LANGO LA MOTONI CHAPTER 18
SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
CHAPTER 18
Ilipoishia
Alipofika pale kauona mlango ukiwa wazi na alipochungulia ndani akamshuhudia nagris akiwa kalala juu ya dimbwi la damu na hata kabla ya kupiga kelele za msaada wahudumu wa hoteli hiyo walishamwona mama salha wakapiga simu polisi na muda mfupi baadae mama salha alikuwa nyuma ya karandinga akipelekwa polisi.
Wakati polisi wakiondoka ali........................... .............................. .......
Endelea
Wakati polisi wakiondoka alionekana mtu mmja akipita upande aliokuweepo mwalimu jack, mwalimu jack akawa kama amegundua kitu ingawa mtu yule hakuonesha sura lakini mwendo wake ulikuwa kama wa mwanaume aliyewahi kuonana nae akajitahidi kwenda haraka amfuate amuone lakinin mtu huyo alipotelea kenye lango moja na mwaimu jack akashindwa kulifunua na kurudi harak kuomba msaada japokuwa waliporudi mtu huyo hakuwepo tena eneo lile.
" jamani huyo mtu ni kama nimewahi kumuona, ingawa hakunipa nafasi ya kumwona vyema" aliongea mwalimu jack na mazungumzo yao yakakatishwa baada ya ben kuwasili eneo hilo kwani alipokea ujumbe kutoka kwa samira.
" nafuu umekuja maana kuna mambo yameetokea hapa, hali ya nagris inatisha na kapelekwa hospital sijui kama atapona, tumwombee"
" mbona haya mambo sasa yananitisha kabisa" halihoji ben na wakaondoka eneo hilo mpka kituo cha polisi ili kujua hatma ya mama salha ingawa walinsindwa kumwekea dhamana kutokana na kesi yake kuwa ngumu na hatimaye wakaishi kuondoka kwenda hospital.
Nagris aliwekwa katika chumba maalumu na kupewa huduma ya kwanza na hali yake ikawa ikionesha kuna matumaini na hakuna aliyeruhusiwa kumwona hivyo wakaishia kuondoka na kurudi nyumbani.
" Hakika maisha yako dada na ya aunt amina yamekuwa .magumu kwa binadamu wa kawaida kusimuliwa ila Mungu naamini yuko upande wetu na kuna siku haya yote yataisha" aliongea salha huku akilia sana
"sijui baba aliwakosea nini ndugu zake yaani kila nikifikiri kuwa ndugu wanaweza kukufanyia hivi nakosa kabisa imani ya kuamini kuwa kuna siku nitakuja kuwa salama" yalikuwa maneno ya samira ambaye alionesha kukata tamaa
" wanangu bado tunasafari ndefu hivyo msikate tamaa sasa nfikiri kilichobaki sasa ni sisi kuondoka na kenda mbali kwani hata huyu ben nae simwamini kwani naona labda watu wanatufuata kwakujua tupo nae bila ya yeye kujua mbona jana tumekuja kwa siri au laba watu hao walitaka kumtafuta nagris pekee, tutajuaje kama na sisi hawatatufuta, salha pia na wewe sasa ushafahamika hivyo utakuwa hatarini pia" aliongeza aunt amina
" Kwa kweli mie yule mtu pale hospitali bila ya ben kuja mapema nilihisi ni yeye kwani walikua wanafanana sana tembea" alisema mwalimu jack
" hapana!! hapana!!! hapana! mimi nakataa kwani haiwezekani mtu aliyetusaidia muda wote huo aje leo atake kukudhuru mimi hilo sitaamini"
" samira uko sahihi lakini binadamu hawatabiriki mwanangu"
"sawa sawa mwalimu jack mwambie huyo bado mtoto, kumbuka sio kila mtu kumwamini ila tunaushukuru msaada wake na tuwemakini pia" alihitimiha aunt amina
Nagris alikaa hospital kwa zaidi ya wiki moja katika chumba maalumu tena chini ya uangalizi wa jopo maalumu la madaktari. Leo hii ilikuwa ni siku ya pili tangu ahamishiwe katika chumba cha kawaida na watu wengi walikuwa wakija kumtazama.
Saa nane kasoro za mchana nesi mmoja alikuja na kumwomba ampe dawa na kumchoma sindano na kisha kuondoka. Nagris akaanza kuona macho yakiishiwa nguvu huku akikosa pumzi na mikono inakuwa mizito na kila akijaribu kupaza sauti kuomba msaada akishindwa na muda mfupi baadae alifariki na kuiaga dunia.
Ilikuwa ni pigo kubwa kwa inspekta rose ambaye alikuwa kashaanza uchunguzi na siku hiyo jioni alikuwa anatakiwa kufanya mahojiano na nagriis ambaye asubuhi ya siku hiyo aliomba wahojiane jioni kwani muda huo alikua kaijisikia vibaya.
Mama salha aliachiwa siku ya pili baada ya kifo cha nagris kwani rose alikuwa akiamini kuwa mama salha aliwekewa mtego tuu ila kuna watu nyuma yake walikuwa wakihusika.
" Pole sana mama salha, tunashukuru umetoka na sisi sasa nafikiri ni muda wa kuondoka ila htun jini tunatakiwa kuondoka na salha"
" asante sana dada yangu aunt amina, nafikiri sasa ni muda wa salha kuishi na dada yake, ila tangu akiwa mdogo kwa kuwa sikujua kama ningeweza ktunza akianza chuo hivyo nikawa namwekea akiba kila mwezi nitaomba nikampe malezo ya hela hizo na kisha imsaidie katika mabo muhimu kwani hapa sasa sio pazuri tenakwa uhai wakee" aliongea mama salha
Siku ya pili yake aunt amina pamoja na wanae wawili walianza safari ya kwenda kusikojulikana kuanza maisha mapya wakiwa wamepewa mtaji mdogo wa kujikimu na kuanzia maish kutoka kwa mwalimu jack na mama salha na baadhi ya marafiki.
***
Alhamis tarehe 14.07.2005
Ilikuwa imetimia miaka miwili na miezi kama mitatu tangu aunt amina, samira na salha wakimbie ule mji na kwenda kusikojulikana bila ya kuwa na mawasiliano na mtu yoyote wa eneo lile.
Siku hii alionkana mze zombo akiwa na mawazo sana na kuwa ameota ndoto ya ajabu sana na kuwa ndoto hiyo ni ya hatari sana. " Eti kila nikijaribu kumlenga samira kumpiga risasi mara anatokea baba yak, mara mama yake n cha kunitisha zaidi kuna mtoto mwingine anafanana sana na samira yeye akaja akiwa amewashika wanangu wawili na kisu mkononi na wanacheka sana wakiwa na kiwi'
"Mzee bilionea hapo lazima kuna kitu na hautakiwi upuuie hilo" aliongea mpambe mmoja ambaye yeye hujifanya ni mshauri wa karibu wa mzee zombo
"Niitieni kiwi haraka sana"
Kiwi alifika pale na mzee alimrukia n kuchapa bakora kama kumi huku akifoka kwa sauti "kwa nini uwepo kwenye ndoto yangu lazima utakuwa msaliti wewe"
"Hapana mzee ni ndoto tuu" alilalamika kiwi
Kila mtu alimshangaa sana mzee zombo lakini kamwe mtu usingediriki kuongea neno pale kwani anafahamika kwa ubabe ambao umejengka katika misingi ya hela.
Kuna simu ilipigwa na alipoipokea mzee zombo ikamfanya aanze kukimbiaa na kuingia kila chumba kama kichaa. Simu hiyo ......................
KIsa hiki kitaendelea KESHO na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia Telegram wasiliana nasi kwa Telegram namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini
Asante sana mdhamini mkuu wa kisa hiki www.karibumbeya.com ambaye anakupa nafasi ya kutangaza biashara yako bure kwa kujisajili kupitia tovuti yao na pia unaweza kuuza na kununua mahitaji yako ya msingi
KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki
0 comments: