Babu amwaga chozi mbeye ya wajukuu
Babu mmoja Mzee sana alienda ishi kwa mwanae wa kike , alie kua ameolewa na amezaa mtoto mmoja . Mzee huyoo alikua ni mtu wa kutetemeka mda wote , na pia alikua haoni vizuri sababu ya ukungu ulokua umetanda ndani ya macho yake , na alikua hawezi tena kutembea vizuri .
Kama familia walikula pamoja kwenye meza ,lakini kwa bahati mbaya BABU na mikono yake ya kutetemeka na macho yake yalimsababishia kutokula vizuri . Punje za mchele mara kwa mara zilikua ziki mwagika wakati akila chakula , wakati akishika Glasi aweze kunywa maji , maji yalimwagika mara kwa mara kwenye kitambaa cha mezani .
Mme wa mwanae na mwanae wa kike wanakasirika kutokana na kitendo hicho cha Babu kumwaga mwaga msosi " baba inabidi tufanye kitu kuhusu hii hali " alisema mtoto , " nimechoshwa na tabia hii ya kumwaga maji , maziwa , kelele za kugongwa gongwa vijiko kwenye sahani , chakula sakafuni kila BABU akiwa anakula " .
Basi mume na Mke wali mwandalia babu meza na kiti pembeni mwa sebule , ili wakati wanakula babu yao ale peke yake wakati wao wakijinoma mezani ! KWakua BABU alisha vunja Sahani nyingi mno , ilibidi MUME amchongee Babu sahani ya mbao kwa kutumia VIFAA vyake vya kazi .
Kuna muda ulifika kila wakati wakula wakimuangalia BABU alikua na chozi usoni kwake , kwakua alikaa mwenyewe muda wakula , na alipo angusha kijiko au sahani hiyo ya mabao MAMA na BABA wa familia hiyo walikua wakali na kugomba huku wakimtolea maneno mabaya .
Mtoto wao wa kiume mwenye umri wa miaka minne alikua akiangalia yote yanayo fanyika mda wa kula kwa babu yake !
Siku moja jioni BABA alimuona mwanae akichezea ubao na vifaa vyake vya kazi , huku akionekana kama ana UNDA kitu flani kisicho eleweka . Alimuuliza kwa upole " mwanagu unatengeneza nn ? Utakuja kuwa fundi mzuri ww " kwa upole na ukarimu mtoto alijibu " baba ona natengeneza SAHANI YA MBAO yakwako na mama ,ili mje kula na hizi sahani ,siku NTAKAPO KUA MKUBWA " , baba alitabasamu na kwenda kuendelea na kazi zake
Maneno hayo yaliweza kuwagusa na kuwachoma wazazi kiasi kwamba waliamua kukaa kimya , machozi yalianza kuwatoka wazazi wake walo kua nyumbani . Japo hakuweza kujibu au kumuongelesha mtoto wao , WALIFAHAMU WANATAKIWA WAFANYE NINI
Ilipo fika mda wa chakula cha jioni BABA alimshika BABU mkono na kuenda nae hadi MEZANI ili wapate kula chakula pamoja ! Siku zote za maisha yake zilizobakia BABU ALIKULA chakula na familia ya mwanae ,na kutoka na sabau zisizo eleweka BABA na MAMA walionekana kutojali tena kijiko ,umma na sahani zinapo angushwa na BABU ! Wala maji akimwaga na kulowesha kitambaa cha meza .
Funzo
wewe ni mfano halisii wa ukionacho , haijalishi hali ya Uhusinao ulio na WAZAZI wako !! Utakuja kuwa MISS sana SIKU wakitoweka DUNIANI , unachotakiwa kufanya ni KUWAPENDA ,KUWA HESHIMU ,KUWAJALI NA KUWATUNZA WAZAZI WAKO !
0 comments: