Ujanja ujanja wa kukata tiketi na kuchagua siti ya kukaa kwenye basi kwa kuangalia jina la sitimeti wa kike yamtokea puani kijana mmoja mkazi wa Mbeya mpenda totozi
Nilipigiwa simu asubuhi na mapema kuwa nahitajika kwenda siku ya pili yake dar kikazi.
Kwa kuwa siku hiyo sikuwa na kazi za kufanya pale nyumbani na ukizingatia maisha ya ubachela yalivyo na uhuru nikaona niamke zangu bila kufanya chochote na kwenda kupata ticket na supu huko town.
Nilipendelea sana kutumia usafiri wa basi kwani usafiri wao wa ndege wanasema bei ndogo ila ticket ni za kung'ang'aniana sana au mpaka upange safari ya muda mrefu kidogo ndio iwe bei ya chini.
Nikafika pale kituo cha mabasi cha mbeya na kwenda ofisi za basi moja nililokuwa nikilipenda sana kulitumia na kisha nikaomba kupata ticket ya siku ya pili yake.
Akaniambia zipo ila ningependa anichagulie siti, akauliza ya upande upi na sehemu gani? Nikamjibu anipe ya dirishani na pembeni yake kuwe na binti mzuri.
Akasema una bahati leo wamekuja mabinti wengi wa chuo na wamekata siti za pembeni kwani wengi hawataki kukaa dirishani hivyo kazi kwako kuchangua jina zuri.
Nikatabasamu na kisha kuchukua ile chart na kuanza kuchagua jina ambalo niliamini ningekuwa linamilikiwa na binti kifaa tena wa ukweli.
Majina kama, jane, mary, salome, neema na mengineyo sikutaka hata kuhangaika nayo kwani nimezoea kuwaona wakawaida na baadhi ya wenye majina hayo walishanipiga kibuti hivyo sikutaka.
Nikaona jina moja limeandikwa Anumye nikaona sasa huyu nisije kukaa naye na akaongea kinyakyusa safari nzima.
Jitihada zangu zilifika kikomo baada ya kuliona jina moja lenye hisia kubwa kwangu na jina hilo sio jingine zaidi ya *Genevive *.
Nikaamini kuwa lazima awe zaidi ya mrembo tena mpole na mweye mikogo yote ya kilimbwende, nikalipia siti na kuondoka zangu.
Siku nzima ilitawaliwa na mawazo juu ya Genevive atakavyokuwa kabla ya kurudi nyumbani kujiandaa vyema kwa kila kitu muhimu kumteka Genevive siku ya pili yake.
Na baada ya hapo nikalala na usiku huo nikawa namwona Genevive yule wa movie za kinaijeria akanijia nikajua kesho yake mambo yatapamba.
Niliwahi kuamka nikajipa usafi wa maana nikaiweka poa ipod yangu, ipad yangu, kindle, Novel yenye jina "how to make a woman feel so proud" camera yangu kisha nikajipulizia manukato mazuri kabla ya kuwahi garini.
Wooow, kufika kwenye basi pembeni ya siti yangu alikaa mrembo mmoja ambaye kwa namna yoyote ile alikuwa ni Genevive .
Nikamsalimia na kukaa nikisubiri mpaka basi liondoke ndio nami nitajifanya kuwa kidume na kuanza kuongea na mtoto nikahisi itakuwa safari moja tamu sana.
Basi likiwa litaka kuondoka mara konda akaja na kumwambia yule binti hii sio siti yako na kumtoa pale, kidogo nimwambie konda umekosea ila nikaona nitulie kwani inaweza kuwa toa chombo leta chombo zaidi.
Ebwana..... Aliletwa bibi mmoja mzee wa miaka kama 60 kasoro vile na kwa unyonge nikachungulia ticket yake na kuona kweli kaandikwa Genevive finunu Mwafilombe.
Hasira ikanijaa na wakati huo tunakaribia kuondoka, kaweka begi lake akatoa maji makubwa na keki mbili akala.
Sikushangaa kufika uyole kanunua Mayai ya kuchemsha 3 na Hindi 1 la kuchemsha na Soda ya kopo (Fanta) akapiga taratiiibu!!
Tumefika Makambako!! Kamtuma konda Chipsi Mayai na wakati huo kanunua korosho pakti kubwa huku
kachukua machungwa 4.
Mimi nikaanza kua na mashaka nae aisee!! Maana bibi anakula na uzee ule meno yapo salama kweli?
Na wakati huo sijapata nafasi ya kusoma wala kufanya chochote maana ananisimulia mambo ya zamani kila akiona kitu.
Tumeingia pale sehemu ya kula kitonga mida ya saa sita hivi tunashuka kula chakula cha mchana maana njaa sasa ilikua inauma na bibi nae anaomba nimnunulie mtindi MHH!!!
Kwa kweli mimi nikaanza kumuogopa yule bibi na kuhofia zile kona za ruaha mbuyuni tutasalimika kweli au atataapika hovyo!!!
Na pia sijamsikia akiomba kuchimba dawa, nikajiuliza au ni uzee?
Muda umefika gari linaondoka nikajua Genevive lazima ataomba kuchimba dawa yaani kwa hali ile lazima atembelee msalani!
Mhh!! Bibi kainuka kavuta begi lake kapekua pekua karudisha kukaa namuona kashika Pande la muogo wa kuchoma mfuko wa
karanga mbichi na maji ya Kilimanjaro makubwa!!
Kwenye mfuko wa shati kuna biskuti za chokleti. Nikainuka taratibu na kukaa siti moja mbele yangu ambayo abiria wa siti ile alishukia iringa na hakuna abiria mpya aliyekaa pale.
Nikawasha ipod yangu na mziki wenye sauti kwani nilihisi atakapo anza kupigana na abiria kwa kutaapika mle ndani au shuzi zikianza kukomaa mimi nisiwe mmoja wa watakao shangalia ugomvi?"
Mpaka tunashuka ubungo sikuamini na nilipomchungulia nikaona anauliza bei za pweza pale nje akiwa na ndugu zake, nikakimbia kuwahi daladala maana pengine anatengeneza silaha za maangamizi na angeweza kulipua kitu pale.
Kweli jina Genevive kamwe sitalisahau maana safari hii imekuwa ya vioja..... ........
Whatsapp 0713317171
0 comments: