LANGO LA MOTONI CHAPTER 20

08:07:00 Unknown 0 Comments

SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU

LANGO LA MOTONI 

CHAPTER 20

Ilipoishia


Hivyo basi nimekuja kwa neno moja tuu la kutaka kuwarudishia mali zenu na kuhakikisha mzee zombo anapelekwa kwenye vyombo vya kisheria. Huyu binti niliyenaye ni Khadija alikuwa secretary wa baba samira na anataka nae kutusaidia na tunafanya haya kwa jinsi ambavyo baba samira alitusaidia sisi na familia zetu"


" Asante sana muddy na sitakushukuru sana zaidi ya kumwomba mungu akupe ulinzi, sasa nini kinatakiwa kufanyika?"

" Mzee zombo ni mtu hatari sna kwani haoni taabu kutumia hela nyingi kwa jambo dogo na pia sio mtu wa kutakiwa kujua wapi sisi tulipo na tunataka nini kwa haraka, hivyo kitu cha kwanza itakuwa ni....................................


Endelea

" Mzee zombo ni mtu hatari sana kwani haoni taabu kutumia hela nyingi kwa jambo dogo na pia sio mtu wa kutakiwa kujua wapi sisi tulipo na tunataka nini kwa haraka, hivyo kitu cha kwanza itakuwa ni kuhakikisha hatumpi nafasi ya kupumua na hilo nimelianza jana nikishirikiana na khadija na nyie wakati huu hakikisheni mnakuwa kimya na watu wasifahamu mliko tutarudi baada ya siku nne"

"sawa sisi tutakuwa kimya na kuwasubiri nyie"


" Asante aunt amina naomba nikutakie usiku mwema na hakikisheni hamwasiliani tena na wale kina mwalimu jack au yoyote kati yao"

"tunakuhakikishia uncle muddy na asante" waliongea kwa pamoja salha na samira na kisha wakatawanyika eneo hilo.


Saa kumi na mbili na nusu asubuhi nyumbani kwa mzee zombo kulionekana kuwa kimya sana na kama kawaida yake mzee zombo alikuwa nje ya nyumba yake akifanya mazoezi. Mara kuna gari moja dogo lilisimama na kuna dada mmoja alishuka na moja kwa moja alimkabidhi mzee zombo bahasha na kisha kuondoka bila hata ya kumpa nafasi mzee zombo kuongena neno.

Hali hiyo ilimshtua sana mzee zombo na kuingia ndani haraka na akajifungia kwenye moja ya ofisi zake pale nyumbani na kuifungua ile bahasha. " Mungu wangu, nimekwisha" 

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mzee zombo kumkumbuka muumba wake tena kwa kumtaja jina kwani alishasahau kuwa ni Mungu pekee ambaye anatakiwa kuabudiwa kwani yeye sasa aliamini hela ndio Mungu na furaha kwake na kuwa ni fedha pekee ingeleta heshima maishani mwake ingawa alisahau kuwa Mungu ni ndio kila kitu.

Kwenye bahasha kulikuwa na picha nne pamoja na flash disck ambayo alikuwa bado hajaiweka kwenye computer yake ili ajue nini kipo ndani. Picha ilimwonesha mzee zombo akimchapa kwa panga manka mangi aliyekuwa msimamizi mkuu wa fedha katika kampuni ya baba samira na kuuawa siku chache baada ya kifo cha baba na mama samira na kusemekana ilkuwa ni ajali ya gari..

Flash disck ilimchanganya zaidi mzee zombo kwani ilionesha baadhi ya nyaraka alizozifanyia uhaini na kulikuwa na file moja la mp3 ambalo lilikuwa na mazungumzo ya simu baina ya zombo na baadhi ya watu kuanzia mpango wa kaka yake kuuawa na mkewe pamoja na kuchukua mali zake ikiwa ni pamoja na ule mpango wa kupoteza jina la samira na asiwepo tena mtu huyo.

" Huyu ni nani tena anayenitafuta, anataka nini kwangu, duuuh" mzee zombo alichanganikiwa na kujikuta akinyanyua glass yake na kutafuta pombe kali ilipo kwani muda huo alihisi ni kama ndoto vile sasa alihitaji kitu kichanganye kichwa ili akili imrejee.

Mpaka ilipofika saa nne na nusu mzee zombo alikuwa kalewa na hajitambui na kajifungia kwenye ofisi yake huku hakuna aliweza kuingia ndani zaidi ya kusikia nyimbo mbalimbali za kulugha kutoka kwa mzee zombo zilizoashiria kuna hatari.

" jamani kuna nini kimemsibu mme wangu" alihoji mama zombo

" mama wote hatujui ni nini kemtokea maana hakuna aliyeongea nae" aliongea binti wa kazi ambaye mara nyingi alikuwa akiamka mapema kumwandalia supu mzee zombo lakini siku hiyo ilikuwa ni ajabu

" bhikulonda pakuumba ipresha, bhangoghe, ubhwalwa ngunlekela jhwani" aliimba wimbo huu mzee zombo nakufanya baadhi ya walinzi waangue kicheko kuona sasa anakumbuka na lugha yake asilia kuliko ile ya kiingereza.

Muddy alikutana saa sita na nusu na khadija pamoja na vijana wake wanne na kwa pamoja wakajadili juu ya zoezi lao la kwanza na kwa furaha muddy akasema.

" jamani nawashukuru sana kwani nimepigiwa simu na chanzo chetu cha uhakika kuwa mzee zombo kachanganyikiwa hivyo  nasi tusilegeze kamba tunatakiwa kufanya leo hii hii zoezi la pili" 

"Asante boss tuko pamoja mimi nawaonea sana huruma watoto wale na aunt amina" aliongea binti mmoja ambaye uso wake haukuonekana kutona na miwani kubwa na kofia aliyoivalia usoni

Jioni ya siku hiyo mama zombo alichukua gari na kwenda sokoni kununua vitu vya muhimu ili angalu atengeneze chakula kizuri cha kumfaa mmewe. Alitamani kufanya hivyo ili kuona mzee zombo akiwa na furaha hata kama hakupenda tabia zake ila aliupenda utajiri wake wa haraka na hakutaka kuyarudia maisha yale ya mwanzo ya kutojua kesho ikoje na watoto wangesomaje.

Akiwa sokoni alikutana na binti mmoja ambaye alimpa bahasha na kumwabia anatakiwa akampe mzee zombo. Mama zombo aliichukua bahasha ile na kuiweka kwenye gari na kumalizia manunuzi na kisha karejea nyumbani baada ya kuwapitia watoto shuleni.

Alijiuliza maswali mengi juu ya ile bahasha kama ampelekee mzee zombo au lah, lakini mwisho wa siku akaichukua na kwenda nayo katika chumba maalumu pale nyumbani na kuangalia ndani ya ile bahasha ambapo alikuta ujumbe ulioandikwa " Mzee zombo, muda ndio huu anza kurujisha mali zisizo zako kwani utaumbuka"

Bila hata ya kupepesa macho mama zombo alichukua bahasha ile na kuichoma moto na kisha akarudi kuandaa chakula cha jioni bila hata ya kumshirikisha mmewe ambaye muda huo alikuwa katulia ila ana mzinga wa pombe kali mezani na hakutaka kabisa kutoka nje ya nyumba yake siku hiyo, " nani ayarudie maisha yale... thubutu yake" alijisemesha mama mzombo huku akimalizia kupika chakula cha usiku.

Ben alikuwa kashakunywa bia ya tatu na picha ya samira ikiwa mezani kwake, kila mara aliiangalia na kujipiga kifua na saa nyingine alisimama na kutoka nje billa kujua nini angefanya. Akiwa pale ghafla ak..........................................





KIsa hiki kitaendelea JUMATATU na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia Telegram wasiliana nasi kwa Telegram  namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini

Asante sana mdhamini mkuu wa kisa hiki www.karibumbeya.com ambaye anakupa nafasi ya kutangaza biashara yako bure kwa kujisajili kupitia tovuti yao na pia unaweza kuuza na kununua mahitaji yako ya msingi

KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki

You Might Also Like

0 comments: