LANGO LA MOTONI CHAPTER 9
SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
Mtunzi: Fred Kihwele 0713317171
CHAPTER 9
Ilipoishia
Mtoto huyu nikamtunza kwa mapenzi ya dhati na mpaka hivi leo ni binti mkubwa na anayesoma kidato cha tatu na jina lake anaitwa SALHA yaani wewe mwanangu. Kwa hiyo ukweli ni kwamba wewe ndio mtoto yule niliyekuwa nikimtunza pale hospitali."
Salha alipatwa mshtuko na ku....
Endelea
Salha alipatwa mshtuko na kuanza kulia kwa mfululizo kilio ambacho kilimfanya na mama yake aanze kulia ingawa yeye hakuwa akilia kwa yaliyomsibu Salha la hasha ila yeye sasa akakumbuka jinsi amilvyompoteza mmewe mtarajia asubuhi ya siku ya harusi yao.
Siku hiyo asubuhi mmewe mtarajiwa alikuwa kwenye bodaboda akiwahi kwenda salon kwa ajili ya maandalizi ndipo akakutana ana ajali hiyo iliyomfanya mama salha kuzirai zaidi ya siku nne akiwa mahututi na aliopoamka akapewa habari ya mimba yake ya miezi minne kutoka kwa sababu ya mshtuko.
Waliendelea kulia kwa muda mpaka pale salha aliponyanyuka na kumwendea mama yake na kumwambia, "
"mama, tambua sijalia kwa sababu ya kuwapoteza ndugu ila nalia kwa furaha kwani pamoja na dunia kuwa na watu wa ajabu wenye matukio ya kutisha na kusikitisha ila bado kuna watu kama wewe wenye kutetea uhai wa watu... Nitakuita mama daima na utakuwa mama daima naamini hata mama na baba watafurahi kuona nikifanya hivyo katika ulimwangu wao wa roho, ila nina hamu ya kumfahamu dada"
"Utamfahamu tu mwanangu muda ukifika, ila kwa sasa hata mimi naumiza kichwa kujua yuko wapi maana ndugu zako hawajaweka bayana yuko wapi na ni wagumu sana kuingilika, ila nitajaribu kutafuta mawasiliano ya shangazi yenu mmoja mbaye yeye hakuwa akikaa sana pale wazazi wako na baadhi ya ndugu zako walipokuwa wakiishi"
"Asante sana mama, nakupenda na amini nipo kwa ajili yako" Alinyanyuka Salha na kwenda chumbani kwake ambako mawazo yalimsonga juu ya dada yake na vifo vya baba na mama na baadae usingizi ukamnyemelea na kulala.
**********
Ben na Samira walionekana wakiwa kwenye gari wakitoka hostel na baada ya kutembea umbali wa kilomita kama 25 hatimaye wakawasili kwenye mji mmoja uliofahamika kwa jina la Moshono na moja kwa moja gari likanyoosha na kwenda kusimama katika mtaa mmoja wa watu waliostaarabika uitwao Ichenga na kupaki mbele ya nyumba moja ya kifahari.
"tumefika sasa Samira" aliongea ben huku akimsaidia samira kushuka kwenye gari kisha wakaisogelea hiyo nyumba na kuingia ndani.
" Kaka Ben hii nyumba ni nzuri sana ila mbona inaonesha hakuna watu" alihoji samira huku wakiingia chumba baada ya chumba katika nyumba hiyo ambayo hata kama ilionesha kuwa imetoka kufanyiwa marekebisho lakini bado ile hali ya uzamani iliifanya nyumba hiyo kuwa bora na ya kuvutia tofauti na baadhi ya nyumba pale mtaani.
"samira unajua ninahofia sana na usalama wa Aunt amina na wewe kwani pale nyumba yenu ilishaharibiwa na pia sina uhakika kama hiyo jumamosi akirudi itakuwa busara kumpeleka pale asije patwa na mshtuko, hivyo mtakaa kwa muda katika hii nyumba ili nimsikie nae atakuwa na lipi la kusema"
"Sijui nikuambie nini ili uuje furaha niliyonayo hapa moyoni mwangu, lakini nina imani baba na mama kokote waliko watakuwa wanakuona na kubfurahi pia, Mungu akupe mafanikio mara mia ya sasa.. asante sana kaka" alihitimisha maneno hayo Samira na kuanza kuangua kilio cha chini chini huku wakielekea kwenye gari..
Ni wakati huu ambapo samira akaanza kurudiwa na picha ya udogo wake akiwa na mama yake kwenye gari akipelekwa shule na sehemu mbalimbali na mara mambo ya hatari yakaanza kumsakama mara baada ya baba na mama kufa katika kisa cha ajabu na hatimaye alivyokuja kuokolewa na aunt amina ambaye sasa kuja kwa samira kumekuwa kama mkosi kwa maisha ya familia hiyo.
Akiwa katika msongo huo wa mawazo alishtushwa na sauti ya Ben ikimwambia " samira, tumeshafika hostel yaani ulikuwa na mawazo sana kwenye gari kuna nini kinakusibu kwani nimekusemesha zaidi ya mara tatu unaonekana kama upo haupo vile"
"kaka nilipitiwa na furaha ya nyumba sasa najua nitapumzika salama na kuisubiri siku ya aunt kurudi, zimebaki siku tatu ila naona ni kama miaka nimemkumbuka sana na nina furaha zaidi kuwa sasa kapona"
"Ok, basi mie nakuacha nafikiri zile hela bado unazo hivyo hakuna shida upande wako, nitakucheki kwa simu mida mida" Alihitimisha Ben na kisha wakaachana na samira yeye akaingia hostel.
Wakati anakaribia mlango wa hostel samira kuna kitu kilimfanya asite kuingia na kuamua kurudi nyuma na kujibana sehemu kwani muda huo giza lilikuwa limeanza kuwa la kumfanya mtu asione vyema.
Akajisogeza hatua kama nne na ku...................
KIsa hiki kitaendelea kesho na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia whatsapp wasiliana nasi kwa whatsapp namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini
KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki
Soma kisa cha 1 mpak cha 8 kupitia Karibu Mbeya
0 comments: