi nyumbani anaona kama anaenda Rumande.

4. Wanawake wavumilivu
Wapo wanawake ambao si wavumilivu hata chembe katika maisha, wao akili zao zimeganda kuwa maisha yanasonga mbele bila kujua kuwa kuna wakati wa majaribu lakini kila jaribu lina mlango wa kutokea maana katika maisha ama katika mahusiano kuna matatizo ya kiafya na hata kukwama kabisa kifedha kwa mwanaume ambapo wengi wetu husfikia hatua ya kusinyaa ni kutokana na mawazo.

Matatizo ya kiafya au ukosefu wa fedha ni moja ya wakati wa kipimo kwa kutambua mwanamke mvumilivu ama matatizo mengine si tumeshuhudia wengi wakiwatoroka waume zao na kuachanana wapenzi wao kisa matatizo jambo ambalo kwa mwanamke wa namna hiyo hujidhihilisha kuwa hana sifa ya kuwa mke wa Mtu.

Baada ya kuona baadhi ya tabia ambazo wanaume wengi wanapenda wazione kwa wanawake wanaotaka kuwaoa, wiki ijayo tutaona ni vitu gani muhimu vinavyotakiwa kuwepo kabla ya kufanya mapenzi.

You Might Also Like

0 comments: