LANGO LA MOTONI CHAPTER 29

16:10:00 Unknown 0 Comments

SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU

LANGO LA MOTONI 

CHAPTER 29

Ilipoishia

Salha aliumia mguu ambao ulikatika na hivyo akakimbizwa haraka hospital  ambako alipewa matibabu ya awali na muda huo huo  alichukuliwa na kupelekwa hospital kubwa kwa ajili ya matibabu zaidi.

Taarifa zilimfikia samira na aunt amina wakiwa ofisini kwao na kwa mshtuko aunt amina alizimia na kuomba baadhi ya majirani kumsaidia na samira akachukua usafiri kwenda makao makuu ya mji huo alikopelekwa salha.

Alifika na kukuta matibabu yameanza lakini...............................................

Endelea

Alifika na kukuta matibabu yameanza lakini hakupendezewa na hospitali hiyo kwani pamoja na kutoa matibabu lakini walikuwa wakijivuta sana na kumfanya afikirie kumwamisha tena.

Alitoka haraka na kuelekea kwa dokta mkuu lakini kwenye korido alishtuka lipomuana mtu kama ben akifanyishwa mazoezi, bila hata kumuuliza mtu alienda mpaka pale lakini hakuweza kufanya lolote kwani hakuna aliyemruhusu amguse na ben alikuwa hatambui lolote.

Alirudi  na kuelekea kwa nesi mmoja na kumuuliza juu ya mgonjwa huyo na  nesi huyo akamwambia kuwa mgonjwa huyo anaitwa ben na ana muda mrefu hapo hospitalini kwani kapoteza kumbukumbu baada ya ajali mbaya iliyomwacha na majeraha makubwa sana kichwani kwake.

Iliwachukua siku 10 pale hospitali samira na salha na hatimaye salha aliruhusiwa kuondoka na mbaya zaidi ni kuwa samira hakupata nafasi ya kuongea na ben au ben kumtambua.Kila mwisho wa wiki samira alikuwa akimtembelea ben na kupata dakika chache sana za kumtazama bila ya ben kumtambua.

Jumamosi moja asubuhi samira aliwasili pale kama kawaida yake lakini jumamosi hii haikuwa nzuri kwake kwani alipofika pale aliambiwa kuwa ben kachukuliwa na nduguze na wameamua kwenda kumtafutia mtaalamu mwingine atakayeweza kumsaidia arudishe kumbukumbu mapema.

Samira aliondoka kwa unyonge na kurudi nyumbani nyumbani ambako aliendelea kuhuzunika kwa muda mpaka pale alipoizoea hali hiyo na baada ya miezi kadha aliisahau kabisa hali ile na kujikuta akisonga mbele na maisha yake na familia yake.

***

Jumatano tarehe 14-02-2007

Ilikuwa imepita miezi mingi tangu samira asahau ya kale na kuwa sasa ana ukurasa mpya wa maisha yake na familia yake. Siku hii ya wapendanao alikuwa katika bustani moja akifurahia surprise aliyopewa na rafiki yake wa kiume ambaye walifahamiana nae muda mrefu na ilikuwa ni  miezi michache imepita tangu ajikute akiwa na mahusiano nae..

Siku hii walikaa na kuongea mengi na kupanga mipango ya maisha yao ya baadae na wakati huu waliamini kuwa ni wakati muafaka kwa aunt amina na salha kujua mahusiano yao.

Walikubaliana siku ya pili yake jioni wakae kitako na kumwambia aunt  amina. Kama walivyopanga siku ya pili yake jioni Ramadhani na Samira wakawa na aunt amina na salha huku kwa pamoja wakiongea kuhusu jambo hilo.

Hakuna aliyelipinga hilo kwani walimfahamu Rama kama jirani yao kwa muda mrefu tangu walipohamia eneo hilo na hakuna aliyepinga kuwa rama alikuwa na tabia yenye kumvutia kila binti na jamii ya pale ilimpenda kwa jinsi alivyokuwa akijiwajibisha katika maisha.

Aunt amina alibaki kuwa ndugu pekee katika maisha ya Samira na Salha ukiacha mama salha ambaye yeye alikuwa na nafasi ndogo kwa muda huo kutokana na umbali na kukatika kwa mawasiliano kwa kipindi kirefu.

Ilikuwa ni furaha kubwa kwa rama na samira kukubaliwa kuendelea na mchakato wa kuwa pamoja na kuwa itatakiwa ipangwe pia siku ya wazazi wa rama kuambiwa ushirika huo.

Saa tisa za usiku ben alianza kupiga kelele kama vile alishtushwa na njozi kali na kumfanya dada yake kuamka na kumwendea haraka. Kila mtu aliyeamka usiku huo akajikuta akishangaa kuona ben kaishika tena picha ya binti yule lakini leo kwa mara ya kwanza alilitaja jina la samira na hakutaka yoyote kuishika picha hiyo na akaificha.

Hii ilikuwa ni furaha kwa wote walioamka usiku huo kwani sasa walihisi kuwa fahamu zimemrejea. Kila mmoja akaanza kuongea na ben ambaye usiku huu alionekana kurejewa kumbukumbu na siku ya pili yake dada yake akamchukua na kumtembeza katika hoteli na sehemu mbalimbali alizokuwa akipenda kujumuika pindi alipokuwa akienda kuwasalimia eneo hilo.

Walitembea na kuingia sehemu mbalimbali na mwisho dada yake ben akaona ni vyema aende kununua kuku kwa ajili ya sherehe fupi ya kumshukuru Mungu kwani ben ilipita miezi mingi sana tangu apoteze fahamu na kuwa mtu asiye na kumbukumbu.

Waliingia katika hoteli moja ambayo pia ilikuwa maarufu kwa kuuza kuku na samira alikuwa pale. Samira alishtuka alipomng'aza ben na kupaza sauti kubwa " ben!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!"

Aunt amina akaja haraka kutoka ndani na kumwona ben akiwa kaongozana  na dada yake, ben alipomwona samira alitabasamu ingawa kumbukumbu ilichelewa sana kumrudia hivyo samira akautumia muda huo kumsimulia dada yake ben juu ya ben na alivyowasaidia katika maisha yao.

Samira alishangaa sana kupata habari kuwa ben alikuwa kijijini hapo kwa miezi mingi tangu ahamishwe toka hospitali. Ilikuwa ni furaha kwa kila mtu pale.Na wakamsindikiza mpaka nyumbani kwake na kujumuika kwa chakula cha jioni ya siku hiyo.

Ilimchukua ben siku saba na hatimaye kumbukumbu zikawa zimeshamrejea vyema ingawa kuna mambo machache yalikuwa yakimpa taabu kuyakumbuka na kila alipoyatamka yalimpa shida samira kuelewa, lakini samira sasa alikuwa na furaha na kujikuta akitumia muda mwingi kuwa na ben kuliko kuwa na rama au familia yake.

Rama akaona kama upendo umepungua kwake kwani sasa samira akawa kapunguza muda na masaa ya kuwa na rama. Rama akatumia kila njia ya kumshawishi samira apunguze kuwa na ben lakini ilikuwa ni kama anapambisha moto na siku zikazidi kwenda.

 Mapenzi kwa rama yakapungua na mara moja moja samira akajikuta akimbusu ben na hatimaye aunt amina na salha pamoja na rama wakahisi kitu kati ya wawili hao, na kitu hicho kilikuja kwa mshindo mkuu tofauti na ule muungurumo wa radi na samira akawa binti mwenye furaha kuliko kawaida.

Rama aliumia sana na hasira ikamjia na siku hii kwa mara ya kwanza alikunywa pombe na baada ya kulewa alichukua panga lake na kwenda kwa.............................................................

Kisa hiki kitanendelea JUMATATU

Kwa wale wanaotaka kukisoma kisha hiki  kupitia whatsapp wasiliana nami kwa  namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini kuwa kupewa promo ya bidhaa zako kupiti hadithi hii

Kama umeipenda Jjisikie huru KU-SHARE Pia
*****************
Ili kutangaza Bure kupitia tovuti yetu fuata link hii karibumbeya.com/add-new/ au tuandikie kupitia: support@karibumbeya.com
Pia unaweza kupendekeza sehemu ya kuwepo tangazo lako katikka tovuti yetu ya karibumbeya.com kwa kutuandikia sales@karibumbeya.com au ukatupigia simu kupitia namba 0713317171

You Might Also Like

0 comments: