Kumbukeni haya wapendwa dada zangu kabla ya kufikiria kuingia kwenye mahusiano

15:33:00 Unknown 0 Comments



1} Kamwe usimtegemee mpenzi wako wa kiume kama baba yako, jaribu kumwonyesha ajue kuwa kabla ya kukutana ulikuwa unajiweza na hata ukiachana nae utaendelea kujiweza.

2} Usimkane mpenzi wako kwa kuwa yeye ni masikini sasa, kwani tajiri wa leo ni masikini wa kesho na mtu hawezi kuwa fukara maisha yake yote, Utajiri ni sawa na vitambaa vya meza vinabadilishwa kila siku

3} Usiseme kuwa hakuna wanaume wa ukweli katika maisha yako wakati wewe kila kitu kwako ni feki, Kumbuka utampaka mtu kulingana na wewe ulivyo na maisha yako, ukiwa feki utakutana na feki mwenzako... kuwa real

4} Usiseme wanaume wanautaka mwili wako tuu wakati mavazi yako yanauonyesha mwili wako kila sehemu zikiwa wazi. Jinsi unavyo vaa ndio watu wanavyo kuthaminisha na kukulinganisha na tabia zako.

5} Usilalamike kuwa umekaa nae kwenye mahusiano kwa muda mrefu lakini bado hataki kuyafanya mahusiano yafungue ukurasa mpya
wa kuwa mme na mke, Dada yangu sio kila mahusiano ni lazima yaishie kwenye ndoa.

6} Usiseme wanaume wote wako sawa baada ya kuumizwa, Kumbuka hata vitabu vya dini
vinasema: kama ambavyo nyuso zetu zatofautiana ndivyo hata tabia zetu zinavyotofautiana.

7} Usiyachukie mahusiano kwa kutokana na kumbukumbu zilizopita, zaidi kumbuka kila
mahusiano yana funzo la kukupa, na usifunge macho kwa kuogopa kuona mambo magumu kwani unaweza kuja kufumbua macho na
kugundua kuna mazuri yalipita na bila wewe kuona... Usikate tamaa katika mapenzi

8} Usikimbilie katika kuolewa kwani kama Mungu ajuavyo siku yako ya kuzaliwa na ya kufa hivyo hivyo anafahamu kila mipango juu
yako kwani sisi ni kama sisimizi machoni mwake, Muda wako wa kuolewa utafika kwa wakati kama ilivyo kwa kifo kinavyokuja bila
hodi.

9} Unasema wanaume hawako siriazi na wewe, wakati historia yako na matukio yako ya nyuma
yako kwenye vyumba vya hotel, simu za wanaume mabali mbali na hapa facebook una marafiki 5000 na kila picha yako inaonyesha
jinsi ulivyo na wasifu mbaya, kila gari wewe umefanya gesti na pia kila mtandao upo na una wanaume wengi wengi umejianika vya kutosha, Kitu ambacho kinauonyesha umma kuwa umeathirka kifikra na msimamo

10} Kila siku mbukuka mambo yanatokea vile Mungu atakavyo....


kama una swali niulize kupitia whatsapp 0684868191

You Might Also Like

0 comments: