Busara kutoka kwa mhehe pekee mwenye simati foni
DAIMA KUWA NA FURAHA
Siku moja mwalimu aliingia darasani na kuwaambia wanafunzi wajiandae kwa mtihani wa kushtukiza.
Kila mwanafunzi akawa amejiandaa na wakati huu kila mmoja kakaa kimya akisubiri mtihani huo uanze huku baadhi wakiwa na hofu na wengine kwa furaha kama kawaida yetu tukiwa mashuleni.
Kisha mwalimu akaanza kugawa makaratasi yenye maswali na kuyaweka yatazame chini, na alipomaliza kuyagawa akawaambia wanafunzi wayatazame na kisha mtihani uanze.
Kila mmoja akapatwa na mshangao, kwani hakukuwa na swali lolote zaidi ya alama ndogo nyeusi ya duara liliyokuwa katikati ya karatasi hilo.
Baada ya mwalimu kuona mshangao katika kila nyuso ya wanafunzi hao, akawaambia yafuatayo:
“Nataka kila mmoja aandike anaona nini katika karatasi lake.”
Hapa wanafunzi wakawa wamechanganyikiwa na kila mmoja akaona aanze kuujibu mtiani ambao haueleweki.
Baada ya kumaliza wote, mwalimu aliyachukua makaratasi ya majibu na kuanza kulisoma moja baada ya moja kwa sauti kubwa mbele ya darasa.
Wanafunzi wote bila hata ya kuacha, walikuwa wameilelezea ile alama ndogo nyeusi ya duara liliyokuwa katikati ya karatasi hilo.
Baada ya kuyasoma majibu ya wote, darasa lilikuwa kimya, kisha mwalimu anaanza kutolea maelezo ya kina.:
“Sitaweka rekodi za huu mtihani wa kushtukiza,nilitaka kuwapa kitu cha kuwafanya mfikirie zaidi.
Hakuna mtu aliyeandika kuhusu upande uliobaki wa karatasi jeupe ambao ulikuwa tupu bila neno au alama yoyote ile.
Kila mmoja alielekeza mawazo yake katika ile alama ndogo nyeusi ya duara liliyokuwa katikati ya karatasi. Na hii ni pia hutokea sawa sawa katika maisha yetu ya kila siku.
Tuna karatasi jeuspe la kuliangalia na kufurahia, lakini sisi tunaweka hamasa zetu katika alama nyeusi. Maisha yetu ni zawadi kutoka kwa Mungu baba yetu anayeishi, akitupenda, kutujali.
Na tuna kila sababu ya kufurahia mazingira tuliyonayo na mabayo kila majira hubadilika kwa ajali yetu, marafiki wazuri tulio nao na watuzungukao, kazi ambazo hutupa maisha yetu ya kila siku hasa chakula mezani na hata maajabu ambayo kila siku tunakutana nayo katika maisha yetu...........
Cha ajabu, tunakomalia katika alama nyeusi tuu kama ile ya karatasi ambayo ni –magonjwa yanayotuandama, ukosefu wa hela, ajira, mahisiano mabovu baina ya sisi na wenza wetu, familia zetu na hata changamoto tunazozipata katika maisha yetu na kadhalika......
Ile alama ndogo ya duara ni sawa na vijimatatizo vidogo ambavyo tunavyo katika maisha yetu lakini ndio huwa changamoto kubwa zinazotufanya hata tukose furaha na kujiona kuwa hatuna maana katika maisha haya.
Hebu jaribu kuyapeleka macho yako mbali kutoka kwenye hii alama ndogo tena nyeusi katika maisha yako. Furahia kila baraka unayoipata katika maisha yako, kila hatua unayopiga katika maisha yako na endelea kuamini KILA BAADA YA GIZA NURU HUJA
DAIMA KUWA NA FURAHA IDUMOYO DAIMA!
0 comments: