LANGO LA MOTONI CHAPTER 6

10:38:00 Unknown 0 Comments



SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU

LANGO LA MOTONI 

CHAPTER 6

Ilipoishia

Mzee unamaaisha nini?" alihoji kijana yule kwa uoga ulioambatana na kicheko cha tumboni maana alijua fika mzee zombo hana elimu zaidi ya ujanja ujanja.


Maanada yake nini??? huoni kama huo ni msisitizo wa kwenda kujituma? tatizo lenu hamtembei nchi za mbali, kwanz ahata ukienda utafanya nini? bakini tuu hapa tuwape kazi ngumu, haya logout" 

Kijana yule aliondoka na kuingia kwenye gari lake na kutokomea kusikojulikana akiwa na kicheko mwaka.

Endelea

Saa saba za usiku nyumbani kwa samira kulionekana vijana kama sita waliokuwa wamevalia magwanda ya kujikinga na baridi  na mmoja wao alikuwa ameshika panga na wengine walikuwa wakiranda randa na kuchungulia ndani na kugundua hakuna mtu na kiongozi wao akatoa simu yake na kumpigia mtu.

"Boss mbona kunaonekana hakuna mtu ndani maana tumecheki kila sehemu hakuna dalili za mtu?"

" Nyie msinitanie naomba msinifanye kichaa kabisa mbona kiongozi wenu hapo amenipigia na kunihakikishia hata jioni alimwona akirudi nyumbani? hebu fanyeni kazi na acheni longolongo" alimaliza kuongea boss huyo na kukata simu.

Jambo hilo lilionekana kummaliza nguvu kijana huyo aliyekuwa kashika panga na kuwaamuru wenzake waondoke eneo hilo mara moja kwani walihisi kama majirani walianza kuamka.

Robo saa baada ya vijana wale kuondoka gari moja dogo lililokuwa likiendeshwa na ben na upande wa kushoto akiwa kakaa samira lilisimamaa na kumshusha samira ambaye alisikika akisema, " asante kwa surprise Ben, sikutegema kama leo ningetoka na kula chakula kizuri, nakushukuru umekuwa kaka yangu na asante kwa kumsaidia aunt amina"

"usijali Samira, sisi binadamu ni ndugu, na tunatakiwa kusaidiana bila kutegemea malipo yoyote..na wala usiwe na wasiwasi na mimi juu ya malipo au labda nataka kitu kwako, hapana nami kuna watu waliwahi nisaidia bila hata kudai, naamini na mimi nina deni kwa watu wenye shida pia na asante kwa kuwa dada na mungu atakupigania" alimaliza kuongea maneno hayo bwana ben na kuondoka eneo hilo.


Siku ya pili asubuhi samira alionekana akiwa hospitali kwa furaha akiongea na shangazi yake na akautumia mwanya huo kumsimulia juu ya mkasa aliokutana nao wa kuporwa na jinsi kijana ben alivyomsaidia na kumwahidi kuwa angemsaidia matibabu ya yake.


Akiwa pale hospitali mara alipigiwa simu na ben na alipotoka alikutana na ben akiwa daktari wa hospitali hiyo ambaye alimsuprise baada ya kumwonesha document zote za aunt amina kupelekwa nchini india kwa ajili ya matibabu.

Furaha ilimshika samira na kwa mshtuko ule ghafla alijikuta akianguka na kupoteza fahamu.Nusu saa baadae aliamka na kujikuta yuko pale hospitali kwenye kitanda akiwa kapumzishwa.

" Nesi nilikuwa naota au ukweli kuwa aunt yangu ataenda kupatiwa matibabu nje?"

" sio ndoto samira, ni ukweli mtupu na hivi sasa taratibu zimeshaanza kufuatwa kwani baada ya siku mbili atatakiwa kuwa ameshafika huko ili kuanza matibabu"

"Mungu wangu nakushukuru kwa kunikumbuka kipindi hiki ambapo dunia imenitenga" aliongea samira maneno yale na kutoka nje kwani ulikuwa ni muda wa daktari wa zamu kupita kwa wagonjwa.

Alirudi nyumbani na kuendelea na maandalizi ya chakula cha mgonjwa na jioni ya siku hiyo ben alikuja kumchukua na wakaongozana pamoja kwwenda hospital.Waliporudi ben alimshusha nyumbani na kuondoka zake.

Majira ya saa mbili na nusu za usiku samira akiwa anatoka nyumbani kwa rafiki wa aunt amina kumpa taarifa ya aunt amina kufanikiwa kupata ufadhili wa matibabu ghafla gari moja moja lilisimama na kumchukua kwa kumteka na kumpeleka kusikojulikana.

Hakuna aliyejua wapi alikuwa samira kwani hata majirani walishangaa mpaka inafika mida ya saa sita za usiku hakuwako nyumbani jambo ambalo halikuwa la kawaida kwa samira. 

Baadhi ya majirani wakaanza kujipanga kumtafuta kwa kuanza hospitali ili kujua kama alirudi huko baada ya kutoka uko alikokuwa lakini bado hakukuwa na taarifa sahihi za  kuweza kumpata.


Samira alikuwa kafungwa kitambaa cheusi usoni mwake pamoja  na ule mwanga wa mbalamwezi lakini kamwe usingeweza kumgundua na watu wale walikuwa wamemzingira kana kwamba walitarajia kumshambulia kwa zile silaha za jadi walizokuwa wamezishika mikononi mwao.


" haya wewe binti sali sala yako ya mwisho, haiwezekani mtoto mdogo kama wewe utusumbue kiasi kwamba tunaonekana hatufai katika kazi tuliyotumwa" alifoka kijana mmoja ambaye kwa sauti yake ya ubabe ungehisi kuwa alikuwa ni kiongozi wa wenzake au la alitaka kuonesha kuwa anafanya kazi sana pengine kuwazidi wenzake.


Wakati huo Samira alishapoteza matumaini ya kuishi hapa dunia akisubiri kufa tu ghafla wakashtushwa na kishindo kikuu kilichoambatana na watu wawili kulalamika maumivu ya kichwa na kuanguka chini huku wengine wakikimbia na akiwa katika taharuki alishangaa kuona akibebwa jujuu kama beseni la ndizi na alipojaribu kujitoa mask alikutana na uso wenye mask pia.


Alingizwa kwenye bari moja bila ya kutambua wapi anaelekea kutokana na giza nene wala bila kupata nafasi ya kumtazama dereva  huyo kutokana na ile mask aliyofungwa zaidi.Dakika chache baadae gari lilismama na akashusha na kutupwa chini kisha gari nikaondoka.


Akiwa hajui ni wapi katupwa na anahangaika kujitoa mask mara alisikia sauti ya mtu akimuuliza mwenzake

"Jamani huyu sio mtu huyu?"

" mzee majaliwa huyu ni mtu hebu washa tochi ya  simu yako tumwangalie aliongea mzee mangi ambaye alikuwa akitoka kilabuni akiwa na rafiki yake mzee majaliwa..

" walifanikiwa kumfikia samira na kumsaidia na kuanza kuondoka naaye bila hata ya kumuuliza kitu kwani muda huo alikuwa akitokwa na machozi na kutoamini kama huyo hai na kujiuliza maswali mengi juu ya mambo hayo yanayomtokea na kuishia kusema kwa sauti kubwa " ASANTE MUNGU"

Mzee majaliwa na mzee mangi walifanikiwa kuonana na majirani wengine waliokuwa wakimtafuta samira na wakakubaliana wote waende  kutoa taarifa kituoni ili nae apate nafasi ya kutoa maaelezo ya nini kilichomsibu.

walifika pale kituoni na samira akaeleza mkasa mzima na baada ya hapo wakarudi nyumbani na kila mmoja akaenda kwake na kumwacha samira akiingia nyumbani kwake na kulala.

Asubuhi na mapema samira aliamka na kwenda hospitali kumwangalia shangazi na kuona maendeleo yako ingawa hakutaka kumsimulia mkasa huo na baada ya kuongea na daktari juu ya maandalizi ya siku ya pili yake ambayo aunt amina alitakiwa  kusafiri.

Aliporudi nyumbani alienda kwa jirani na kuazima simu ili ampigie ben na muda mfupi baadae samira aliondoka kwenda ambako ben alimwambia wakutane. Alipofika pale alimsumulia mkasa mzima.

Ben alimpa pole na baada ya hapo akaenda kumnunulia simu mpya na kumkabidhi na wakaachana kwa ahadi ya kukutana siku ya pili yake saa kumi na mbi jioni ili kumchukua aunt amina na kumpeleka uwanja wa ndege kwa ajili ya safari ya kwenda india.

Aunt amina alikuwa mwenye uso wa matumaini muda wote na akamshukuru sana ben ingawa hakuweza kumwona usoni na kumtania kuwa " asante sana mwanangu, naamingi kwa kudra za mwenyezi mungu nikirudi nitakuja kukuona vizuri. Asante"

"karibu sana aunt amina na nakutakia safari njema na matibabu mema"

Aunt amina apelekwa kwenye ndege na waliruka saa 08:45 za usiku kueleka india kwa ajili ya matibabu. Baada ya kuaagana ben na samira wakaondoka na kumwacha samira kituo cha daladala kwani ben alitakiwa kuwahi sehemu kwenye kikao cha biashara.



Mzee zombo alisikika akiongea na vijana wake na wakati huu alikuwa akitoa maelekezo kwa ukali zaidi.

" Pumbavu sana nyinyi, tena sio wanaume ni wanawake, yaani mnapiga simu na kusema kuwa mlipigwa? yaani kazi ndogo hiyo inawashinda? hamjui hata kutumia natural security?"

 'mkuu alituzidi nguvu huyo mtu na hatujui amejuaje mkakati wetu

"nyambafu sana wewe tena usiongee kitu, nataka jioni hii mfanye kitu mbaya nitakutumia ujumbe haraka saa nimekaa sehemu mbaya"


Samira alikaa kituoni kwa muda mrefu kidogo na hatimaye daladala ikaja na akapanda kuelekea nyumbani. Alipofika karibu na nyumbani kwake alishangaa kuona moto mkubwa ukiwaka juu ya paa la nyumba yake na alipotazama kwa ukaribu akaona ............


KIsa hiki kitaendelea kesho jioni na kwa wale wanaotaka kusoma kupitia whatsapp wasiliana nasi kwa whatsapp  namba 0716685567


Asante sana mdhamini mkuu wa kisa hiki www.karibumbeya.com ambaye anakupa nafasi ya kutangaza biashra yako bure kwa kujisajili kupitia tovuti yao

KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki

Kama umeipenda Jjisikie huru KU-SHARE Pia
*****************
Ili kutangaza Bure kupitia tovuti yetu fuata link hii karibumbeya.com/add-new/ au tuandikie kupitia: support@karibumbeya.com
Pia unaweza kupendekeza sehemu ya kuwepo tangazo lako katikka tovuti yetu ya karibumbeya.com kwa kutuandikia sales@karibumbeya.com au ukatupigia simu kupitia namba 0713317171







You Might Also Like

0 comments: