LANGO LA MOTONI CHAPTER 5

10:35:00 Unknown 0 Comments



SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU

LANGO LA MOTONI 

CHAPTER 5

Ilipoishia

" Yatapita na utakuwa na furaha zaidi, sasa mimi nitajaribu kuongea na kina mama wenzangu katika kikundi chetu ambacho aunt amina ni katibu ili tuone tunafanya nini kuokoa maisha ya rafiki, dada na mmdogo wetu aunt amina ni hela kubwa ila naamini Mungu atafungua njia"

"Asante sana mwalimu mimi naomba niondoke na kwenda kumwandalia chakula cha jioni" samira alimaliza kuongea maneno hayo huku akijifuta machozi na kuondoka nyumbani kwa mwalimu jack

Endelea

Samira alikuwa ameshatembea umbali wa mita kadhaa kutoka nyumbani kwa mwalimu  jack na  wakati huo  alikuwa akijiandaa kuvuka barabara. Lilikuja gari moja dogo kwa kasi ya ajabu na kusimama mbele yake na ghafla mlango ukafunguliwa.

Alishuka kijana mmoja mwenye umbo la miraba minne na mwenye sura ya upole na kama ungepata nafasi ya kumtazama kwa ukaribu ungekubali mwenyewe kuwa kaka huyu kweli alikuwa mtanashati, mtu mwenye kila sifa za mwanaume wa kisasa ambaye kamwe asingeliweza kukaa sehemu pasipo jicho la dada yoyote yule kumpa maksi zake za utanashati.

" wewe kaka vipi? yaani na barabara yote hiyo wewe uamue kuja kunifuata hapa nilipo? au ni hako ka Mark X kako ka mkopo kanakupa wazimu?" alitweta samira kwa hasira iliyoambatana na mawazo juu ya aunt amina.

" Samahani dada yangu, na mimi nina mawazo mengi sana hapa"

"wewe una mawazo wewe???? acha dharau,  hebu tuache wenye mawazo tukapumzike"

"Tafadhali nishirikishe mawazo yako kwani naweza kuwa msaada, na kama hutojali naomba nikupe lifti kwenda uendako" alisisitiza kaka huyo huku akimvuta samira na kumfungulia mlango.

Samira hakuwa na jinsi zaidi ya kuingia kwenye gari hilo na safari ikaanza ya kwenda nyumbani kwa samira. Walipofika pale kaka yule alishuka na kumfungulia mlango ingawa samira alihoji amepajuaje mahali pale.

" napafahamu sana hapa kwani mjomba wako alikuwa rafiki yangu sana na kama haitoshi alinisaidia sana kutafuta kiwanja kipindi nahamia hapa."

"Ok basi sawa" alimaliza samira na kuingia jikoni kuanza kumwandalia chakula aunt samira na muda mfupi baadae walikuwa njiani wakielekea hospitali.

" pole sana kwa msiba wa mjomba wako na nimefurahi kuona kuwa wewe umesimama kidete kumsaidia shangazi yako,kwani tatizo ni nini linalomfanya shangazi yako aendelee kubaki hospitali?"

" asante, wanadai anatakiwa kupelekwa india na gharama zake ni milioni kumi za kitanzania, naona kama haitawezekana kamwe" alijibu swali hilo samira na kuanza kulia jambo lililomfanya kaka yule asimamishe gari na kwenda kumnunulia maji samira ili yamsaidie.


Walifika hospitali na kijana yule akabaki nje na  baada ya samira kumlisha shangazi muda wa kuondoka ulifika na moja kwa moja wakaondoka zao na kurudi nyumbani na kaka yule akaondoka lakini alikuwa amemwachia namba ya simu ili ampe maendeleo ya aunt amina .

***

JUMAPILI tarehe 17.02.2002

kikao cha dharula kiliitishwa nyumbani kwa mwalimu jack na ajenda kuu ilkuwa ni suala la aunt amina na uchangishaji wa fedha kwa ajili ya matibabu yake.Samira nae alialikwa pale kikaoni ili aweze  kuchangia jambo na kwa pamoja wapate utatuzi.


Kikako kile kilikuwa kigumu sana kwani wiki tatu kabla ya kifo cha mmewe na aunt amina kutokea, aunt amina alichukua mkopo kwa ajili ya kuanzisha biuashara ya mazao ambayo mmewe alikuwa akiisimamia.

Mkopo huo bado ulikuwa haujarejeshwa na kwa kuwa mmewe na aunt amina ndio alikuwa msimamizi mradi huo na mpaka kifo kinamkuta bado walikuwa hawajakaa vizuri na mkewe kujadili walipofikia hivyo hata aunt amina asingeweza kuwa na neno lolote.

Nguvu za ziada ilibidi zitumike ingawa nazo hazikuzaa matunda yoyote zaidi ya kupatikana shilingi laki saba na sitini elfu ambazo nazo kwa mazungumzo ya chini kwa chini zilitakiwa kulipa gharama za madeni ya msibani na pia kuongeza katika kulipia bili ya hospitali.


Samira alipokea zile hela na kuanza kuondoka kurudi nyumbani kwake mida ya saa nne kasoro za usiku. Akiwa njiani alivamiwa na kundi la vijana wajulikanao kwa jina la SOMBA SOMBA ambao walimdaka na kumpora fedha na wakiwa wanajiandaa kumbaka wasamaria wema walijitokeza na kumsaidia na wale vibaka wakakimbia.


Hali ilizidi kuwa ngumu kwa samira kwani asubuhi tuu alipoamka akiwa na majeraha ya jana yake usiku alipigiwa simu kuwa alitakiwa kwenda kulipa bili hospitali.

Ni wakati huu ambapo samira hakuwa na jinsi zaidi ya kuipekua simu yake na kukutana na namba ya kijana ambaye walikutana jana yake. Hakuwa na jinsi akauweka moyo wake kuwa mgumu na wenye ujasiri na kisha akampigia simu.

" Hallo kaka, "

"niambie samira"

"salama kiasi,tafadhali naweza kuonana na wewe muda huu? kwani nina jambo la muhimu sana"

" Ok usijali, niambie ulipo nitakuja mara moja"


" Naomba tukutane nje ya geti la hospitali"

" sawa usijali, nipe dakika 15" alimaliza kuongea kaka huyo na kukata simu kisha akanyanyuka kulifuta gari lake na kuondoka.


Samira alionekana akiwa nje ya geti kuu la kuingilia hospitali na hazikupita dakika nyingi kaka yule ajulikanaye kwa jina la BENITO SONGOMBO aliwasili pale na kwa haraka akashuka na kumfuta samira ambaye alikuwa amekaa kwa huzuni.

" pole samaira nini kimetokea?"

" jana nilipewa laki saba na elfu sitini kwa ajili ya malipo ya aunt amina na kumalizia deni la msiba wa mjomba, nikiwa narudi nyumbani nikavamiwa na kuumizwa na wakataka kunibaka nawashukuru majirani walitoka na kuniokoa na asubuhi nimepigiwa simu kuwa natakiwa kulipa bili ya hospitali na sijui nini nifanye"

Ok, usijali hebu nifuate kwenye gari," aliongea ben huku akimsaidia samira kuingia kwenye gari na kuondoka nae mpaka benki moja na kumtolea fedha taslimu shilingi laki nane na kumwambia samira akalipe bili na abakiwe na elfu arobaini kwa ajili ya matumizi madogo huku akifanya mchakato wa kutafuta fedha nyingine za matibabu zaidi ya aunt amina.

kw amara ya kwanza samira alionekana kuwa na uso wenye matumanini kwa haraka alimwangukia ben miguuni na kumshukuru huku akisema, " kweli nimeamini hata malaika wa heri anatembelea motoni, maana nilikuwa katika moto.

Waliachana pale na samira kaondoka huku akimwacha ben akimwangalia kwa makini samira mabye alikuwa ni chotara aliyechakaa kutokana na matatizo mpaka ikafikia kipindi zile nywele zake zilizopendwa na wengi zikafifia kutokana na shida.


***

Mzee zombo alionekana akiwa ndani ya gari akiongea na mtu kwa maneno makali yenye kuonesha kuwa amekatishwa tamaa na utendaji kazi wao.

" hivi wewe si ni mbwa? hela zote zile halafu eti leo nasikia samira bado yupo mtaani na huyo aunt yake? hivi nyie mnanitafutia nini mimi? au na nyie niwakodie watu waje kuwapa shughuli?"


"Samahani mkuu"

"Mkuu pua yako, sasa nawapa hii mara ya mwisho tu, ikishindikanika inahamia kwenu nataka mpaka ifikapo kesho kutwa nione majeneza mawili yanapita hapa? sawa?


"Sawa mkuu" 

" haya toa makalio yako hapa, unaona raha kukalia magari ya kifahari , pumbavu zako... escape verocity wewe"

Mzee unamaaisha nini?" alihoji kijana yule kwa uoga ulioambatana na kicheko cha tumboni maana alijua fika mzee zombo hana elimu zaidi ya ujanja ujanja.


Maanada yake nini??? huoni kama huo ni msisitizo wa kwenda kujituma? tatizo lenu hamtembei nchi za mbali, kwanz ahata ukienda utafanya nini? bakini tuu hapa tuwape kazi ngumu, haya logout" 

Kijana yule aliondoka na kuingia kwenye gari lake na kutokomea kusikojulikana akiwa na kicheko mwaka.


Saa saba za usiku nyumbani kwa samira kulionekna vijana kama sita waliokuwa wamevalia magwanda ya kujikinga na baridi  na mmoja wao alikuwa ameshika........................




KIsa hiki kitaendelea kesho jioni na kwa wale wanaotaka kusoma kupitia whatsapp wasiliana nasi kwa namba 0713317171


Asante sana mdhamini mkuu wa kisa hiki www.karibumbeya.com

KUmbuka unaweza kutangaza bure kupitia karibu mbeya

Kama umeipenda Jjisikie huru KU-SHARE Pia
*****************
Ili kutangaza Bure kupitia tovuti yetu fuata link hii karibumbeya.com/add-new/ au tuandikie kupitia: support@karibumbeya.com
Pia unaweza kupendekeza sehemu ya kuwepo tangazo lako katikka tovuti yetu ya karibumbeya.com kwa kutuandikia sales@karibumbeya.com au ukatupigia simu kupitia namba 0713317171

You Might Also Like

0 comments: