HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Season 10

07:50:00 Unknown 0 Comments

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Season 10

Yaliyomo
Baba Pachu ni kijana aliyejaliwa kuwa na mke na watoto wawili na familia yake imekuwa ya furaha na amani kwa muda mrefu.

Pamoja na kuwa na furaha hiyo pia Baba Pachu amejaliwa kuwa na mafanikio makubwa katika kazi zake binafsi na pia ni mfanyakazi wa kampuni moja maarufu sana yautafiti wa madini.

Siku moja akiwa katika mihangaiko yake binafsi nje ya jiji la Mbeya majira ya usiku akiwa chumbani mwake mara anapokea simu ngeni kutoka kwa mtu asiyemfahamu.

Mara ya kwanza ilionekana kama ni WRONG NUMBER lakini baada ya muda ulivyozidi kwenda ikaonekana kuwa sio WRONG NUMBER tena bali ni mtu anayemfahamu fika ingawa yeye hamtambui na nia yake ikiwa haieleweki.

Simu hii ya AJABU ikanza kuipoteza furaha ya baba pachu na hatimaye furaha ya familia nzima, kazini mpaka jamii inayomzunguka kuanza kumwona kama mtu anayeanza kuchanganyikiwa.

Baba Pachu anaanza mkakati wa kutatua tatizo lake na mkakati huo unamfanya baba Pachu kujikuta anapita katika njia zenye visa vya kutisha, majaribu, vioja na heka heka nyingine nyingi zenye maumivu na kuifunza jamii.


ILIPOISHIA 
Safari hii mambo yalikuwa tofauti kabisa na nilivyodhania kwani simu iliita kwa muda kidogo halafu ikapokelewa. 
Mwee!! mwee!! mwee!! mwee!! niliachia shuzi moja kubwa kama bomu la nyuklia kwani nilisikia sauti ya yule dada akasema hivi..........................

Endelea

Mwee!! mwee!! mwee!! niliachia shuzi moja kubwa kama bomu la nyuklia kwani nikasikia sauti ya yule dada akasema hivi, "  Haya niambie sasa naona leo umeamua kunipigia kwani niliitegemea sana simu hii kutoka kwako"
Aliendelea kusema, " We mwanaume umeniudhi sana kwa tabia uliyoifanya na kama utarudia siku nyingine yaani kitu nitakachokufanyia hutokaa usahau maisha yako yote"
Muda wote huo sikujibu hata neno moja nikipumua kwa chini chini mithili ya askari aliyeko vitani na kupata ishara ya adaui kuwepo eneo hilo na sikuweza kukumbuka aliendelea kuongea maneno gani zaidi ya neno la mwisho alilosema " NAJUA KILA KITU UNACHOKIFANYA NA NITAKUFUATA POPOTE UTAKAPOENDA"
Kwa uoga nilikata simu ile na nikapata wazo la kumpigia rafiki yangu mmoja maana niliona maji yashazidi unga, na nikiendelea kuficha nikakumbuka ule msemo wa vijana usemao mficha maradhi kifo kitamuumbua hivyo nikampigia rafiki yangu aitwaye Dole Gumba Mwakibubu.
Mwakibubu ni moja kati ya marafiki zangu niliosoma nao enzi hizo nikiwa chuoni Tumaini pale iringa na nakumbuka mara baada ya kuhitimu na kupata kazi njombe na kufanya kwa miezi kadhaa alibahatika kupata ufadhili wa kwenda kusoma nje kwa mwaka mmoja.
Kwa kuwa mkewe alikuwa mjamzito wa mwezi mmoja aliamua kutafuta binti wa kazi ili asaidiane na mkewe kwa kipindi atakacho kuwa masomoni na binti yule alipatikana ingawa kwa mwonekano alionekana ni binti wa kawaida sana aliyehitmu masomo ya kidato cha nne na kukosa nafasi ya kujiendeleza.
Akiwa masomoni akaongezewa muda na kukaa mwaka mmoja na miezi kadhaa na siku anarudi mkewe alikuwa kijijini na yule binti wa kazi kabaki nyumbani.
 Mwakibubu alishikwa na mshangao kuona jinsi yule binti alivyobadilika na kuwa mtoto mzuri tena mwenye mvuto wa ajabu tofauti na alivyomwacha.
Wajua tena mtoto wa kibongo ambaye ni kuku wa kienyeji apate bahati na akae sehemu yenye rutuba anavyonawiri!!!!. Basi mwakibubu akamwomba penzi na binti akakataa kwa jinsi alivyokuwa akimheshimu dada yake ambaye ni mke wa mwakibuku ingwa hakuweza kumdhibiti mwakibubu kwani alifanikiwa kumwingilia kinguvu binti yule.
Binti akamwamabia mwakibubu akimtahadharisha kuwa angepatwa na mkasa mzito lakini yeye kwa dharau akacheka na kuendelea na mambo yake. Muda ulipozdi kwenda na mkewe yupo kijijini mwakibubu akaanza kugunduaq boxer zake zinapotea mle ndani kimiujiza na baada ya kushindwa kuvumilia akamuuliza yule binti.
Mwakibubu kidogo azimie baada ya kujibiwa na yule binti kuwa boxer hizo amezichukua na kazituma kwa babu yake huko sumbawanga kwani babu alimkataza asitembee na mtu yoyote mpaka ndoa hivyo atakayemfanya avunje ahadi hiyo lazima afanyiwe mila.
Ilichukua zaidi ya siku tisini za kutolala usingizi na kuchanganyikiwa huku akizidi kukonda bwana mwakibubu na kujikuta akimlipa fedha nyingi huyo binti ili amtumie babu yake na mwakibubu aokoke kukumbwa na janga la kimila na mwishowe mwakibubu akaja kugundua kuwa hakukuwa na mila yoyote zaidi ya binti kufungua duka kubwa la nguo mtaa wa nne kutoka kwao kwa ufupi binti alitumia fursa ya kibunifu kujipatia mtaji.
Kutokana na kisa hicho cha mwakibubu ambacho kilitufanya tumcheke sana na kumwona ni zube lakini wakati huu nikaona kuwa yawezekana visa vyetu vinaendana nimfuate ingawa mimi simwoni adui yangu na mpaka sasa sijui anataka nini na uwezo wake wa kutambua ratiba zangu anautoa wapi na kwa namna zipi?
Nilimpigia simu ili nimweleze yanayonisibu na nakumbuka tuliongea kwa muda kisha tukakubaliana tukutane ili nimweleweshe kwa undani zaidi. 
Basi tukakubaliana tukutane maeneo ya forest na kwa kuwa ni jirani na Gracious House of Cakes, tukaona ni vyema tukutane hapo na maongezi yaendelee huku tukitafuna cake na bisi kuyafanya mazungumzo yetu yanoge zaidi ingawa kwangu bado nilikuwa naona kama natazama filamu tena ya kihindi..
Mwakibubu aliwahi kufika pale na nikamkuta akiwa tayari akinisubiri na maongezi yetu yakaanza kwa mimi kumsimulia kisa kizima tangu sekeseke hili linaanza mpaka lilipogeuka na kuwa muvi ya kutisha na kuninyima usingizi.
Alishangaa sana na kunilaumu kwa kukaa kimya kwa muda wote huo na kuniomba nimpe meseji hizo ili azisome mwenyewe na kuhakikisha maana aliona ni kama filamu, eti kudume mimi natishiwa mpaka nanusurika kugongwa tako na bodaboda kisa ujumbe wa simu???? Haikumwingia akilini.
Aliichukua simu ile na alipoifungua meseji ya kwanza  alishtuka na kuniambia............................................................................................................. Je ni nini aliniambia? Na aliona nini kwenye hiyo meseji? Je tatizo litatatulika au ndio mwanzo wa safari mpya ya kutisha????
Usikose kusoma kisa hiki cha kusisimua jumatatu mida kama hii.

Unaweza kuwa mdhamini wa kisa hiki cha kusisimu na chenye funzo kubwa kwa vijana wa sasa katika masuala ya mapenzi.


Nawe waweza kuwa mdhamini wa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

share, like na comment

You Might Also Like

0 comments: