SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU LANGO LA MOTONI CHAPTER 26

SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
CHAPTER 26
Ilipoishia
Saa kumi na mbili kasoro za asubuhi mlinzi mmoja wa kampuni binafsi alikuwa njiani akiwahi kwenda kazini mara akasikia sauti ya mguno wa mtu aliyekuwa akigumia kama anahitaji msaada.
Kumsogelea na kummulika vyema akaona ni kijana ambaye amepigwa risasi na damu zimemtapakaa mwilini, mlinzi akamchukua na kuomba msaada wa baadhi ya wasamaria na kumpeleka hospitali ambako matibabu yakaendelea.
Endelea
Ben aliwasha gari lake majira ya saa mbili jumapili hiyo na kuanza safari ya kuelekea kwa samira kama alivyoelekezwa. Kwenye gari alikuwa akisikiliza wimbo maarufu wa Michael Jackson uitwao Human Nature na sehemu aliyoipenda ilikuwa ni,
"Looking Out
Across The Morning
The City's Heart Begins To Beat
Reaching Out
I Touch Her Shoulder
I'm Dreaming Of The Street"
Wimbo huo wakati unaimba yeye alikuwa akifikiria jinsi atakavyomwambia samira kuwa anampenda na samira akamkubalia na kufikiria furaha itakayowatawala muda huo.
Alifikiria mengi sana juu ya mapito ya samira na wakati huo alikuwa akinywa bia yake ya kopo kama kawaida yake akiwa safarini.Safari iliendelea huku wimbi la mawazo likimtanda juu ya samira.
"Hivi samira atanielewa kweli?, au ataniona kama nilifanya yote yale kwa kumpenda?, na je atafikiria nini baada ya kumwambia nampenda huku sikumtafuta tangu alivyo hama?, ila nampenda samira hata iwaje" maneno haya alijisemesha ben huku akiendesha gari.
Saa nne na nusu za asubuhi ben alikuwa akiendesha gari lake kwa kasi huku mawazo yake ya kiwa kwa samira na jinsi atakavyopokelewa, mbele yake kulikuwa na gari dogo ambalo lilikuwa likienda kwa kasi na ben alikuwa karikaribia. Gari hili mara likaanza kuyumba yumba pale barabarani na ghfla likafunga break ya ghlfa na kumfanya ben kuligonga kwa nyuma na yeye kuangukia upande wa pili na gari kutumbukia kwenye korongo,
Korongo hili kubwa lilimfanya ben na gari lake kutosikika kwa muda mpaka waokoaji wakuja kumwopoa ben alikuwa hajitambui na kaumia vibaya sana kichwani mwake.Alichukuliwa mara moja na kupelekwa hospital kwa matibabu zaidi.
Samira alishangaa sana kuona aunt amina hajatoka ndani siku hiyo baada ya kusubii kwa muda mrefu akaona ni vyema ampelekee kifungua kinywa aunt yake chumbani kwake,
Alishtuka kuona aunt amina akiwa analia tena kalala chini kama alipigwa na mtu au anakumbuka mmewe aliyefariki. Samira akatoka nje na kumwita salha na kwa pamoja wakajitahidi kumsihi aunt asilie.
" nini kimekusibu aunt"
" Muddy alipatwa na ajali mbaya na sasa yu maututi na yupo hospitali ya rufaa"
"Nani kakuambia" alihoji samira
" nimepigiwa simu na mzee shomari yule mlinda ghala la kijiji"
Samira hakuongea kitu akaufungua mlango na kutoka nje hata kabla hajakaa simu nyinge iliita na alipoipokea alikuwa ni mwalimu jack akimwambia juu ya habari ya ajali mbaya ya ben na kuwa sasa anapumulia mashine.
"mungu wangu, hivi dunia hii ina nini, kila anayetaka kutusaidia anapatwa na janga, tumekukosea nini mungu, jamaniiiii" maneno haya ya huzuni aliyatoa samira huku akilia
Kilio chake samira kiliwashtua baadhi ya majirani na kumfuata inagawa hakuna aliyefanikiwa kujua nini ilikuwa tatizo kwa samira kulia muda huo na kuna baadhi wao walionekana kulia hata kama hawakujua shida ilikuwa nini.
Mzee zombo alirudi nyumbani kwake saa sita kasoro za mchana siku hiyo na kama kawaida hakuna aliyeweza kumuuliza wapi alikuwa. Muda mwingi alionekana kuwa na furaha kutokana na umahiri wa Suzane kitandani jana yake.
Aliingia chumbani na kumshuhudia mkewe akiwa bado kalala fofofo, hkufanya lolote zaidi ya kuondoka na kwenda sebuleni ambako alijumuika na wazee wenzake aliowaalika kupata vinywaji muda huo.
Saa kumi kasoro kuna mgonjwa alianza kurusha miguu kama dalili za kutaka kukuta kauli, manesi na madaktari walikizunguka kitanda chake na dikika mbili baadae mgonjwa ali.......................
Kisha hiki kitanendelea KESHO
Kwa wale wanaotaka kukisoma kisha hiki kupitia whatsapp wasiliana nami kwa namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini kuwa kupewa promo ya bidhaa zako kupiti hadithi hii
Kama umeipenda Jjisikie huru KU-SHARE Pia
*****************
Ili kutangaza Bure kupitia tovuti yetu fuata link hii karibumbeya.com/add-new/ au tuandikie kupitia: support@karibumbeya. com
Pia unaweza kupendekeza sehemu ya kuwepo tangazo lako katikka tovuti yetu ya karibumbeya.com kwa kutuandikia sales@karibumbeya. com au ukatupigia simu kupitia namba 0713317171
*****************
Ili kutangaza Bure kupitia tovuti yetu fuata link hii karibumbeya.com/add-new/
Pia unaweza kupendekeza sehemu ya kuwepo tangazo lako katikka tovuti yetu ya karibumbeya.com kwa kutuandikia sales@karibumbeya.
0 comments: