LANGO LA MOTONI CHAPTER 16
SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
CHAPTER 16
Ilipoishia
Wakati sherehe hiyo inakaribia ukingoni mzee zombo aliwaaga wageni wake na moja kwa moja akaingia kwenye gari lake akiwa na binti mmoja ambaye alimpata katika hafla hiyo na akawa sasa anaondoka kwenda kutafuta hoteli ya kulala na mrembo huyo.
Akiwa barabara kuu kuna dada mmoja aliiyeonesha kuwa mrembo na mwenye umbile la kimahaba hasa baada ya taa za gari kummulika na alikuwa akasimamisha gari la mzee zombo, mzee zombo akafanikiwa kuingia katika mtego huo wa tamaa na hata kabla ya gari kusimama vizuri alishtuka kuona akizingirwa na......................
Endelea
Akiwa barabara kuu kuna dada mmoja aliiyeonesha kuwa mrembo na mwenye umbile la kimahaba hasa baada ya taa za gari kummulika na alikuwa akasimamisha gari la mzee zombo, mzee zombo akafanikiwa kuingia katika mtego huo wa tamaa na hata kabla ya gari kusimama vizuri alishtuka kuona akizingirwa na watu waliomchukua na kumwamishia kwenye gari jingine lililokuwa limefichwa na kuondoka eneno haraka huku mmoja akiwafuata na gari la mzee zombo.
" Oya masela wangu kuna nini tena kama ni mtonyo niambie niwape na mie mniache nisepe na road" aliongea mzee zombo na kuwafanya watu wale waliovalia mask waangue kicheko kwani wote walikuwa wakisikia ubabe wa mzee zombo lakini muda huu walishangaa kuona kalainika na mbaya zaidi ni kuwa alishaachia ushuzi wa hofu zaidi ya mambo kadhaa.
Hakuna aliyemjibu na gari liliongeza mwendo na ahatimaye lilikomea nyuma ya jumba moja kukuu kukuu ambalo lilikuwa limesahaulika kwa muda kidogo na wakamshusha na kumweka kwenye kiti kimoja wakimfunga kitambaa mdomoni kumfanya asiongee na kile cha machono ili asione chochote kisha vijana wale wakaondoka.
Asubuhi majira ya saa nne kasoro gari moja dogo la kifahari lilimshusha mtu mmoja pale na moja kwa moja akaingia na kuelekea alikofungwa mzee zombo.
"Mfungue kitambaa" aliamuru mama huyo aliyekuwa ameingia chumba hicho
" Whaaat!!!!! the hell is world, Nagris umerudi lini na je wewe ndio uliyeamuru nifungwe hapa"
" ha ha ha ha acha kujifanya unajua kiingereza na usije ukarudia tena na kufikiri mimi ni yule Nagris wa enzi zile wa utani na kupenda hadithi zako wakati nafanya kwa kaka yako. nimekuja na ajenda moja tuu.
Nasikia unamsaka Samira ili umuue sasa nakupa siku nne uwe umemtafuta na kumpa kinachomhusu au mimi nitadeal na wewe mpaka kufa, na pia nataka kujua yule mtoto wa marehemu kaka yako aliyekuwa kazaliwa kabla ya muda wake nijue yuko wapi, sitaongea na wewe kwa kukutana ana kwa ana tumia namba hiii" alihitimisha Nagris nakumpa kikaratasi na kisha akaamuru wamfunge tena na kuondoka akiwa kampa onyo la mtu yoyote kutojua kama yeye yupo hapo jijiji
Nagris alikuwa msimamizi mkuu wa kampuni nne za baba samira katika upande wa mahesabu na kwa siri walikuwa na uhusiano wa kimapenzi ambao ulianza kujengeka midomoni kwa wafanyakazi wa baba samira.
Mama samira aliposikia nakawa kaweka mtego wa wawili hao kudakwa lakini kutokana na intelejensia imara ya baba samira akawa kaudaka mpango mzima na kumtengenezea kesi nagris pale ofisini na kumwamishia jijini Londoni huku akifungua kampuni na kumpa hisa na kuendelea kuwa na mahusiano ya siri.
Dada huyu alipendwa na watu wengi kutokana na utendaji wa kutukuka katika majukumu yake na pia alimpenda kila mmoja kama amambavyo yeye aliamini kuwa kumfanya mtu afurahi na kumsaidia katika kutatua baadhi ya kero zake ni zaidi ya sadaka.
Usiku wa siku hiyo mzee zombo alichukuliwa na walipofika karibu na mitaa yake akapewa gari na vijana wale wakapotelea kusiko julikana,
" duuh yule mwanamke kawa gaidi sijawahi ona, mtu mzima napigwa biti nimelegea kama mlenda wa tukuyu, ama kweli kila kiumbe kina udhaifu wake... sasa nifanyeje maana hatakiwi mtu kujua nitachekwa.. ila ngoja mie ndio zombo no none can immediate me" aliongea huku akiwa na maana ya intimidate na kisha akaingia ndani na kujitupa kitandani.
****************
"Salha,Salha mwanangu salha" ilisikika sauti ikimwita salha na muda mfupi baadae salha akaitika kutoka nje na kuja pale ndani. Walikaa na mama wakaongea na jambo kubwa lilikuwa ni juu ya kuanza kuwatafuta samira na aunt amina popote walikokuwa na kuwa siku ya pili yake kwa kuwa ni siku ya mapumziko basi wasafiri mpaka kijiji walichoambiwa kuwa aunt amina yupo.
Siku ya pili walifanikiwa kufika katika kijiji hicho wakiwa wamekaa sehemu wanajiandaa kuulizia kwa aunt amina mara salha alishtuliwa kuona mtu akimshika bega na kwa furaha mtu huyo akasema....................... ......
KIsa hiki kitaendelea KESHO na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia Telegram wasiliana nasi kwa Telegram namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini
Asante sana mdhamini mkuu wa kisa hiki www.karibumbeya.com ambaye anakupa nafasi ya kutangaza biashara yako bure kwa kujisajili kupitia tovuti yao na pia unaweza kuuza na kununua mahitaji yako ya msingi
KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki
0 comments: