LANGO LA MOTONI CHAPTER 3
SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
CHAPTER 3
Ilipoishia
" hivi binadamu wakoje? mbona wanapenda sana kufuatilia mambo yasiyowahusu? hivi hela za mdogo wako si za kwako? na elimu inahusiana vipi na matumizi tena bar? au natakiwa ninywe kwa calculator? wameniudhi sana wale vijana na nikionana nao naweza hata wagonga na gari"
Akiwa katika dimbwi hilo la mawazo yasiyo na msingi wowote mara dirisha la gari lake liligongwa na alipolifungu alikutana uso kwa uso na............................ ..
Endelea
Akiwa katika dimbwi hilo la mawazo yasiyo na msingi wowote mara dirisha la gari lake liligongwa na alipolifungua alikutana uso kwa uso na askari wa usalama barabarani aliyekuwa akimtaka mzee zombo aliondoe gari kwani alilipaki sehemu isiyo sahihi.
Mzee zombo aliondoka na kujikuta aikishia kwenda bar nyingine na kuendelea kunywa lakini muda mwingi alionekana kutawaliwa na mawazo na hakuwa zombo aliyezoeleka.
Jioni ya siku hiyo aunt amina alionekana akiwa na mawazo mengi na uso wake ulikuwa uligubikwa na machozi hasa baada ya kumkumbuka kaka yake aliyekufa katika mazingira ya kutatanisha huku polisi wakishindwa kuwapata wahusika na mbaya zaidi akakumbuka jinsi alivyoahidiwa kupewa mtaji wa biashara siku chache kabla ya kifo cha marehemu
Aliumia pia kuona jinsi mtoto samira mapito aliyopitia na kujikuta akitokwa na machozi zaidi na alipogeuka nyuma macho yake yaligongana ya yale ya samira ambaye nae alianza kutokwa na machozi baada ya kuona shangazi yake akiwa katika hali ile, na muda mfupi baadae nyumba hiyo iligubikwa na huzuni na majonzi mpaka pale mmewe na aunt amina alivyoingia akiwa na mahitaji ya chakula cha usiku na wote wakaingia jikoni kuanza kuandaa chakula hicho.
Ilipofika mida ya saa nne mme wa aunt amina akiwa amelala na samira amelala pia, aunt amina aliamka na kwenda nje kisha akaichukua simu yake na kumpigia mtu.
" weee malaya mkubwa nimekuambia usinipigie simu tena na ukome kama hela nilishakulipa wataka nini tena? mzee zombo siibiwi kirahisi na kama huamini uliza mabinti wa mji huu, mimi ndio bilionea wa ukubwani" aliongea mzee zombo kwa sauti ya kilevi huku sauti za mziki na kelele za baadhi ya wanywaji zikisikika
" samahani kaka, mimi ni amina, mdogo wako"
" Bado tuu unamawazo yako ya kutetea upumbavu, si nakuuliza?"
" hapana mimi sipo huko ila nauliza juu ya samira kama amerudi likizo kutoka huko shule ya bweni maana nilitamani aje kunitembea"
" mbona unajifanya kama mwalimu mkuu vile? unajua mimi ni kaka yako? habari za likizo niachie mimi, na akirudi utaambiwa... kwani nani analipa ada yake??
tulishakuja kukuomba???? tena kwa kukukomesha yule mtoto juzi nimeongea nae zaidi ya nusu saa na anaongea kiingereza sana unajua gharama zake wewe?????
unaanza kuulizia uliza kuhusu likizo na siku utauliza risiti.... sasa kwa kifupi na kwa kumalizia utapewa taarifa akirudi na mwambie na huyo mjinga mwenzako tena ashukuru tangu muoane sijawahi onana nae, maana ningempiga kelebu, mtu gani hawezi hata kuleta wajomba.... yaani anazidiwa na kuku bwana.. maana kila siku tunakula mayai na kuku wapya?"
" sawa kaka asante na usiku mwema" alikata simu aunt amina na kurudi sebuleni ambako aliyasahau kabisa masuala ya samira na sasa akaanza kulia kwa uchungu baada ya kuitafakari kauli ya kaka yake juu ya yeye kutopata mtoto.
Alilia kwa muda mpaka pale mmewe aliposhtushwa na sauti ya kilio na kwenda sebuleni na akajaribu kumuuliza mkewe na baada ya kusimuliwa kisa kizima alimpa mkewe maneno yenye kumpa nguvu,
" mke wangu, Mungu ana neno ambalo anataka kututumia mimi na wewe kama mfano kwa wengine, sijawahi kukusaliti na kuwa na mtu mwingine, nami hujawahi kunifanyia hivyo..
pengine kwanza tuamini kuwa hii ni bahati kwetu kwani kuna wenzetu wana watoto lakini ndoa zao zinawaka moto na wengine wanafikia kushindwa kuvumilia na kwenda nje ya ndoa na kuzaa huko..
lakini wengine wana watoto na kwa kuwa walishindwa kuwatunza leo hii ni majambazi, mashoga, changudoa na wanajutia kuzaa hata kufa kwa presha.... Muda wa Mungu huja kwa wakati na ukija huja na furaha zaidi... amka mpenzi wangu tukalale" alimazima kuongea huku akimsaidia mkewe kunywa maji na kisha wakaelekea chumbani
Asubuhi na mapema mzee zombo bila hata ya kuaga alimka na kulitia mafuta gari lake na kisha kwenda kwenye kile kituo cha watoto yatima kilichopo umbali mrefu kidogo ili akadadisi kama samira yupo ingawa ilikuwa imepita miaka kadhaa bila ya yeye kwenda hapo.
Alipofika pale kituoni alionana na uongozi na muda mfupi baadae alioneka mzee zombo akiwa anatoka nje ya kituo hicho huku mikono ikiwa kichwani kuashiria hali haiko shwari na akawasha gari lake na kuanza safari ya kurudi mjini haraka.
Akiwa njiani alionekana kuwapigia simu baadhi ya watu na hazikupita dakika nyingi alionekana akiingiza gari katika hotel moja iliyotulia na kukutana na baadhi ya watu waliokuwa wametangulia eneo hilo.
Baadhi ya ya watu waliokuwa hapo ni pamoja na wadogo zake watatu pamoja na mjomba wao ambao kwa pamoja walionekana kushtushwa na taarifa hizo ingawa sio kwa kumwonea huruma bali walianza kuona madhambi yao yanaanza kufichuka.
" Duuuh, sasa na huyu amina na mmewe wana wazimu? walijuaje? dada yetu yule anaweza kuibua kesi na hapo mipango yetu yoote itafichuka..... mimi naona tuamue kitu ndugu zangu" aliongea mjomba
" hapa hakuna kudiscuss sana mimi naona na familia yao iwafuate baba na mama samira maana meno hayajachoka kabisa kutafuna kuku na mtu anataka kukunyan'anya kipande mdomoni... au nyie mnaonaje?" aliongea zombo
"Hilo ndio suala zima kaka, maaana mimi sitaki tena kurudia yale maisha ya zamani maana hata hapa si waona nimekuja nikiwa nimekaa sasa nani arudi kulima viazi" aliongea mdogo wa zombo
"Sasa mimi natoa oda, wewe bwana mdogo KIWI unatakiwa usafiri mpaka mji anaokaa amina na uone mazingira kisha uje tukae na kujadili kitu" aliongea mzee zombo kwa msisitizo huku akimkabidhi kitita cha fedha bwana kiwi.
Kesho yake Kiwi alishuka katika kituo cha magari cha paranga'anda majira ya saa kumi na nusu na moja kwa moja akatafuta hotel na kuweka mizigo yake na kuanza kuzunguka mitaani. Asubuhi yake majira ya saa kumi na moja kasoro alimng'aza samira akiwa anatoka shule na akamtambua ingawa ulipita muda mrefu tangu aonane na samira.
Alianza kumfuatilia kwa ukaribu mpaka akaona nyumba aliyoingia na kuona nje akiwa kakaa aunt amina na baadhi ya marafiki wakiongea neno.Akaondoka zake na kurejea hotelini na siku ya pili alikuwa njiani akirudi mjini ili kutoa ripoti ya utafiti wake.
Asubuhi iliyofuata nyumbani kwa zombo alionekana mzee zombo na kiwi wakinena jambo na baadae mzee zombo alisimama na kupiga simu na dakika ishirini baadae gari moja dogo liliingia na vijana wawili wakashuka na kuungana na mzee zombo na kiwi pale sebuleni.
" Asante sana kwa kuwahi, sasa kuna kazi moja ndogo sana nataka kuwapa,naona kuna vinyang'au vinataka kunisumbua nataka msaada wenu, si mnajua TV ikiwa inapiga sana kelele inatakiwa kuzimwa au kui-mute kupitia rimoti? sasa nyie kama rimoti nataka mtumike vyema."
"Sawa sawa mzee ila unakumbuka kazi ile ya kwanza kuna malipo hukutumalizia?"
"Msijali hii itakuwa na malipo safi, sasa nataka msafiri mpaka paranga'anda kuna nyumba moja iko jirani sana na eden bar mtaona watu hawa hapa pichani, nataka mhakikishe mnawaliza sawa?
kwani nataka yabaki makochi tu mle ndani, kila kitembeacho hakikisha kinapotezewa uhai na mikikuta hata ubwabwa nyie kuleni" alimaliza mzee zombo huku akitoa bahasha na kuwapa wale vijana na kuahidi kuwapa ndonge nono zaidi.
Saa mbili na nusu za usiku aunt amina alianza kuangahika baada ya vidonda vya tumbo kumshika, akamtuma samira aende mtaa wa tatu akanunue maziwa kutoka kwa mfugaji mmoja wa ng'ombe na wakati huo mmewe aunt amina alikuwa ndio anaingia kutoka kazini.
Dakika chache baadae baada ya samira kuondoka mlango uligongwa na baada ya aunt amina kuufungua mlango alikutana uso kwa uso na sura zilizovalia mavazi ya kininja na kuficha nyuso zao na wakampulizia kitu usoni.
wakati akipiga kelele mara mmewe aliyekuwa ndani akaja ili kutoa msaada na kukutana na gongo moja la utosini na kuanguka kisha wakampulizia kitu fulani puani na kuondoka na mmoja wa watu wale aliiona picha ya samira ikiwa ukutani na akaipenda na kuondoka nayo pia.
wakati samira akiwa anarudi alipishana na gari moja lililotokea eneo hilo kwa kasi na kumfanya ajifiche na alipoingia ndani alishtuka kuona mjomba wake akiwa kalala huku damu nyingi zikimtoka na aunt amina akiwa analia kuomba msaada .
Akatoka mbio na kwenda kwa majirani huku akipiga kelele za kuomba msaada na majirani wakaanza kukusanyikana na muda mfupi baadae walikuwa hospitali...............
SAFARI NDIO INAANZA
Unaweza kuwa mdhamini wa simulizi hii au kutumiwa whatsapp kwa kuwasiliana nasi kwa namba
0713317171
Kama umeipenda Jjisikie huru KU-SHARE Pia
*****************
Ili kutangaza Bure kupitia tovuti yetu fuata link hii karibumbeya.com/add-new/ au tuandikie kupitia: support@karibumbeya.com
Pia unaweza kupendekeza sehemu ya kuwepo tangazo lako katikka tovuti yetu ya karibumbeya.com kwa kutuandikia sales@karibumbeya.com au ukatupigia simu kupitia namba 0713317171
*****************
Ili kutangaza Bure kupitia tovuti yetu fuata link hii karibumbeya.com/add-new/ au tuandikie kupitia: support@karibumbeya.com
Pia unaweza kupendekeza sehemu ya kuwepo tangazo lako katikka tovuti yetu ya karibumbeya.com kwa kutuandikia sales@karibumbeya.com au ukatupigia simu kupitia namba 0713317171
0 comments: