LANGO LA MOTONI CHAPTER 19
SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
CHAPTER 19
Ilipoishia
Kila mtu alimshangaa sana mzee zombo lakini kamwe mtu usingediriki kuongea neno pale kwani anafahamika kwa ubabe ambao umejengka katika misingi ya hela.
Kuna simu ilipigwa na alipoipokea mzee zombo ikamfanya aanze kukimbiaa na kuingia kila chumba kama kichaa. Simu hiyo ......................
Endelea
Kuna simu ilipigwa na alipoipokea mzee zombo ikamfanya aanze kukimbiaa na kuingia kila chumba kama kichaa. Mzee zombo hakutaka kabisa kumshirikisha mtu yoyote juu ya simu hiyo au ilimtaka kufanya nini, hali hiyo ilifanya wale walinzi wake waishie kumshangaa mpaka pale alipowaamuru wampelekee bar.
" unajua kuna watu wanatafuta makubwa au wanataka na wao tutumie rimoti kontroo kumyuti sauti zao, miaka miwili nimekaa bila ya shida ila naona huyu sasa anajifanya kuleta chenga wakati chanenli yangu ilikuwa klia kabisa, ok basi mimi nitamsaidia ajue maana ya kuhamia digitali maana kaja kwa spidi isiyo ya kawaida"
"Mzee ni nani huyo tena anayejaribu kuiharibu siku yako, au hajui kuwa wewe huingiliki"
" People are playing of mzee zombo, escape velocity kabisa, sasa nitatumia natural security" aliongea maneno hayo mzee zombo huku akiacha tabasamu kwa baadhi ya walinzi wake kwani walijua hakujua maneno hayo ya kiingereza yalikuwa na maana gani.
Salha siku hiyo aliwahi kurudi kutoka kwenye duka lao dogo walikokuwa wakipatia kula kwa kuuza baadhi ya mboga mboga na matunda na moja kwa moja aliwakuta samira na aunt amina wakiwa wamechoka kwani nao walikuwa wametoka bustani kumwagilia mboga na kuwatika mbegu mpya.
Wakati wakiwa wanasalimiana mara mlango wao ukagongwa na kwa taharuki aunt amina akajikuta akishangaa kuiona sura ya Mohamed au maarufu kwa jina la Muddy akiwa na binti mmoja mrembo.
" Mungu wangu, wewe muddy umefahamu vipi kuwa tuko katika mji huu na umekuja kwa heri au shari?"
" Hapana aunt amina nimewatafuta sana na baadae nimekuja kupata habari juu ya uelekeo mlioenda kutoka kwa mwalimu jack."
" karibu muddy ila bado nahofia ujio wako na mbona mwalimu jack hajui tuliko?"
" aunt amina nitaomba kama hautajali wewe na kina samira tukae sehemu nje ya hapa nyumbani tujadili kuna jambo nataka tuliweke sawa" alihitimisha mjadala huo muddy na baada ya hapo waliondoka.
Muddy ni kijana ambaye aliaminika sana na baba samira enzi za uhai wake na miezi kama saba kabla ya kifo cha baba samira na mama samira muddy aligundua mpango fulani wa kuuawa baba samira uliokuwa ukiendeshwa kwa siri na mzee zombo.
ALimshirikisha baba samira ingawa baba samira hakutaka kabisa kuamini habari hizo mpaka pale muddy alipokuja kutoweka katika mazingira ya kutatanisha. Baba samira aliomboleza kwa muda hasa baada ya kupokea taarifa za kifo cha muddy ambaye ilisemekana kuwa alitupwa mtoni na watu wasiojulikana na kufa akiwa ndani ya gari lake.
Kuanzia hapo baba samira akaanza kuwa makini sana na baadhi ya ndugu zake jambo lililopelekea mzee zombo kubadili namna ya kuutekeleza mpango wake na kujikuta akitumia majambazi sugu wa kukodiwa na kufanikisha kumuua baba samira na yeye kupitia kikao cha ukoo kujichukulia mali zote za baba samira kwa kuwa kila mwanafamilia alimwogopa na wengine walihongwa fedha kidogo.
" Nafikiri hoteli hii ni nzuri na salama kwa sisi kuongea hapa, naomba agizeni mtakachotaka kula au kunywa" aliongea muddy baada ya kufika hotelini
Kila mtu aliagiza alichokitaka na baada ya hapo muddy akaanza kusimulia mkasa mzima wa yaliyomsibu baada ya kuhojiwa na aunt amina.
" Kama unavyokumbuka kuwa mimi nilikuwa mfanyakazi na mtu wa karibu sana wa marehemu baba samira"
"Ndio nakumbuka na sikupata habari zako tangu kifo cha kaka yangu baba samira"
" miezi michache kabla ya baba samira kufariki niliugundua mpango uliosukwa na mzee zombo wa kumfanya baba samira awe kichaa na wao wauchukue utajiri wake, hivyo nikaongea na baba samira
Baba samira kama umjuavyo alivyowapenda nduguze hivyo ikawa ni jambo lisilo la kawaida kwa yeye kuamini kiurahisi. Nikaongea na secreatry wake na kumtahadharisha juu ya chakula chochote au kinywaji kutoka kwa mtu yoyote kumfikia baba samira.
Pia nikaongea na mama samira na kumtahadharisha hivyo mpango wa mzee zombo ukagonga ukuta. Baada ya hapo wakataka kumpandikiza binti mmoja ili aje kutembea na baba samira na kuja kumdhuru hapo baadae lakini nilipougundua nikafanya juu chini na kumwokoa.
Baada ya kuona kuwa nimekuwa kikwazwo jioni moja nikiwa nyumbani nikasikia vishindo vya watu hivyo nikaondoka taratibu na kutokea mlango wa nyumba nikawasha gari langu na wakaanza kunikimbiza.
Kuna sehemu nilifika na kulifanya gari kudumbukia mtoni na siku ya nne baadae gari liliopolewa bila ya mimi kuonekana na wote wakaamini kuwa nimekufa kumbe usiku ule nilipotupa gari mtoni nilirudi na kuchukua baadhi ya vitu vyangu muhimu na kukimbia eneo hilo na kwenda mbali kuanza maisha.
Nimekuwa nikipata taarifa za jinsi samira alivyokuwa akiteseka na nikawa nikitaka kufahamu yule mtoto aliyeachwa hospitali yuko wapi ni kupitia safari hiyo nikajikuta nakutana na mama lasha aliyenipeleka kwa mwalimu jack na nikaanza kuwatafuta hapa.
Hivyo basi nimekuja kwa neno moja tuu la kutaka kuwarudishia mali zenu na kuhakikisha mzee zombo anapelekwa kwenye vyombo vya kisheria. Huyu binti niliyenaye ni Khadija alikuwa secretary wa baba samira na anataka nae kutusaidia na tunafanya haya kwa jinsi ambavyo baba samira alitusaidia sisi na familia zetu"
" Asante sana muddy na sitakushukuru sana zaidi ya kumwomba mungu akupe ulinzi, sasa nini kinatakiwa kufanyika?"
" Mzee zombo ni mtu hatari sna kwani haoni taabu kutumia hela nyingi kwa jambo dogo na pia sio mtu wa kutakiwa kujua wapi sisi tulipo na tunataka nini kwa haraka, hivyo kitu cha kwanza itakuwa ni............................ ........
KIsa hiki kitaendelea KESHO na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia Telegram wasiliana nasi kwa Telegram namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini
Asante sana mdhamini mkuu wa kisa hiki www.karibumbeya.com ambaye anakupa nafasi ya kutangaza biashara yako bure kwa kujisajili kupitia tovuti yao na pia unaweza kuuza na kununua mahitaji yako ya msingi
KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki
0 comments: