SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU LANGO LA MOTONI CHAPTER 24

SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
CHAPTER 24
Ilipoishia
Ilipofika saa nne kasoro za usiku wa siku hiyo mzee zombo akiwa ofisini kwake hana raha na mama zombo akiwa kakaa kibarazani kwake kutokana na joto ndani mara aliona gari likipaki getini na mara mlinzi akapewa bahasha na moja kwa moja akamletea boss wake mama zombo.
Mama zombo aliichukua na kuifungua pale kwani ilikuwa kama ni kadi ya send-off lakini alipoifingua ndani alijikuta akiamka pale aliko na kwenda haraka chooni ili kuipisha haja ndogo ipite kutokanna na mshtuko ulioambatana na hofu kuu.
" Mungu wangu Grey kauawa!!!!!!!! Nimekwisha"
Endelea
" Mungu wangu Grey kauawa!!!!!!!! Nimekwisha" Hii ilikuwa ni kauli aliyoitoa mama zombo huku akiichana chana ile picha na kuifanya iwe rahisi kuiweka kwenye tundu la choo na kisha akaiflashi na kuondoka hapo.
Alitoka kwenda kibarazani lakini kabla ya kufika nje alianza kusikia dalili za kizunguzungu na hazikupita sekunde nyingi kishindo kikuu cha mama zombo akianguka chini kiliwashtua watu wote waliokuwepo pale ndani na kumkimbilia.
Nusu saa baadae walikuwa tayari wamefika katika katika hospitali moja nje ya mji inayomilikiwa na kanisa moja na haraka matibabu yakaanza. Muda wote huo mzee zombo yeye alionekana kutokujali na baada ya mgonjwa kupewa sehemu ya kupumzika huku akiwa bado hajazinduka mzee zombo na wengine waliruhusiwa kuondoka ili nao wakapumzike usiku huo.
Mama zombo fahamu zilimrudia saa moja kasoro za asubuhi pale hospitalini na alikuwa peke yake katika chumba hicho. Simu yake ilikuwa ikiita lakini hakutaka kuangalia kwani alihisi ingempa joto bure.
Dakika chache akasikia kishindo cha mtu akija akajua ni nesi au daktari alikuwa akija hivyo akawa kajiandaa vyema kuonesha kuwa yuko imara sasa ili aruhusiwe kutoka mapema.
Moyo wa mama zombo kidogo umpasuke baada ya kuona ni yule dada aliyekutana naye sokoni na akamteka. Mama zombo akajikuta akitetemeka huku akijiuliza kajuaje kuwa yupo katika hospitali hiyo.
"Unaendeleaje mama zombo?"
"salama kiasi dada"
" mbona jana hukufanya kama ulivyoagizwa?"
" mzee zombo jana hakutoka kabisa na kujifunga katika chumba chake hivyo nikashindwa"
" na unataka niamini maneno hayo?"
"tafadhali dada naomba niamini na pia tangu juzi hali yangu haiko salama"
" Haya naondoka na nategemea kusikia lolote kutoka kwako kabla ya leo kuisha" Aliongea dada huyo na kutoka nje kisha wakaungana na khadija na kuondoka eneo hilo bila ya mtu kuwaona.
Mama zombo alitafakari kwa muda juu ya hali hiyo na kila dakika akajiona kama akizidi kuchanganyikiwa hasa akikumbuka kifo cha mpenzi wake aka serengeti boy wake na kuumia zaidi.
Nusu saa baadae mzee zombo aliingia pale hospitali na kumshuhudia mkewe akiwa katika hali nzuri inayoleta matumaini ya kuruhusiwa.
" sweetie naona uko fiti leo, pole sana mke wangu"
" Asante baba, yaani sijui nini kilinisibu"
" hujapata muda wa kupumzika inatakiwa weekend ijayo wewe na watoto mwende mkapumzike sehemu moja nzuri"
" Asante mme wangu"
" Karibu" Aliongea mzee zombo na kisha kwenda kwa daktari na kuongea nae na muda mfupi baadae mama zombo aliruhusiwa na wakaondoka kurudi nyumbani huku akiwa bado anatafakari juu ya nyaraka.
" Naomba nipigie simu saa saba kamili mchana wa leo kupitia namba hii" ujumbe huu uliingia katika simu ya Ben bila jina la mtumaji.
" mmh huyu atakuwa nani tena... ?" alijiuliza ben na kuiweka simu pembeni kisha kunedelea kuendesha gari lake akiwahi majukumu yab siku hiyo.
Muda mchache mama zombo alikuwa kawasili nyumbani kwake na akawa sasa akihitaji kupata mtori ili apate nguvu, muda huu akajifanya kudeka na kumwomba mzee zombo aende sokoni ili akamtafutie ndizi na nyama nzuri.
Mzee zombo pamoja na ubabe wake kwa hili akalegea na kujikuta akikubaliana na kuondoka na mabaunsa wake na kwenda sokoni. Huku nyuma mama zombo akautumia mwanya huo kwenda chumba cha siri cha mzee zombo na kuchukua mkoba wenye nyaraka na kuuficha mahala tayari kwakuupeleka kwa watekaji.
Nusu saa baadae mzee zombo alikuja akampa binti wa kazi mizigo nae akaanza kumwandalia mama zombo mtori. Baada ya kula waliendelea kuongea na baadae mama zombo akaingia kupumzika huku mzee zombo akiingia katika chumba chake.
Saa sita za mchana mzee zombo alimuaga mkewe na kisha akaondoka na kwenda mtaani ili apate kujumuika na wazee wenzake kwani siku hiyo ilikuwa ni jumamosi.
"haloo"
"habari, naongea na nani?"
" Hallo kaka ben, ni mimi samira"
"Samira!!!! ni wewe, habari za miaka ndugu yangu?"
" Salama kiasi, nimekukumbuka sana na samahani kwa kuondoka bila kuaga nafikiri wajua nini kilikuwa mbele yetu"
" Usijali samira naelewa, uko wapi? yaani natamani kukuona na familia yako"
" Kaka Ben, utaniona na nitakutumia meseji ya wapi niliko naomba ukiweza niambie ni lini waweza kuja tuonane, Nakupenda sana kaka, asante kwa kuwa nasi kipindi kile"
" Nakupenda pia samira" hata kabla ya kujua kama samira alisikia neno la mwisho simu hiyo ilikatwa na hata alipojaribu kuipigia tena haikuwa hewani namba hiyo.
"uuuuuh!!!!, Samira!, samira! samira!" aliongea ben huku akichukua picha ya samira nakuibusu na kisha kuendelea na majukumu ya pale ofisini kwake.
Saa kumi na mbili kasoro siku hiyo mama zombo aliondoka na gari lake kwenda nje ya mji kama alivyoambiwa na muda mfupi alikuwa kafika kwenye mashamba fulani na kulikua na nyumba moja kuu kuu huku nje yake kukiwa na gari moja dogo likiwa limepaki.
Alishuka akiwa na mkoba ule wa nyaraka na alipofika kwenye gari alishtuka na kuachia mkoba ule ukianguka baada ya kuona mabinti wawili pamoja na kaka mmoja wakiwa wamekufa baada ya kupiga na risasi na akmtambua binti mmoja.
"Mungu wangu" aliongea mama zombo huku akiokota mkoba ambao ulikuwa umeanguka na kisha akaondoka haraka eno hilo na kurudi nyumbani.
Je ni nini kitaendelea tuonane JUMATATU
Kwa wale wanaotaka kukisoma kisha hiki kupitia whatsapp wasiliana nami kwa namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini kuwa kupea promo ya bidhaa zako kupiti hadithi hii
Kama umeipenda Jjisikie huru KU-SHARE Pia
*****************
Ili kutangaza Bure kupitia tovuti yetu fuata link hii karibumbeya.com/add-new/ au tuandikie kupitia: support@karibumbeya.com
Pia unaweza kupendekeza sehemu ya kuwepo tangazo lako katikka tovuti yetu ya karibumbeya.com kwa kutuandikia sales@karibumbeya.com au ukatupigia simu kupitia namba 0713317171
*****************
Ili kutangaza Bure kupitia tovuti yetu fuata link hii karibumbeya.com/add-new/
Pia unaweza kupendekeza sehemu ya kuwepo tangazo lako katikka tovuti yetu ya karibumbeya.com kwa kutuandikia sales@karibumbeya.com au ukatupigia simu kupitia namba 0713317171

0 comments: