SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU LANGO LA MOTONI CHAPTER 23

16:03:00 Unknown 0 Comments


SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU

LANGO LA MOTONI 

CHAPTER 23

Ilipoishia

" Duh, mambo juu ya mambo, nikisema niwaibie huo ufunguo wa chumba cha siri cha mzee zombo na kuwapa haya mafaili na mzee kombo akinishika nitaachika, na nikisema nisiwape ndani ya siku mbili wamedai watanifanya kitu kibaya, sasa hapa sijui nafanyeje mbona nahisi kufa kufa!!!, ila piga ua mimi bado ni mtoto wa mjini tutapelekeshana tu" almaliza kuongea mama zombo na kuanza kuoga.

Saa saba kasoro dakika 20 za usiku simu iliita......................................


Endelea



Saa saba kasoro dakika 20 za usiku simu iliita na wakati huo mzee zombo alikuwa akikoroma vya kutosha kwani mida kabla ya usingizi kumchukua alikuwa akitwika pombe kali. Mama zombo akaingalia simu ile na kugundua ilikuwa ni ya mzee zombo.

Akiwa anatafakari nini afanye mara simu yake nayo ikaita mlio ulioashiria kuna ujumbe mfupi wa maneno uliingia muda kidogo, hivyo kwa tahadhari  akanyanyuka na kuiweka kimya simu ya mzee na akanyata kuelekea  chooni ili apate mwanya wa kwenda kuisoma meseji hiyo.

" nisamehe nakutumia ujumbe huu mida hii, ila jioni ya leo nimetishiwa sana juu ya uhusiano wetu na watu wawili tofauti, hivi hapa  nimekimbia sijalala kwangu naomba asubuhi tuonane tuliweke sawa jambo hili. Hawa watu hawajasema wanataka nini ila nina hofu sana na maisha yangu hivi sasa"

"Mungu wangu!!!" alijikuta mama zombo akitamka kwa sauti bila hata ya kutarajia na ili kupoteza maboya kama mzee zombo kasikia akajifanya kufungulia sinki la maji kama ana flash choo na kutoka kwenda sebuleni.

Moja kwa moja akajikuta akipitiliza mpaka kwenye kabati la vinywaji na kuchagua kinywaji kimoja kikali na kisha akakimiminia mdomoni bila hata ya kuwa na glass. Alikaa pale kwa muda na kichwa kikaanza kuwa kizito na kwa mbali wazo la kwenda chumba cha mzee zombo likawa likimnyemelea ingawa akaishia kupekua simu yake kuangalia sms.

Kulikuwa na kama sms 2 ambazo ziliingia baada ya yeye kulala kwani alikuwa na tabia ya kufuta sms kila mara ili kuepusha shari la wivu wa mzee zombo, moja wapo kati ya sms hizo ilikuwa ni kutoka kwa wale waliokteka wakimkumbusha kuwa kesho yake jioni  alitakiwa afanikishe zoezi hilo.

Meseji hii ilimfanya anyanyuke kichovu akiwa na pombe yake na kwenda chumba cha siri cha mzee zombo. Alipekua baadhi ya mafaili na makorokoro mengine  na kuja kukutana na kitu kilichomfanya aigugumize ile pombe na kuanza kulia kilio cha chini chini kilichompelekea kulala.

Aliamshwa saa kumi na mbili kasoro wakati binti wa kazi alipogonga mlango ili amuulize mzee zombo kama angependa kupata supu ya aina gani asubuhi hiyo kwani huwa anawahi sana kuamka kufanya mazoezi pamoja na kuongea na simu na wadau wake wa siri.

Binti alifungua mlango na kumwona mama zombo akiwa kalala huku kashika picha ya samira mkononi. Binti akamwamsha na mama zombo alipoamka alimshangaza binti alivyo kurupuka na kuyaweka mafaili vizuri na kisha kuondoka haraka huku akimwambia binti akae kimya kama hajaona kitu.

Mama zombo alirudi haraka chumbani na kumwona mzee zombo akiendelea kukoroma nae taratibu akajilaza kitandani na kumkumbatia kama hakuna kilichotokea vile. Masaa mawili na nusu baadae wote walikuwa mezani wakipata kifungua kinywa.

Samira aliamka kwa kuchelewa kuliko siku zote na siku hii alikuwa hana raha kabisa na hata ile kawaida yake ya kuimba  na kuwachekesha wenzake ilikuwa imetoweka. Salha alikuwa mtu wa kwanza kuligundua hilo hivyo akaamua amshirikishe aunt amina na wote wakamfuata chumbani kwake.

" samira una nini leo?, sio kawaida yako kuwa hivi" alihoji aunt amina huku akiketi kitandani kwa samira


" Kiukweli nafikiri tumefanya jambo lisilo na busara kutokumkumbuka Ben pamoja na nguvu, mali,pesa na muda alioutumia juu yetu. Kwangu naona ni unyama  pia kama ambao na sisi tunadai uncle zombo hakumfanyia sawa baba kwa kumuua pamoja na mali, fedha, jitihada, upendo na kila fadhila aliyowapa kama nduguze lakini bado walikuja kumuua.

Mimi nafikiri ni vyema tuwasiliane nae na  sina uhakika kama anaweza kutudhuru maana kama angekuwa wa kutudhuru basi angeshatudhuru bila hata ya kupoteza fedha zake"


" Nafikiri uko sahihi dada samira" aliongea salha ambaye nae pia aliumia kwa umamuzi wao

" mwanangu uko sahihi lakini hofu yangu kubwa ni kuwa kama ukiwasiliana nae atataka tuonane na kina muddy kwa sasa wamekataa kuwasiliana na mtu yoyote sasa tufanyeje maana hata mimi naona hapo nilipotoka katika maamuzi"

" aunt mimi nafikiri tuwasiliane nae kwa siri sidhani kama kina muddy wata......." hata kabla ya kumaliza kuongea samira alishtushwa na sauti ya khadija akiugonga mlango.

Walimkaribisha na alipoingia hakutaka kukaa zaidi ya kuwapa taarifa ya walikofikia juu ya mkakati wao na kuwa wanategemea jioni ya siku hiyo wataweza kupata nyaraka muhimu kutoka kwa zombo kwani wameshakamilisha kila mpango na wana uhakika.

Kila mtu alifurahi na kimya kirefu kikapita kabla ya aunt amina kuongoza sala fupi ya kumwomba Mungu aendelee kusimamia mipango hiyo ili ikikamilika mzee zombo afikishwe mahakamani. Baada ya hapo khadija aliondoka na kuwaacha wanafamilia wakiwa na furaha isiyo na kifani.


Mida ya saa nne na nusu baada ya kifungua kinywa  mama zombo aliondoka nyumbani kwake na moja kwa moja  akaongoza ili kwenda ambako alitakiwa kukutana na grey ili waongee. walifanikiwa kuongea na akampa kiasi cha shilingi milioni moja na kumwambia aondoke hapo mjini aende mbali na kuwa atakuwa akimtumia fedha ya kuishi ili wasimuone na abadili namba na watawasiliana wiki nne baada ya kufika kisha mama zombo akarudi nyumbani.

Alikuwa kajiridhisha kabisa ya kuwa hakuna ambaye angemsumbua kwani wale watu wasingekuwa na ushahidi wowote tena. Aliendelea kufanya kazi zake za nyumbani mpaka mida aliyotakiwa kupeleka nyaraka inapita lakini hakuwa na hamasa ya kufanya lolote.

Ilipofika saa nne kasoro za usiku wa siku hiyo mzee zombo akiwa ofisini kwake hana raha na mama zombo akiwa kakaa kibarazani kwake kutokana na joto ndani mara aliona gari likipaki getini na mara mlinzi akapewa bahasha na moja kwa moja akamletea boss wake mama zombo.

Mama zombo aliichukua na kuifungua pale kwani ilikuwa kama ni kadi ya send-off lakini alipoifingua ndani alijikuta akiamka pale aliko na kwenda haraka chooni ili kuipisha haja ndogo ipite kutokanna na mshtuko ulioambatana na hofu kuu.

" Mungu wangu Grey kauawa!!!!!!!! Nimekwisha"


Je nani kamuua grey na kwa nini?, na  je nini hatma ya mama zombo, samira na ben .... ????tuonane jumatatu



 Kwa wale wanaotaka kukisoma kisha hiki  kupitia whatsapp wasiliana nami kwa  namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini kuwa kupea promo ya bidhaa zako kupiti hadithi hii

Asante sana mdhamini mkuu wa kisa hiki www.karibumbeya.com ambaye anakupa nafasi ya kutangaza biashara yako bure kwa kujisajili kupitia tovuti yao na pia unaweza kuuza na kununua mahitaji yako ya msingi

KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki

You Might Also Like

    0 comments: