LANGO LA MOTONI CHAPTER 30

SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
CHAPTER 30
Ilipoishia
Rama akaona kama upendo umepungua kwake kwani sasa samira akawa kapunguza muda na masaa ya kuwa na rama. Rama akatumia kila njia ya kumshawishi samira apunguze kuwa na ben lakini ilikuwa ni kama anapambisha moto na siku zikazidi kwenda.
Mapenzi kwa rama yakapungua na mara moja moja samira akajikuta akimbusu ben na hatimaye aunt amina na salha pamoja na rama wakahisi kitu kati ya wawili hao, na kitu hicho kilikuja kwa mshindo mkuu tofauti na ule muungurumo wa radi na samira akawa binti mwenye furaha kuliko kawaida.
Endelea
Rama aliumia sana na hasira ikamjia na siku hii kwa mara ya kwanza alikunywa pombe na baada ya kulewa alichukua panga lake na kwenda kwa samira.
Alipofika nyumbani kwa kina samira alimkuta aunt amina akiwa nje anaanua nguo kwani giza lilikuwa linaanza kuipoteza nuru ya siku hiyo. Aunt amina alishtuka kumwona rama akiwa katika hali ile tena kashika panga mkononi.
" Mwanangu rama nini kimekusibu?"
" Siongei neno nataka kumwona samira anipeleke kwa huyo mvunja ndoa za watu nimfundishe adabu" aliongea rama kwa sauti ya kilevi huku akjaribu kutaka kuingia ndani na salha wakati huo alikuwa katoka na alipoona hali ile akaufunga mlango na kwenda kumsaidia aunt amina ambaye alikuwa muda huo akijaribu kumsihi rama atulie.
" Mwanangu rama, samira hayupo hapa muda huu, na ugomvi hautamfanya samira arudishe moyo wake kwako. Naomba twende taratibu katika hili kwani hakuna linaloshindikana, na naamini samira atakuwa na sababu ya kufanya hivyo"
"hapana nataka mmtoe aje hapa nje"
" Samira hayupo hapa, aliondoka tangu saa nne ya asubuhi na hakusema anaelekea wapi"
Maneno hayo yalimfanya rama acharuke na kumshika salha ambaye alimwongoza mpaka mtaa anaokaa dada yake ben. Wakati wakielekea huko pia aunt amina alikuwa hana jinsi zaidi ya kuwafuata ili aende kujua nini kilikuwa kinaelekea kutokea ili awe msaada wa kuepusha janga hilo lisitokee.
Mida ya saa mbili na madakika walikuwa wamefika nyumbani kwa dada yake ben, na dada yake ben alikuwa sebuleni akiangalia tamthiliya ya simu ya ajabu. Alishtushwa kuona rama akiingia kwa fujo bila ya kubisha hodi huku kashika panga na mkono mwingine kamshika salha.
" Samira yuko wapi?"
" jamani kwani kuna nini tena?, mbona mnaingia kwa shari nyumba hii"
"Nimesema namtaka samira pamoja na huyo mbwa mwingine"
" Ben na samira waliondoka hapa mida ya saa nne na kuniaga kuwa wanaenda kule bwawani kwani samira alikuwa anatamani kuogelea huko, na mpaka sasa sijui wako wapi mie nikajua wako kwa aunt amina"
"Kwangu hawajaonekana tangu samira aondoke saa nne asubuhi" alidakia aunt amina ambaye alikuwa kasimama mlangoni.
" Basi tuvute subira watakuja" alisisitiza dada yake ben huku aunt amina akitikisa kichwa kuashiria kukubaliana nae.
" hapana nitabaki hapa mpaka arudi na najua mimi nitajificha wapi" aliongea rama huku akiliweka panga lake kwapani na kufungua kichupa kidogo na kuinywa pombe ile mafunda manne na hatimaye akaondoka na kwenda nje.
Dada yake ben aliukimbilia mlango na kuufunga kwa haraka kisha akarudi kwenye sehemu yake aliyosimama hapo awali na kumwambia aunt amina " dada tunafanyaje maana huyu mtu sina imani nae naona kama anaweza kumdhuru ben au samira"
" Nimejaribu kuwatafuita wote wawili kwenye simu zao tangu tunatoka nyumbani lakini hawapatikani" aliongea aunt amina
" Mungu wangu wasije wakawa wamepatwa na shida huko maana hata mimi namtafuta ben hapa naona simu yake haipo hewani" ilikuwa ni kauli iliyoamsha hisia mpya juu ya usalama wa ben na samira huko bwani kutoka kwa dada yake ben.
Waliagana na aunt amina akarudi nyumbani akiwa kaambatana na salha ingawa walikuwa na hofu kubwa juu ya samira na rama ambaye hawakujua alikuwa wapi muda huo.
Walikaa sebuleni wakijaribu simu ya ben na samira mapaka saa nane kasoro za usiku na kuamua kulala baada ya kumpigia dada yake ben na kukubaliana waonane asubuhi ili watoe taarifa kwa mjumbe wa mtaa huo ambaye pia ni baba yake rama.
Rama alishtuka saa moja kasoro akiwa kalala nje ya nyumba ya dada yake ben ambako alijificha jana yake usiku. Alitumia kama dakika kumi aktafakari kuwa alifikaje eneo hilo bila ya majibu na alikuwa kachoka na kichwa kinamuuma sana.
Aliposimama akamfanya dada yake ben amwone na haraka akafunga mlango wa nje na akanyanyua simu yake na kumpigia aunt amina ili kumpa habari ya rama kulala pale na kuwa hakuna dalili zozote za samira na ben kuonekana.
Wakati anaongea na simu rama aliondoka eneo hilo huku akijaribu kuangalia huko na huku kama kuna mtu alimwona akiwa hapo kisha akapotea eneo hilo huku kichwani akiwa na maswali mengi juu ya kilichomfanya alale pale.
Saa tatu na nusu watu walikuwa wamekusanyika kwa mjumbe na mjumbe ambaye ni baba yake rama alioneshwa kuumizwa sana na kitendo cha mwanae ambaye jana yake alifanya kitendo alichodai kuwa sio cha kiungwana.Na wakati wote rama alionekana kuuficha uso wake kwa kiganja cha mkono wake huku akimwomba msamaha aunt amina kwa sauti ya chini.
Robo saa baadae watu hao walitawanyika na moja kwa moja baadhi yao wakiwa wameambatana na aunt amina, baba yake rama, dada yake ben, salha na rama waliondoka kuelekea bwawani ili kuona kama kuna lolote lililotokea kwa wawili hao.
Walipofika pale mtoni wote kwa pamoja walishikwa na mshangao walipoliona gauni la samira likiwa limenasa kwenye kisiki kimoja kando ya bwawa hilo. Wakiwa pale mara wakaona....................... .........................
Kisa hiki kitanendelea KESHO
NUNUA KISA CHA SIMU YA AJABU LEO KWA KUPIGA SIMU 0713317171
Pia Kwa wale wanaotaka kukisoma kisha hiki kupitia whatsapp wasiliana nami kwa namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini kuwa kupewa promo ya bidhaa zako kupiti hadithi hii
Kama umeipenda Jjisikie huru KU-SHARE Pia
*****************
Ili kutangaza Bure kupitia tovuti yetu fuata link hii karibumbeya.com/add-new/ au tuandikie kupitia: support@karibumbeya.com
Pia unaweza kupendekeza sehemu ya kuwepo tangazo lako katikka tovuti yetu ya karibumbeya.com kwa kutuandikia sales@karibumbeya.com au ukatupigia simu kupitia namba 0713317171
0 comments: