LANGO LA MOTONI CHAPTER 7

10:45:00 Unknown 0 Comments



SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU

LANGO LA MOTONI 

CHAPTER 7

Ilipoishia

" Pumbavu sana nyinyi, tena sio wanaume ni wanawake, yaani mnapiga simu na kusema kuwa mlipigwa? yaani kazi ndogo hiyo inawashinda? hamjui hata kutumia natural security?"

 'mkuu alituzidi nguvu huyo mtu na hatujui amejuaje mkakati wetu

"nyambafu sana wewe tena usiongee kitu, nataka jioni hii mfanye kitu mbaya nitakutumia ujumbe haraka saa nimekaa sehemu mbaya"

Endelea

Samira alikaa kituoni kwa muda mrefu kidogo na hatimaye daladala ikaja na akapanda kuelekea nyumbani. Alipofika karibu na nyumbani kwake alishangaa kuona moto mkubwa ukiwaka juu ya paa la nyumba yake na alipotazama kwa ukaribu akaona kuwa moto umepamba na majirani wakijaribu kuuzima.

Majirani walipomuona samira walishikwa na mshangao ulioambatana  na kumrukia kwa furaha kwani walihisi yuko ndani na wakashangazwa kuona jinsi watu hao waliochoma nyumba moto  walivyoweza kuufunga mlango na kufuli kubwa nje ili kuhakikisha jitihada zozote za kuwaokoa waliomo ndani zinakwama.

Wakati huu samira hakutokwa hata na chembe ya chozi ila uso wake ulionesha kuwa ni mtu aliyekata tamaa na hakuongea neno zaidi ya kuangalia nyumba ile ikiteketea na juhudi za watu zikigonga mwamba kuokoa chochote kile kutokana na kushindwa kupata njia ya kuingia ndani.

Basi kikao chaa dharula kikafanyika nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa na mwalimu jack akaomba amchukue samira iili aweze kumtunza mpaka hapo aunt amina atakaporudi ili taratibu nyingine ziendelee.. 

Samira alipokelewa vizuri na familia ya mwalimu jack ambaye yeye alikuwa ameolewea na anaishi na mmewe pamoja na mtoto wao mdogo kwani ndoa yao ilikuwa bado changa.


Maisha yaliendelea na sasa samira akawa na jukumu pia la kumsaidia mwalimu jack kukaa na mtoto wakati mwalimu jack akiwa kazini na mmewe akiwa dukani kwake ambako ni jirai sana na makazi yao.

Siku moja majira ya saa nne za asubuhi mwalimu jack akiwa kazini na samira akiwa anafanya usafi sebuleni baada ya kumlisha na kumlaza mtoto, mara mmewe na mwalimu jack aliingia na kunza kuongea na samira.

"unajua wewe mtoto ni mzuri sana?"

"asante anko"

"naona chakula changu sasa kinakufanya unawiri sawa sawa"

" ha ha ha asante mjomba sio chakula tu, ila hata ukarimu wenu umenifanyanisahau kote nilikopitia nawashukuru sana"

"ok, sasa si unajua hii ni jamii?"

" ndio anko"

" sasa unaonaje tukijamiana kabisa?"

" anko unamaanisha nini tafadhali sijakuelewa?"

"ninachomaanisha nipe kidogo nichangamshe damu,  si wajua huwezi kukaa hapa hivi hivi? hata kama ni mpangaji si lazima alipe kodi?" mjomba alimaliza kuongea maneno hayo na kuanza kumshikashika samira na kumlazimisha kuingia chumbani.

Samira alifanikiwa kumponyoka na kutoka nje akiwa analia kwa uchungu kwani alibanwa sana kooni na kuparuliwa usoni wakati wa tafrani hiyo. Mmewe na mwalimu jack akatoka nje kwa haraka na kuongea maneno ya chinichini yenye kuogofya ndani yake.

" Sasa wewe si kabambe? basi nitakuonesha na kama unadhani wewe mjanja basi msimulie na huyo mama mundu uone, hata pombe inaonjwa sasa wewe ni nani upitishe togwa na kuiweka kabatini kwangu na niiache?" alimaliza maneno hayo na kuondoka zake kurudi dukani kwake.

Usiku wakati wakiwa mezani kwa chakula cha usiku mwalimmu jack alishangaa kumwona samira akiwa na kovu usoni hivyo akaona amuulize.

" Samira vipi tena mbona una mikwaruzo usoni"


" aunt jack niliumia wakati naanika nguo ila usijli naendelea vyema"

" jamani kuwa makini usije pata majeraha na aunt  amina akija aumie"

"Usijali aunt jack" alimaliza neno hilo na kunyanyuka kuelekea jikoni akimwacha mwalimu jack akiwa na mmewe mezani ambaye wakati huo alijifanya kuwa busy na kijiko chake huku mkono mwingine akiigusa gusa simu yake.

Siku ya pili asubuhi mmewe na mwalimu jack aliamka akiwa na hasira kama mbogo na kudai kuwa kaibiwa hela yake aliyoiweka juu ya kabati ingawa hakuna aliyedai kazichukua. 

Hapo ndipo baba wa watu akapandisha hasira na kuanza kupekuwa chumba baada ya chumba mpaka akafanikiwa kuikuta bahasha yenye fedha hizo ikiwa kwenye kabati la nguo za samira tena katikati ya dira lake.

Samira alipokea kipigo cha mbwa mwizi kutoka kwa mmewe na mwalimu jack na kibao kimoja kilichomfanya aangukie sakafuni na kumpa nafasi mwalimu jack kumuuliza

" samira umeanza na tabia ya kuiba? humu ndani tupo watu wazima watatu tuu na mtoto mdogo asiyejua hata nini maana ya fedha, unafikiri utasema nini ueleweke na wakati wewe ndio unabaki hapa?"

" samahani aunt, kamwe sitakuja kuiba na sijawahi kuiba, labda wakati nafanya usafi nilichua bila kuona ila naombeni mnisamehe" aliomba samira kwa sauti ya chini huku akizidi kuomba msamaha.

Wakati huo mmewe na jack alishapiga simu polisi na hazikupita dakika nyingi polisi wawili walifika pale na kumchukua samira wakiambatana na mwalimu jack na mmewe kwenda kituoni kutoa maelezo. Baada ya kufika pale na kutoa maelezo samira alichukuliwa na kuweka mahabusu na kwa hasira mwalimu jack na mmewe wakaondoka.

Wakiwa njiani waliachana mwalimu jack akaelekea kazini na mmewe akanyoosha kuelekea dukani kwake na alopokuwa peke yake akaanza kujisemesha,

 " pumbavu sana, yaani wewe umepewa bure na uko nyumbani kwa mtu bure unakula jasho lake lakini bado unaleta kiburi?

 sasa kiburi chake kimemponza, yaani mchezo mdogo tuu nimemchezesha nae kaingia kati na nafikiri sasa huko atajamiana na mbu, na nitakapoenda kumtoa hapo baadae lazima alegeee tuu mtoto mdogo sana yule, ngoma yangu ile"


Pale polisi baada ya masaa kama mawili vile, polisi walikuwa wanakabidhiana zamu na polisi aliyekuwa akiingia muda huo alipofungua mlango wa mahabusu akashagaa kumwona samira.

 " samira mdogo wangu kuna nini tena mpaka uko humu ndani? si ni jana tu nimekuona hapo mtaa wa pili ukiwa huru, vipi kuna nini?"

" dada nimetuhumiwa kuwa nimeiba fedha lakini ukweli sijaiba fedha yoyote ile"

" Kwa hiyo umefanya utaratibu gani? maana hapa sio pazuri"

"yaani sijui lolote dada"


"huna ndugu yoyote wa kuja kukuwekea dhamana?"

" Yupo kaka ben, ila sina namba yake kichwani"

"ook yule ben mwenye ile gari mark X?"

"Ndio"

Polisi yule wa kike baada ya kujibiwa hivyo na kwa kuwa anamfahamu ben alimpigia na muda mfupi baadae ben alikuja na akafanikiwa kumwekea dhamana na kumtoa kisha akaondoka mpaka nyumbani kwa mwalimu jack na kuomba msamaha kwa niaba ya samira na akaomba pia amchukue samira ili amtunze mpaka aunt yake atakaporudi jambo ambalo mwalimu jack alilipokea kwa furaha ili kuepusha kuendelea kuibiwa.


Ben na samira wakaondoka mpaka hostel moja ya wanafunzi ambapo ben akampangia chumba samira na kumwekea mahitaji yote  ya msingi, kisha wakaachana. 

Huku nyuma nyumbani kwa mwalimu jack mmewe na mwalimu jack aliishiwa nguvu kwani aliona kuwa njama zake zimegonga mwamba na akaanza kukaa kwa hofu akihisi kuwa samira angetoa siri muda wowote.


***

Ulikuwa umepita mwezi mmoja tangu mzee zombo afanikiwe kuteketeza nyumba ya aunt amina ambaye ni dada yake wa damu ili tu kuhakikisha anatumia nafasi hiyo kupoteza kabisa utambulisho wa samira na kwa habari alizokuwa nazo ilikuwa ni kwamba samira alikufa katika moto huo mkubwa ulioteketeza kila kitu.

Mzee zombo alikuwa akisherehekea ushindi  wa kumtoa duniani   samira nawatu walikuwa wakinywa kwa furaha na  katikati ya tafrija hiyo mara gari la polisi likaizingira nyumba hiyo.



KIsa hiki kitaendelea kesho jioni na kwa wale wanaotaka kusoma kupitia whatsapp wasiliana nasi kwa whatsapp  namba 0713317171


Asante sana mdhamini mkuu wa kisa hiki www.karibumbeya.com ambaye anakupa nafasi ya kutangaza biashra yako bure kwa kujisajili kupitia tovuti yao

KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki


Kama umeipenda Jjisikie huru KU-SHARE Pia
*****************
Ili kutangaza Bure kupitia tovuti yetu fuata link hii karibumbeya.com/add-new/ au tuandikie kupitia: support@karibumbeya.com
Pia unaweza kupendekeza sehemu ya kuwepo tangazo lako katikka tovuti yetu ya karibumbeya.com kwa kutuandikia sales@karibumbeya.com au ukatupigia simu kupitia namba 0713317171








You Might Also Like

0 comments: