LANGO LA MOTONI CHAPTER 4
SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
CHAPTER 4
Ilipoishia
wakati samira akiwa anarudi alipishana na gari moja lililotokea eneo hilo kwa kasi na kumfanya ajifiche na alipoingia ndani alishtuka kuona mjomba wake akiwa kalala huku damu nyingi zikimtoka na aunt amina akiwa analia kuomba msaada .
Akatoka mbio na kwenda kwa majirani huku akipiga kelele za kuomba msaada na majirani wakaanza kukusanyikana na muda mfupi baadae walikuwa hospitali.
Akatoka mbio na kwenda kwa majirani huku akipiga kelele za kuomba msaada na majirani wakaanza kukusanyikana na muda mfupi baadae walikuwa hospitali.
Endelea
Hospitalini walionekana baadhi ya watu wakiwa wamekaa na kusimama eneo la mapokezi huku wakiwa na hofu na kwa mbali daktari alionekana akitoka kwenye moja ya chumba cha wagonjwa wa dharura na kuwafuata na kuongea nao kisha vilio vikaitawala hospitali hiyo.
Vilio hivyo vilikolezwa zaidi baada ya kuambiwa kuwa mmewe na aunt amina alikuwa kashafariki hata kabla ya kufikishwa katika hospitali hiyo. Mbaya zaidi hali ya aunt amina ilikuwa bado ni mbaya kwani alikuwa akilalamika maumivu ya macho na kichwa kwa ujumla hivyo samira na majirani wengine wakaondoka eneo hilo na kurudi nyumbani kwa ajili ya taratibu nyingine za mazishi ya mjomba wake.
Zilipita siku saba baada ya mazishi ya mjomba wa samira huku aunt amina akiwa bado yuko hospitali, na siku hii samira alionekana akiteta jambo na daktari na baada ya maongezi hayo samira akaondoka mpaka wodini.
Alifika karibu na kitanda cha aunt amina na kukaa pembeni huku akimwangalia aunt yake ambaye alikuwa kafungwa kitambaa cheupe machoni mwake ili kuzuia mwanga usimuumize zaidi macho yake yaliyokuwa yameathiriwa na sumu aliyopuliziwa usoni siku ya tukio.
" nesi, nesi nesi" aliita aunt amina
"hapana sio nesi ni mimi samira, pole sana aunt yangu, unaendeleaje leo?"
" Bado nina maumivu makali, niliogopa nilivyosikia mtu akiufungua mlango na kisha akakaa kimya nikadhani labda watu wale wanakuja kunimaliza, naogopa sana mwanangu samira, sijui wananitakia nini watu hawa,mjomba wako anaendeleaje?"
Zilipita sekunde kadhaa samira akiwa kimya ingawa machoni alikuwa akitokwa na machozi mfululizo na kilio cha chini kilichomfanya ashindwe kujizuia na kulia kwa sauti kubwa na dakika moja baadae daktari alikuja na kumtoa nje jambo lililompa wasiwasi zaidi aunt amina.
" jamani naomba mniambie ukweli mme wangu yuko wapi?"
"tulia dada, mmeo yuko salama wewe pumzika nafikiri mwanao samira ameshindwa kujizuia kukuona bado unaumwa ila wewe jikaze ili apate nguvu ya kukuhudumia" alimaliza kuongea nesi wa zamu aliyekuwa pale wodini.
Samira aliondoka pale wodini na kurudi mpaka nyumbani na wakati huu alikuwa katika dimbwi zito la mawazo juu ya hatma yake na shangazi yake ambaye alihitaji fedha nyingi ili aweze kupelekwa hospitali nzuri nje ya nchi na kufanyiwa upasuaji mdogo na macho yake yaweze kuona tena.
***
MojaMOja Bar
Zilikuwa zimepita takribani wiki mbili tangu kitokee kifo cha mme wa aunt amina na mbaya zaidi ni kwamba hakuna ndugu yoyote wa aunt amina aliyehudhuria msibani wala kumtakia pole pamoja na taarifa kuzagaa kuwa walipatwa na majanga.
Katika bar hiyo ya mojamoja walionekana mabinti sita wakiingia kwa mbwembwe na madaha na kwenda kuizunguka moja kwa moja sehemu ambayo bilionea wa ukubwani mzee zombo alikuwa ameketi huku akijitamba kama kawaida yake.
"kuna watu duniani hawana akili, hivi mtu unatoka bafuni unaenda kushika nyaya ya umeme bila hata ya kandambili? inabidi ifike pahala watu tuheshimiane kabisa, sasa vijana wangu wamefanya kazi nzuri na jinsi nilivyofurahi nitawapa na bonasi" aliongea maneno hayo mzee zombo huku akiwatizama vijana wake wa kazi waliotekeleza amri ya kuimaliza familia ya aunt amina na wakati huo walikuwa wana imani kuwa familia yote ipo ahera.
Akiwa katikati ya maongezi ghafla simu yake iliita na akatoka nje kwenda kuipokea na aliporudi alikuwa kabadilika yaani sio yule mzee zombo wa majigambo.
" inawezekana kuwa kweli? mbona niliambiwa kuwa kazi imefanyika kwa ufanisi? hapana lazima kitu kifanyike haraka sana" alijisemesha mzee zombo kiasi cha kuwafanya wapambe wake waingiwe na wasiwasi.
" Mzee kuna nini tena?" alihoji mmoja wa wapambe wale
" acha upumbavu wako, kwani hujui kilichotokea au wajifanyisha tu hapa? tena toka kabisa usikae karibu yangu" alimaliza mzee zombo huku akimwacha mpambe huyo katika tafakari nzito na kuanza kuingiwa na hofu kwani mzee zombo tangu aupate utajiri huo wa ukubwani amekuwa mtu wa kuropoka mambo yasiyo na tafsiri sahihi.
Mpambe yule alisimama kwa muda eneo lile na kumwangalia mzee zombo aliyekuwa akiondoka taratibu huku akijisemesha kama vile mtu aliyekuwa akiandamwa na madeni.
Songambele
Samira alionekana akiingia nyumbani kwa mwalimu Jack ambaye alimkaribisha samira na wakakaa sebuleni ingawa samira alionekana kutokwa na machozi kama vile alihitaji msaada wa haraka kuirejesha furaha yake.
" Pole sana mwanangu samira, aunt amina anaendeleaje?"
" wamesema natakiwa kuwa na fedha kiasi cha shilingi millioni 10 ili tumsafirishe mpaka india na aweze kutolewa sumu machoni mwake kwa upasuaji na ndipo atapata ahueni na kuona tena, nimechanganyikiwa mwalimu, wajua yeye ndio mama, baba na ndugu yangu sijui maisha haya yana siri gani kwangu"
"sikia mwanangu, kitu cha msingi ni kumuomba Mungu amtunze na kutupa sisi nguvu ya kuweza kutafuta njia maalumu ya kumsaidia, ukizidi kulia na kukumbuka maisha yako na maswahiba haya, utazidi kujitesa mwanangu"
" Asante, ila mapito yangu na umri wangu haviendani, natamani kuishi kama wasichana wengine kwa kuwa na furaha katika maisha"
" Yatapita na utakuwa na furaha zaidi, sasa mimi nitajaribu kuongea na kina mama wenzangu katika kikundi chetu ambacho aunt amina ni katibu ili tuone tunafanya nini kuokoa maisha ya rafiki, dada na mmdogo wetu aunt amina ni hela kubwa ila naamini Mungu atafungua njia"
"Asante sana mwalimu mimi naomba niondoke na kwenda kumwandalia chakula cha jioni" samira alimaliza kuongea maneno hayo huku akijifuta machozi na kuondoka nyumbani kwa mwalimu jack
Samira alikuwa ameshatembea umbali wa mita kadhaa kutoka nyumbani kwa mwalimu jack na wakati huo alikuwa akijiandaa kuvuka barabara. Lilikuja gari moja dogo kwa kasi ya ajabu na kusimama mbele yake na ghafla mlango ukafunguliwa.
KIsa hiki kitaendelea kesho jioni na kwa wale wanaotaka kusoma kupitia whatsapp wasiliana nasi kwa namba 0716685567
Asante sana mdhamini mkuu wa kisa hiki www.karibumbeya.com
KUmbuka unaweza kutangaza bure kupitia karibu mbeya
Kama umeipenda Jjisikie huru KU-SHARE Pia
*****************
Ili kutangaza Bure kupitia tovuti yetu fuata link hii karibumbeya.com/add-new/ au tuandikie kupitia: support@karibumbeya.com
Pia unaweza kupendekeza sehemu ya kuwepo tangazo lako katikka tovuti yetu ya karibumbeya.com kwa kutuandikia sales@karibumbeya.com au ukatupigia simu kupitia namba 0713317171
*****************
Ili kutangaza Bure kupitia tovuti yetu fuata link hii karibumbeya.com/add-new/ au tuandikie kupitia: support@karibumbeya.com
Pia unaweza kupendekeza sehemu ya kuwepo tangazo lako katikka tovuti yetu ya karibumbeya.com kwa kutuandikia sales@karibumbeya.com au ukatupigia simu kupitia namba 0713317171
0 comments: