SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU LANGO LA MOTONI CHAPTER 25

16:06:00 Unknown 0 Comments


SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU

LANGO LA MOTONI 

CHAPTER 25

Ilipoishia


Saa kumi na mbili kasoro siku hiyo mama zombo aliondoka na gari lake kwenda nje ya mji kama alivyoambiwa na muda mfupi alikuwa kafika kwenye mashamba fulani na kulikua na nyumba moja kuu kuu huku nje yake kukiwa na gari moja dogo likiwa limepaki.

Alishuka akiwa na mkoba ule wa nyaraka na alipofika kwenye gari alishtuka na kuachia mkoba ule ukianguka baada ya kuona mabinti wawili pamoja  na kaka mmoja wakiwa wamekufa baada ya kupiga na risasi na akmtambua binti mmoja.


Endelea


"Mungu wangu" aliongea mama zombo huku akiokota mkoba ambao ulikuwa umeanguka na kisha akaondoka haraka eno hilo na kurudi nyumbani.


Nyumbani mama zombo alionekana kuchahanganyikiwa sana na moja kwa moja akaingia chumba cha mzee zombo na hapo akaona ni bora aufungue mkoba ule kuona kuna nini ndani yake.

" Kiruuuuu!!!! hapana hapa mzee zombo anahusika tuu, mbona mkoba una makaratasi ambayo hayana kitu, ila hapa sasa sina jinsi ni kujikausha tuu, maana kama ni yeye basi atakuwa anajua yote kuhusu mimi... MUNGU wangu, lakini mbona hajaniuliza?" Alimaliza kujihoji na kisha akaondoka na kwenda chumbani ambako muda mfupi usingizi ulimpitia.

" Mkuu muddy, tumevamiwa nimefanikiwa kutoroka ila wenzangu pamoja na khadija wameuawa ila mkinga amechukuliwa na watu hao, na  sijui wamelekea wapi" 

" uko wapi muda huu"


" Nipo kwenye huu msitu ........." hata kabla ahajamliza kusema  ni msitu gani, muddy alisikia sauti ya mlio wa bastola na kimya kikuu kilichofuatiwa na mshindo mkuu akajua tayari na huyu kashapigwa risasi.


Muddy aliondoka alipokuwa na kuendesha gari kwa haraka mpaka kwa aunt amina na kumweleza mkasa wote na kuwa yeye hawezi kuendelea kukaa hapo na kuusimamia mkakati huo kwani mwenzao kashikwa na kuna uwezekano mkubwa wa yeye kutafutwa na sasa hatakuwa na usaidizi.Hivyo aondoke akajiandae na atarudi kwani lengo lake kuhakikisha ukweli unapatikana

Akiwa mle ndani alihisi kama kuna mtu alikuwa akinyata kuja hivyo akanyata na kuingia chumba cha samira na kutokea dirishani mpaka nyuma ya migomba fulani na kukaa sehemu ambayo ilimfanya aone nyumba kwa ufasaha.

ALikaa pale kwa muda mpaka giza lilipoanza kukulea na hakukuwa na dalili ya mtu yoyote, akarudi ndani kwa kunyata na kuwaaga kina aunt amina ambao wao walikuwa wakilia hasa wakimkumbuka khadija na wale vijana wengine.

Muddy akaondoka na hakutaka kabisa kulala mji huo hivyo akaendesha gari ili atoke nje ya mji huo. Baada ya kutembea kwa muda wa nusu saa akasimamishwa na gari moja lililokuwa na polisi wawili waliovalia sare na watatu nguo za kiraia na kumwamuru ashuke chini ili walikague gari huku nae wakitaka awape kitambulisho chake.

Wakati anashuka tuu akaanza kuhisi kama sio askari wa ukweli bila hata kukawia askari wale walipiga risasi nne na kuondoka na gari lao haraka eneo hilo.

Mzee zombo alionekana mtu mwenye furaha sana siku hiyo pale Billionaires Palace Garden  na alikuwa akitoa ofa kwa kila mtu na wakati huu alikuwa yupo na Suzane binti ambaye ndio kwanza alikuwa amerudi kutoka masoni.

Usiku huu mzee zombo alikuwa akimfanyia suzane sherehe ya kumpongeza kuhitimu masomo na  kurudi salama kutoka nchini Kenya ambako alienda kusomea masuala ya usimamizi wa hoteli.

Kila mtu alionekana kufurahi huku mzee zombo kila mara akionekana kumbusu hadharani suzane jambo liliowafanya baadhi ya wanaume watoe macho ya wivu kutokana na jinsi suzane alivyoumbika.

Mzee zombo na suzane walifahamiana miaka kama 10  iliyopita wakati mzee zombo aliposafiri na kwenda mji jirani. Jioni ya siku hiyo akaitembelea bar moja ya uswahilini. Alikunywa pombe nyingi na baada ya kulewa akawa akihitaji mwanamke wa kulala nae.

Alipoongea na muhumu wa eneo hilo, mhudumu akampa namba ya suzane ambaye alikuwa akifanya kazi ya kujiuza kwa kuacha namba zake kwenye bar au baadhi ya hoteli za uswahilini kwa ajili ya wageni wafikao kwani pale mtaani watu walishamchoka na habari zake za umalaya wa kujiuza zilitapakaa kila kona za mji huo.

Sifa kubwa ya suzane ilibaki ukiachana na mvuto wa sura, nywele na macho  ilikuwa ni umbo lake ambalo liligawika mithili ya umbo namba nane na hakuna nguo ambayo angeivaa na ikamkataa sema tuu maisha yalikuwa magumu.

Suzane baada ya bibi yake kufa alijikuta akiacha shule akiwa kidato cha tatu na kujiingiza kwenye biashara ya kuuza mwili baada ya kukosa ndugu au hata mtu wa kumsaidia kwani baba na mama walikufa pia kutokana na gonjwa la ukimwi na kumwacha yeye na wadogo zake wanne.

 Kila aliyejitokeza kumsaidia aliishia kumtaka kimapenzi na kumkimbia jambo lililomfanya akate tamaa ya maisha na kujiona ni kama mtu aliyetengwa na dunia..

Usiku huo mzee zombo aliondoka na suzane na kwenda nae hotelini ila hata alipofika hakuweza kufanya lolote kutokana na pombe nyingi. Asubuhi alishtuka kumwona suzane akitoka kuoga na kuanzia siku hiyo aliapa kutomwacha na kila sehemu alikuwa nae mapaka hapo alipoamua kumpeleka shule na baada ya kukaa huko kwa muda mrefu siku hii ndio alikuwa karudi na sasa ilikuwa ni shrehe kubwa.

" Ndugu zangu, asanteni sana kwa kuja na kuniunga mkono katika hafla hii fupi ya surprise ya kumkaribisha Suzane ambaye amerudi kutoka masomoni kenya, na anarudi kuanza majukumu yake kama .meneja mkuu wa Billionaires Palace Garden.......... Billionaire zomboooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!! ""

Billionaire FOREVERRRRRRRRRRRR!!!!!!" aliitikiwa na watu wote na baada ya hapo vinywaji viliendelea na muda mfupi baadae suzane alikuwa chumbani kamwegemea kifuani mzee zombo huku akimkuna kidevu cheke na kumshukuru kwa nafasi hiyo na kumwahidi kuwa mtiifu achilia mahusiano yao.

" Thank you" aliitikia mzee zombo

******

Saa kumi na mbili kasoro za asubuhi mlinzi mmoja wa kampuni binafsi alikuwa njiani akiwahi kwenda kazini mara akasikia sauti ya mguno wa mtu aliyekuwa akigumia kama anahitaji msaada.

Kumsogelea na kummulika vyema akaona ni kijana ambaye amepigwa risasi na damu zimemtapakaa mwilini, mlinzi akamchukua na kuomba msaada wa baadhi ya wasamaria na kumpeleka hospitali ambako matibabu yakaendelea.

Ben aliwasha gari lake majira ya saa mbili jumapili hiyo na kuanza safari ya kuelekea...........................................

 Kisha hiki kitanendelea KESHO

Kwa wale wanaotaka kukisoma kisha hiki  kupitia whatsapp wasiliana nami kwa  namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini kuwa kupea promo ya bidhaa zako kupiti hadithi hii

Kama umeipenda Jjisikie huru KU-SHARE Pia
*****************
Ili kutangaza Bure kupitia tovuti yetu fuata link hii karibumbeya.com/add-new/ au tuandikie kupitia: support@karibumbeya.com
Pia unaweza kupendekeza sehemu ya kuwepo tangazo lako katikka tovuti yetu ya karibumbeya.com kwa kutuandikia sales@karibumbeya.com au ukatupigia simu kupitia namba 0713317171

You Might Also Like

0 comments: