LANGO LA MOTONI CHAPTER 27

16:08:00 Unknown 0 Comments



SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU

LANGO LA MOTONI 

CHAPTER 27


Ilipoishia

Mzee zombo alirudi nyumbani kwake saa sita kasoro za mchana siku hiyo na kama kawaida hakuna aliyeweza kumuuliza wapi alikuwa. Muda mwingi alionekana kuwa na furaha kutokana na umahiri wa Suzane kitandani jana yake.

Aliingia chumbani na kumshuhudia mkewe akiwa bado kalala fofofo, hkufanya lolote zaidi ya kuondoka na kwenda sebuleni ambako alijumuika na wazee wenzake aliowaalika kupata vinywaji muda huo.

Saa kumi kasoro kuna mgonjwa alianza kurusha miguu kama dalili za kutaka kukuta kauli, manesi na madaktari walikizunguka kitanda chake na dikika mbili baadae mgonjwa ali.......................


Endelea

Saa kumi kasoro kuna mgonjwa alianza kurusha miguu kama dalili za kutaka kukata kauli, manesi na madaktari walikizunguka kitanda chake na dikika mbili baadae mgonjwa alikata kauli.

Muddy aliiaga dunia muda huo na hakika lilikuwa ni pengo kubwa sana katika harakati ya kuhakikisha samira na salha wanapata haki yako kutoka kwa mjomba wao mzee zombo ambaye alimuua marehemu baba yao na kujinyakulia mali zote za familia ya samira na salha.

Ben alikuwa kaumia vibaya mno sehemu mbalimbali za kichwa chake na hakuweza kuona, kusema au hata kusikia lolote zaidi ya mashine kumsaidia katika kila jambo.

Siku sita baadae aunt amina, samira na salha walisafiri mpaka kwa mwalimu jack na kwa pamoja walienda kwenye kaburi la muddy kutoa heshima zao na baada ya hapo walienda mpaka hospitali ambako walifanikiwa kumwona ben ingawa hakuwa katika hali nzuri kwani bado aliendelea kutumia mashine.

Wakaondoka na kurudi kijijini kwao wakiendelea na maisha yao na kwa pamoja wakakubaliana waendelee na maisha yao bila ya kujaribu kitu chochote juu mzee zombo na mara kwa mara samira alimtembelea ben ingawa bado hali yake haikuleta matumaini.

Maisha yaliendelea na siku moja usiku baada ya miezi kama nane wakiwa wamelala walisikia kishindo cha mtu nje kwa muda ingawa hakuna aliyejali kwani nyumba yao ilikuwa jirani na uchochoro hivyo wakajua ni wapita njia.

Asubuhi saa kumi na mbili salha alikuwa wa kwanza kuamka na alipotoka nje alikutana na bahaya kubwa ya kaki ikiwa mlangoni na juu kulikuwa na na maneno " iwafikie SAMIRA, SALHA na AUNT AMINA".

Salha alishtuka na kurudi haraka ndani na kuwasimulia samira na aunt amina ambao walitoka na baada ya mabishano ya muda kama waichukue au waiache wakakubaliana waichukue na kwenda ndani ili wafungue na kuona kuna nini.

"Mtumeeeeeeee!!!!!!!" alipayuka aunt amina kwa mshtuko baada ya kukuta kuna mabunda kadhaa ya fedha. pamoja na karatasi lilioandikwa kwa kutumia mashine ya kuandikia (typing machine) na ujumbe ulisomeaka.

" Kwenu ndugu zangu wapendwa SAMIRA, SALHA na AUNT AMINA,

Maisha yanamapitio mengi ambayo kwa undani wake yana machungu na furaha kwa baadhi ya watu.

Kuna mengi twajifunza kupitia mapito haya hata kama mtu utaumia kwa kiasi gani. Pia kuna watu ambao wao hupoteza furaha za watu kwa kisingizio cha kuipatia utajiri.

Kwa waliowahi au kujaribu kupitia hayo mnayoyapitia wanaujua uchungu na kukata tamaa ya maisha kama hali inayowakuta sasa.

Sitapenda kufahamika ila naomba kiasi hicho cha pesa cha shilingi milioni 15 mkitumie kwa kufanya kitu kitakachowapa kipato cha siku na nitaendelea kuwafuatilia na nitafurahi kama nitaona matunda.

Narudia, msiogope mkajua ina madhara ila naomba muamini baba samira na salha aliishi na watu vyema na watu na kutatua matatizo ya wengi  na naamini huko aliko na mkewe watafurahi kuona kama kuna watu wanajaribu kurudisha fadhili.

Nawatakia maisha mema

Wasalamu

Asiye taka kufahamika"


Baada ya kusoma barua hiyo kila mmoja alijikuta akilia na baada ya hapo walizihifadhi hela zile na kujadiliana kama waziache au lah kwani wote walishapoteza imani na mtu yoyote duniani.

Siku hiyo ilimalizika salama huku kila mmoja akiwa na mengi ya kujiuliza bila majibu na siku ya pili samira alisafiri kwenda kumtembelea ben ingawa alipofika pale ashtuka kuona..................................................

Kisa hiki kitanendelea KESHO

Kwa wale wanaotaka kukisoma kisha hiki  kupitia whatsapp wasiliana nami kwa  namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini kuwa kupewa promo ya bidhaa zako kupiti hadithi hii

Kama umeipenda Jjisikie huru KU-SHARE Pia
*****************
Ili kutangaza Bure kupitia tovuti yetu fuata link hii karibumbeya.com/add-new/ au tuandikie kupitia: support@karibumbeya.com
Pia unaweza kupendekeza sehemu ya kuwepo tangazo lako katikka tovuti yetu ya karibumbeya.com kwa kutuandikia sales@karibumbeya.com au ukatupigia simu kupitia namba 0713317171

You Might Also Like

0 comments: