HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Season 9
HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Season 9
Yaliyomo
Baba Pachu ni kijana aliyejaliwa kuwa na mke na watoto wawili na familia yake imekuwa ya furaha na amani kwa muda mrefu.
Pamoja na kuwa na furaha hiyo pia Baba Pachu amejaliwa kuwa na mafanikio makubwa katika kazi zake binafsi na pia ni mfanyakazi wa kampuni moja maarufu sana yautafiti wa madini.
Siku moja akiwa katika mihangaiko yake binafsi nje ya jiji la Mbeya majira ya usiku akiwa chumbani mwake mara anapokea simu ngeni kutoka kwa mtu asiyemfahamu.
Mara ya kwanza ilionekana kama ni WRONG NUMBER lakini baada ya muda ulivyozidi kwenda ikaonekana kuwa sio WRONG NUMBER tena bali ni mtu anayemfahamu fika ingawa yeye hamtambui na nia yake ikiwa haieleweki.
Simu hii ya AJABU ikanza kuipoteza furaha ya baba pachu na hatimaye furaha ya familia nzima, kazini mpaka jamii inayomzunguka kuanza kumwona kama mtu anayeanza kuchanganyikiwa.
Baba Pachu anaanza mkakati wa kutatua tatizo lake na mkakati huo unamfanya baba Pachu kujikuta anapita katika njia zenye visa vya kutisha, majaribu, vioja na heka heka nyingine nyingi zenye maumivu na kuifunza jamii.
ILIPOISHIA
Namshukuru Mungu tulifika nyumbani salama na huwezi amini nyumba ilikuwa chafu sana tukaanza kushusha mizigo na baadae nikamwacha mama pachu akifanya usafi nami nikaingia bafuni kuoga na niliporudi nikachukua simu yangu na kuelekea sebuleni ili niwashe simu yangu na kuangalia TV nione yapi yamejiri kwa siku hiyo.
Nilipowasha simu ziliingia meseji kadhaa kutoka kwa marafiki zangu nikawa nazisoma moja moja na kuzijibu, laaah haula!! moja kati ya meseji zilizoingia nashindwa hata kukuambia..................... .............................. ................?
Endelea
SMS ilisema hivi, " Karibu tena nyumbani mpenzi"
Macho yalinitoka kama nimeonana ana kwa ana na nyoka aina ya Anaconda, nilitetemekea sana na moyo wangu ulijawa na ghadhabu na hasira nyingi sana.
Nikajiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu, Hivi huyu ni nani na anataka nini kwangu? Katokea wapi? Namba yangu kaijuaje?
Kabla sijamaliza kujihoji vizuri maswali hayo, mke wangu alikuja pale sebuleni na kunipa chakula ambacho nilianza kula bila hata ya kuwa na hamu nacho.
Ilivyofika usiku mida ya saa mbili na nusu nilimuaga mama Pachu kuwa natoka kidogo naenda kukutana na marafiki zangu bar ya jirani ambayo haikuwa mbali na nyumbani.
Kweli nilitoka ila nia yangu kubwa ilikuwa ni kununua vocha ili nipige ile namba na niweze kutatua tatizo langu huku nikipata nafasi ya kujua ni nani anayenipigia kila simu.
Nilifika dukani na kununua vocha ya mtandao mmoja unaojulikana sana kwa kutoa offer ya kukopesha wateja wake. Baada ya kuiweka ile vocha ya shilingi elfu kumi na kujihakikishia kuwa nitapiga simu bila kukatisha maongezi yetu, nikaamua sasa kuanza kuipiga ile namba.
Simu iliita zaidi ya mara tano bila ya kupokelewa, uso wangu ulianza kushamiri furaha na kuona kama ushindi unakaribia kwani nilijua kuwa yule dada anayenisumbua ananiogopa, hivyo kwa ujasiri, kiburi na dharau nikaamua kupiga tena kwa mara ya mwisho.
Safari hii mambo yalikuwa tofauti kabisa na nilivyodhania kwani simu iliita kwa muda kidogo halafu ikapokelewa.
Mwee!! mwee!! mwee!! mwee!! niliachia shuzi moja kubwa kama bomu la nyuklia kwani nilisikia sauti ya yule dada akasema hivi.......................... .............................. .............................. ...........................
Je dada yule aliongea nini? Na nini hatma ya Baba Pachu? ... Usikose kisa hiki cha kusisimua kesho mida kama hii.
Unaweza kuwa mdhamini wa kisa hiki cha kusisimu na chenye funzo kubwa kwa vijana wa sasa katika masuala ya mapenzi.
0713317171
0 comments: