LANGO LA MOTONI CHAPTER 17

08:03:00 Unknown 0 Comments


SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU

LANGO LA MOTONI 

CHAPTER 17

Ilipoishia


"Salha,Salha mwanangu salha" ilisikika sauti ikimwita salha na muda mfupi baadae salha akaitika kutoka nje na kuja pale ndani. Walikaa na mama wakaongea na jambo kubwa lilikuwa ni juu ya kuanza kuwatafuta samira na aunt amina popote walikokuwa na kuwa siku ya pili yake kwa kuwa ni siku ya  mapumziko basi wasafiri mpaka kijiji walichoambiwa kuwa aunt amina yupo.

Siku ya pili walifanikiwa kufika katika kijiji hicho wakiwa wamekaa sehemu wanajiandaa kuulizia kwa aunt amina mara salha alishtuliwa kuona mtu akimshika bega na kwa furaha mtu huyo akasema.............................


Endelea


Siku ya pili walifanikiwa kufika katika kijiji hicho wakiwa wamekaa sehemu wanajiandaa kuulizia kwa aunt amina mara salha alishtuliwa kuona mtu akimshika bega na kwa furaha mtu huyo akasema, " mbona nimekutafuta sana niambie nini kimekukuta, ulikuwa wapi ? ".

Salha pamoja  na mama yake walishikwa na mshangao jambo lililomfanya ben ahisi kuchanganyikiwa sana kwani tangu siku samira alipotoweka amekuwa mtu wa kumtafuta bila ya mafanikio na kuishia kunywa pombe bila nidhamu akijua samira kauwa na wale watekaji wake.

Mama yake salha hakutaka hata kuongea neno na kuondoka eneo hilo akijua kijana huyo atakuwa kawachanganya. Wakafika mpaka kwenye duka moja kubwa na kumuulizia aunt amina na kwa bahati nzuri kumbe walikuwa nje ya duka la mmewe na mwalimu jack.

Akawachukua na kuwapeleka nyumbani na baada ya kufika huko wakasimuliwa mkasa mzima wa maisha ya aunt amina  samira na mwalimu jack,  kwani mwalimu jack siku hiyo alikuwa nyumbani hivyo walipokelewa na kupewa kisa kizima kwa ufasaha.

Lakini mama yake na salha akajikuta akishtuka baada ya kukumbuka kitu na kumwambia mwalimu jack, kuwa wakiwa pale kituoni kuna mtu aliwavamia kama vile aliwafannanisha akitaka kujua tulikuwa wapi. 

Bila hata ya kusubiri waliamka wote na kwenda mpaka eneno hilo na kwa bahati nzuri wakamkuta ben akiwa bar jirani akilewa pombe kama mtu aliyepoteza tumaini fulani.

" nilijua atakuwa ni huyu kijana kwani amewasaidia sana samira na aunt amina na siku waliyoondoka alikuwa hapatikani kwenye simu na wao walitaka kuawa hivyo walikimbilia kwangu na ndio tukawasaidia waondoke hapa kijijini kwa siri, kijana huyu anaitwa Ben"

wakaongea nae ingawa alikuwa kalewa lakini aliposikia habari ya samira na salha akajikuta akipata nguvu na wote kwa pamoja wakakubaliana siku ya pili yake asubuhi waondoke mwalimu jack, mama salha, salha na ben ili waende huko aliko aunt amina na samira.

Mzee zombo alionekana nje ya hoteli moja yenye hadhi akinywa  kinywaji chake lakini siku ya leo hakuwa yule zombo wa majigambo wala utani, na kila mara alijaribu kuipiga simu moja ambayo ilionesha kutokuwa hewani na kuishia kujisemesha, " duuh huyu mkuu wa operesheni mbona hapatikani maana ni muhimu sana awepo hapa"

Dakika chache baadae walikuja vijana wanne na kuizunguka meza yake na idadi yao kufikia watu watano na kuna mazungumzo yaliendelea pale kwa takribani dakika 45 na baada ya hapo wote wakaondoka na sasa wawili wakaondoka na gari jingine na wawili wakawa na mzee zombo.

" sasa ndugu yangu kiwi hii ni hali ya hatari kwani kuanzia sasa No Playing yani hakuna mchezo tunatakiwa kuwa makini kwani nagris kajiandaa na nafikiri atatuumbua" aliongea maneno hayo mzee zombo ambaye pia alikuwa akiufurahia mkakati wa kupewa walinzi na ule mwingine wa siri ambao haukusikika.


Saa nne na nusu siku ya pili gari moja dogo aina ya mark x nilionekana likitembea kwa mwendo wa kasi kuelekea makao makuu ya mji wa kilolo, liliposimama gari hilo mbele hotel moja kubwa pale kijijini alishuka ben, mwalimu jack, mama salha na salha mwenyewe na wote wakaingia kupata kifunguakinywa.

Wakiwa pale mwalimu jack akwa tayari ameshawasiliana na unt amina ambaye alikuwa njiani akija huku wakiwa wanaendelea kula mara simu ya mwalimu jack iliita na akatoka nje kwenda kuongeakwai ni mewe baba jack alikuwa akipiga.

" mama jack, kuna mgeni hapa anashida na aunt amina anaitwa nagris hivyo ataomba kuongea naye"

 "sawa baba jack ila bado aunt amina hajaja, akifika nitampa ujumbe huu pia, sisi tumefika salama baba  jack" alihitimisha maneno hayo na kurejea hoteli mwalimu jack

Muda mfupi baadae samira na aunt amina walifika pale na hata bila ya utambulisho aunt amina alitambua kitu, akamgeukia samira na kumkumbatia na wote wakaanza kulia na mara salha akajikut akiwakimbilia na kuwakumbatia.

" damu ni nzito kuliko maji,  hatimaye wamekutana" aliongea mama salha huku nae akitokwa na machozi baada ya kumshuhudia salh na samira wakikumbatiana kwa furaha huku machozi ya furaha yakiwatoka.

Baada ya hapo walikaa kwa muda na kujadili mengi na pia mwalimu jack akawa tayari kashamwambia aunt amina juu ya simu na wakaongea na kukubaliana kuwa kutokana na umuhimu wa jambo alilotaka kuwaambia basi samira na aunt amina waongozane na kina ben mpaka kijijini kwa kina mwalimu jack.

Safari ikaanza na saa moja kasoro za jioni wakawa wamefika na baada ya kuoga na kupata chakula chajioni mwalimu jack, mama salha na aunt amina wakaongozana mpaka hotel aliyokuwa kafikia nagris na wakakutana.

Nagris akawasimulia mkasa wa wake na baba samira na kusema kuwa sasa alikuwa anahitaji kuja kumsaidia samira kurudisha mali zake zote zilizopo mikononi mwa baadhi ya ndugu wasio na huruma hivyo wakakubaliana kuwa siku ya pili yake waje wakiwa na watoto samira na salha ili awaambie nini cha kufanya.

Kilikuwa ni kikao kizuri sana na wote wakafurahi na baada ya masaa mawili baadae wote wakaondoka kurudi kwa mwalimu jack wakimwacha nagris akiwa pale na kila mmoja alivutiwa na moyo wa nagris na kusema "angekuwa kimada mwingine asingewakumbuka watoto hawa".

 Usingizi wa siku hiyo nyumbai kwa mwalimu jack ulikuwa wa kukumbukwa kwani kila mmoja alilala kwa amani na nuru ya matumaini mapya kwa watoto salha na samira ikionekana.

Siku ya pili assubuhi walijiandaa na kwenda mpaka hotelini pale ambako walikaa kwa dakika kadhaa bila ya nagris kutoka wala  kupokea simu, hivyo mama salha akaona ni bora aende akamgongee mlangon wajadili mapema ili nae awahi kurudi kijijini kwake aendelee na ajira yake kwani siku hiyo alitakiwa kuingia mmchana pale hospitalini. 

Alipofika pale kauona mlango ukiwa wazi na alipochungulia ndani akamshuhudia nagris akiwa kalala juu ya dimbwi la damu na hata kabla ya kupiga kelele za msaada wahudumu wa hoteli hiyo walishamwona mama salha wakapiga simu polisi na muda mfupi baadae mama salha alikuwa nyuma ya krandinga akipelekwa polisi.

Wakati polisi wakiondoka ali................................................................



KIsa hiki kitaendelea KESHO na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia Telegram wasiliana nasi kwa Telegram  namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini

Asante sana mdhamini mkuu wa kisa hiki www.karibumbeya.com ambaye anakupa nafasi ya kutangaza biashara yako bure kwa kujisajili kupitia tovuti yao na pia unaweza kuuza na kununua mahitaji yako ya msingi

KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki

You Might Also Like

0 comments: