LANGO LA MOTONI CHAPTER 14
SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
CHAPTER 14
Ilipoishia
"Sawa boss" Aliongea kijana huyo kwa uoga huku akimchukua ben ambaye bado alikuwa hajaamka kutokana na sindano ile.
Muda mfupi baadae vijana wale walifika pale njia panda walikomchukua ben na kumwingiza kwenye gari lake na kisha wao wakatokomea kusikojulikana wakimwacha ben akiwa pale ndani ya gari lake na wakati huo ilikuwa inakaribia kumi na moja kasoro za alfajiri.
Saa moja kasoro za asubuhi ben ali........................... .............................. ...
Endelea
Saa moja kasoro za asubuhi ben alishtushwa na mtu aliyekuwa akigonga dirisha la gari lake kwa fujo, ben akajitahidi kuufungua mlango ule ingawa hakuwa na nguvu kabisa na hatimaye dada yule aliyekuwa akigonga akafanikiwa kuingia ndani.
Dada alijaribu kumsemesha ben lakini alishindwa kwani ben alionekana kukosa fahamu kabisa kama vile alilewa sana au kula madawa ya kulevya vile, dada akaanza kujisemesha mwenye.
" jana mimi ndio nilikuwa mtu wa mwisho kumhudumia ben, sasa iweje atoke pale na kuja kuishia hapa njia panda, au kuna kitu kala kikamfanya aishiwe nguvu maana inaonekana alivyotoka pale aliishia hapa tuu" alijisemesha dada huyo mhudumu wa hoteli aliyokuwa akinywa ben jana yake jioni kabla ya kukumbwa na yaliyomsibu na kumfanya awe vile.
Dada ule akamsogeza pembeni ben na kuligeuza gari kila akalipeka mpaka hoteli ni baada ya kudadiliana na meneja wake wakaona ni vyema wampe chumba apumzike na baada ya fahamu watoe taarifa polisi kwa kuwa ni mteja wao wa siku nyingi.
Aunt amina aliamka kwa kuchelewa siku hiyo na kumkuta samira nae akiwa kalala fofofo sebuleni kwenye sofa. Hakutaka kumsumbua akamwacha na kuendelea na majukumu ya asubuhi mpaka pale samira alipokuja kuamka na wote wakajumuika mezani kwa asjili ya kifungua kinywa.
" samira mbona uliamua kuja kulala sebuleni"
"aunt sikuwa na usingizi hivyo nikaona ni vyema nije kuangalia thamthiliya ya simu ya ajabu, ni muda nilikuwa sijatulia na kuiangalia tangu mambo haya yawe mazito"
"pole mwanangu samira, lakini pia unatakiwa kumshukuru Mungu kwa kuwa sasa mambo haya yamefika ukingoni na tumshukuru Mungu kwa kutupa Ben ambaye amekuwa ndugu yetu sasa"
Baada ya aunt amina kulitaja neno Ben, samira alijikuta tena akiwa katika dimbwi zito la mawazo mpaka pale aliposhtuliwa na mkono wa aunt amina ukimgusa na kumwambia "mwanangu sasa naomba basi unichukue mpaka pale kaburini kwa mme wangu na baada ya hapo nimpitie mwalimu jack na baadhi ya majirani ili kuwapa asante na kisha kuwaambia wapi nilipo kwa muda"
"sawa aunt" alihitimisha maneno hayo samira na kisha akaingia chumbani kujitayarisha na muda mfupi baadae walikuwa kwenye daladala wakielekea mtaa waliokuwa wakikaa kabla ya kusambaratishwa kutokana na hila za mzee zombo a.k.a bilionea wa ukubwani.
Samira hakuwa na furaha kabisa kwani kila alipojaribu kumpigia au kumtumia sms ben haikujibiwa kapatwa nahofu na kujua labda kuna jambo limempata.Walifika kaburini na baada ya hapo waliwatembelea baadhi ya majirani na kituo cha mwisho kilikuwa ni kwa mwalimu jack.
Walipofika kwa mwalimu jack aunt amina alishikwa na mshangao kwani badala ya mwalimu jack kumlaki aunt amina kama wengine walivyofanya yeye alimkimbilia samira na kumwangukia miguuni na kuanza kulia akisema,
" mwanangu samira naomba nisamemeh, najuta kwa hasira niliyokufanyia kumbe hukufanya lolote ila zilikuwa ni hila mme wangu baada ya kushindwa kulala na wewe ndio akaona atumie mwanya huo wa kukusingizia, samira nisamehe, nimekutafuta tangu siku nilipokupeleka kituoni na sijawahi kukuona wala kupata taarifa ya kuwa uko wapi nisamehe samira"
Wakati huo samira alikuwa akitokwa na machozi mfululizo kama vile mto wa iwambi ulikuwa ukititisha maji, aunt amina alimsogelea mwalimu jack na kumnyanyua na baadae wakaingia ndani.
Samira alisimulia kisa kizima jinsi ambavyo mmewe na mwalimu jack alikuwa akimtisha na baada ya hapo wakawa wameyamaliza huku kila mmoja akimsimu samira kwa jinsi alivyoweza kukabiliana na hilo.
Ilipofika mida ya jioni samira na aunt amina sasa waliondoka na wakawa njiani kurudi kwao ingawa samira bado alikuwa na hofu kubwa juu ya ben kwani mpaka muda huo alikuwa hapatikani kwenye simu.
Walipokaribia nyumbani kwao wakaona washuke na kupita njia ya nyuma ya nyumba, walipita taratibu lakini walipokaribia waligutushwa kuona kuna gari moja dogo limepaki kwenye kichaka bila hata ya kumsemesha kitu samira alimbana aunt amina mdomoni ili asiongee kitu na kumnong,oneza aunt amina " aunt hapa tumevamiwa nafikiri kuna watu nyumbani sasa lala hapa bila kuongea kitu nakuja"
Samira akajivuta taratibu na alipokaribia akaona kuna watu watatu wako nyuma ya mti mmoja na mmoja alikuwa akivuta sigara na walikoliweka gari na wao kusimama kamwe kama ungepita mlango wa mbele usingewaona.
Wakati samira anajiandaa kumrudia aunt amina mara aka.......................
KIsa hiki kitaendelea KESHO na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia Telegram wasiliana nasi kwa Telegram namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini
Asante sana mdhamini mkuu wa kisa hiki www.karibumbeya.com ambaye anakupa nafasi ya kutangaza biashara yako bure kwa kujisajili kupitia tovuti yao na pia unaweza kuuza na kununua mahitaji yako ya msingi
KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki
0 comments: