LANGO LA MOTONI CHAPTER 15
SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
CHAPTER 15
Ilipoishia
Samira akajivuta taratibu na alipokaribia akaona kuna watu watatu wako nyuma ya mti mmoja na mmoja alikuwa akivuta sigara na walikoliweka gari na wao kusimama kamwe kama ungepita mlango wa mbele usingewaona.
Wakati samira anajiandaa kumrudia aunt amina mara aka.......................
Endelea
Wakati samira anajiandaa kumrudia aunt amina mara akashtuka kuona kuna mtu akimnyemelea aunt amina, samira akajificha nyuma ya ua moja kubwa na kuitoa chupa ndogo ya pafyumu yake na kumnyemelea yule jamaa bila kuona na kumshika bega.
Yule jamaa alipogeuka alipokelewa na pafyumu aliyopuliziwa machoni na samira na kisha kujitupa chini huku akilalamika maumivu makali yaliyotokana na pafyumu hiyo kuathiri macho na kumpa mwanya samira kumchukua aunt amina na kutokomea kwenda kujificha mbali na pale.
Wenzake na yule kijana walifika pale na kumkuta mwenzao akiwa anagalagala kwa maumivu na walipomuuliza aliwaambia kuwa amemwona mtu ila hajamtambua kwani alimpilizia kitu machoni na kukimbia.
Ikawabidi waondoke haraka kwani wakahisi kuwa majirani angeweza kuwashtukia na hivyo kuwaharibia mpango wao waliotumwa na boss wao.Samira na aunt amina baada ya kufanikiwa kutoka pale waliendelea kukimbia kuelekea mjini wakipitia njia za mkato na saa sita kasoro za usiku waliingia nyumbni kwa mwalimu jack.
Samira alijitahidi kumtafuta ben usiku ule akitumia simu ya mwalimu jack kwani yake aliipoteza akiwa anawakimbia wale watu lakini jitihda za kumtafuta ben hazikufanikiwa. Asubuhi walipoamka mwalimu jack na mmewe waliwandalia chakula na baada ya hapo sasa wakaanza kusimulia kisa kizima.
" sasa unafikiri nini itakuwa hatma ya haya yote aunt amina? " alihoji mme wa mwalimu jack huku nae akiwa anatetemeka kutokaa na yale madhambi aliyommfanyia samira kwani bado yalikua yakimwandama, kama wasemavyo kuwa "binadamu hauwezi kuyakimbia makosa yako kwani huwa kama kivuli chako na makosa hayo hata ukijificha yanajua wapi kwa kukupatia kwani yanakuwa ni moja ya sehemu yako labda uamue kuyasafisha"
" Ki ukweli shemeji mimi nataka kuondoka hili eneo niende mbali kusikojulikana nikaanze maisha upya, na sababu ya kuja jana hapa ni kwamba kuna ile nyumba iliyoungua moto pamoja na kile kiwanja cha jirani na kile kiwanja chenu pale nilipopanda mihogo,naomba mnisaidie kuuza na fedha mnitumie, lakini pia kwa kuwa huko niendako sijui kama nitaanzaje kuishi nilikuwa naomba mniazime fedha na mtakapouza maeneo mtachukua deni na kunitumia yangu itakayosalia"
" kutokana na hali ilivyo hatuna jinsi zaidi ya kutafuta hata kwa kukopa kwani hata sisi kifedha tumeyumba ila ngoja niende kwa mangi yule rafiki yangu nione nini kitatokea, mke wangu nafikri hatuna jinsi" aliongea mme wa mwaimu jack huku akinyanyuka na kwenda mtaa wa pili.
Siku ya pili asubuhi mwalimu jack na mmewe waliwasindikiza samira na aunt amina kwa gari lao ili watu wasiwaone mpaka kijiji cha ne kutoka pale kwao na kuwapakia kweye basi ambalo muda mfupi baadae liliondoka na kuuacha mji huo huku samira na aunt amina wakiwa ndani yake.
Ben alikaa pale hotelini kwa siku mbili bila ya kuwa na fahamu nzuri na siku hii aliamka na kujikuta akiwa na nguvu na baada ya kuletewa chakula alimwita dada yule aiyekuwa akimuhudumi na kumuuliza nini kilimtokea.
Alisimuliwa mkasa wote na baada ya hapo akajianda ili aondoke kwenda kwake, muda mfupi badae akaingia kwenye gari lake na kuichukua simu yake na kugundua kuwa haikuwa na chaji hivyo akangoza moja kwa moja mpaka nyumbani na kuichaji.
Alipoiwasha alikutana na sms kibao kutoka kwa samira na kila alipojaribu kuitafuta simu ya samira haikuwa tena hewani. Akondoka na kwenda mpaka nyumbani kwa kina samira akakuta hakuna dalili za watu. Alihangaika siku hiyo kwenda huku na kule lakini hakukuwa na daili ya samira wa aunt amina.
Siku ya pili akarudi tena nyumbani kwa kina samira lakini haukuwa a dalilli ya wao kuwepo akiwa katika harakati za kujua nini kimewatokea akawa amezunguka na kwenda nyuma ya nyumba hiyo na kuona kuna chupa ya pafyumu na simu ikiwa pale chini.
Alipoichukua na kuiangalia akagundua kuwa ni ya samira bila hata ya kutarajia akajikuta akisema " maskini wameshamteka tena mtoto wa watu " kisha kaondoka haraka eneo hillo.
************
Mzee zombo kama kawaida yake alikuwa ndani ya bar moja maarufu sana pale mtaani kwake na siku ya leo alikuwa akisherehekea siku yke ya kuzaliwa ingawa hakuna aliyekuwa na uhakika kama kweli siku hiyo ndiyo siku maalumu ya yeye kuzaliwa kwani mwaka uliopita alishrehekea siku hiyo tarehe tofauti na mwezi tofauti na sasa.
" Happy Birth day mzee zombo"
" Happy birth day to you too rafiki" haya ndio baadhi ya majibu ambayo yalimfanya kila mmoja aliyehudhuria halfa hiyo atokwe na kicheko cha tumboni au hata kutoka nje na kucheka na kurudi ili kutoonekana na mzee zombo na kisha kutimuliwa kwenye sherehe hiyo
Wakati sherehe hiyo inakaribia ukingoni mzee zombo aliwaaga wageni wake na moja kwa moja akaingia kwenye gari lake akiwa na binti mmoja ambaye alimpata katika hafla hiyo na akawa sasa anaondoka kwenda kutafuta hoteli ya kulala na mrembo huyo.
Akiwa barabara kuu kuna dada mmoja aliiyeonesha kuwa mrembo na mwenye umbile la kimahaba hasa baada ya taa za gari kummulika na alikuwa akasimamisha gari la mzee zombo, mzee zombo akafanikiwa kuingia katika mtego huo wa tamaa na hata kabla ya gari kusimama vizuri alishtuka kuona akizingirwa na......................
KIsa hiki kitaendelea JUMATATU na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia Telegram wasiliana nasi kwa Telegram namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini
Asante sana mdhamini mkuu wa kisa hiki www.karibumbeya.com ambaye anakupa nafasi ya kutangaza biashara yako bure kwa kujisajili kupitia tovuti yao na pia unaweza kuuza na kununua mahitaji yako ya msingi
KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki
0 comments: