LANGO LA MOTONI CHAPTER 28

16:10:00 Unknown 0 Comments

SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU

LANGO LA MOTONI 

CHAPTER 28


Ilipoishia


Baada ya kusoma barua hiyo kila mmoja alijikuta akilia na baada ya hapo walizihifadhi hela zile na kujadiliana kama waziache au lah kwani wote walishapoteza imani na mtu yoyote duniani.

Siku hiyo ilimalizika salama huku kila mmoja akiwa na mengi ya kujiuliza bila majibu na siku ya pili samira alisafiri kwenda kumtembelea ben ingawa alipofika pale ashtuka kuona..................................................

Endelea

Siku hiyo ilimalizika salama huku kila mmoja akiwa na mengi ya kujiuliza bila majibu na siku ya pili samira alisafiri kwenda kumtembelea ben ingawa alipofika pale ashtuka kuona kitanda cha ben kiko tupu.

Akamfuata dada mmoja aliyekuwa akifanya usafi pale na kumuuliza kulikoni. Dada kamwambia kuwa mgonjwa  huyo alizidiwa sana usiku na hivyo ndugu walikuja na asubuhi hiyo wamemwamisha na haijulikani wapi wamempeleka.

Likikuwa ni pigo zito kwa samira kwani muddy hayupo tena na sasa ben kahamishwa na hajui kama amekufa au huko aliko yukoje. Aliogopa kuendelea kukaa pale hivyo akaamua aondoke kurudi nyumbani ingawa kabla ya kuondoka akapitia kwenye bonde moja na kuyachukua yale maua aliyotaka kumpelekea ben na kuyatupa na kisha akaondoka.

Ilikuwa ni safari ndefu lakini aliwasili nyumbani na kujitupa kitandani bila hata ya kutaka kumsimulia mtu na hatimaye akapitiwa na usingizi mzito ulioambatana na mawazo na simanzi.

Siku sita baadae nyumbani kwa mzee zombo kulioneka kundi la wageni  wakiwasili, siku hivyo mama zombo alikuwa kachelewa kurudi kutoka matembezini. ALishtuka aliporudi na kushuhudia baadhi ya nduguze kutoka kijijini wakiwa pale nyumbani.

Pamoja na mshtuko aliokuwa nao hasa ukizingatia hakuambiwa kama kuna ugeni lakini alijifanya kutabasamu kila dakika huku akiongea nao kwa furaha na kila mmoja alionesha kumsifia jinsi alivyopendeza.

Dakika chache baadae mzee zombo aliingia pale nyumbani akiwa  kaambatana na wapambe wake. Aliwasalimia wageni na kumwita binti wa kazi awape vinywaji na kila mtu akawa hajui nini kinaendelea.

" Ndugu zangu, poleni kwa safari, i know its a high way traffic jam with bam bam up to here, ila asanteni kwa kuja na nimewaita hapa kwa jambo kuu na muhimu sana" wakati huo kila mtu alikuwa katulia akimfuatilia na wengine wakitabasamu kwa kiingereza chake

" leo natangaza rasmi kuwa mke wangu na mimi tutatengana kwani amekuwa sio mwaminifu hasa kwa kushirikiana na maadui ili kunimaliza mimi" wakati akiendelea kuongea mezani aliweka bahasha yenye picha kimwonesha mama zombo akiwa kule porini na mkoba na nyingine akiwa hotelini na agrey.

KIla mtu alijifanya kushtuka sana na wengine waliongeza kushtuka ili angalau mzee zombo awaone na baadae wapate mgao mkubwa wa fedha kwani ndio ilikuwa njia pekee ya kuonesha kama wanaumiza.

Baada ya kumaliza hakuongea neno zaidi ya kumpa funguo ya gari moja na kumwambia anatakiwa afungashe mizigo na kupotea kabisa eneo hilo na kuwa watoto wote watapelekwa shule za bweni.

Usiku wa siku hiyo ulikuwa mrefu sana kwa mama zombo ingawa hakuna jitihada liyofanikiwa kumfanya mzee zombo amwelewe. Na hatimaye siku ya pili yake aliondoka na kurudi kijijini kwake na huku mjini akampa nafasi suzane kuwa free na mzee zombo.

***

Ilipita miezi sita huku kukiwa hakuna dalili au fununu ya wapi ben aliko au anaendeleaje. Aunt amina pamoja na wanae samira na salha walifanikiwa kuwa na mradi mkubwa wa kuku na kwale ambao waliwafuga na kufanya vizuri katika mauzo.

Walikuwa pia na hotel ambayo ilipendwa sana na watu wengi  kwa ukarimu wao pamoja na kuwa na vyakula vya bei rahisi na salha alikuwa kafanikiwa kupata kazi kama secretary katika kampuni mmoja ya uwakili na yeye alipendwa sana kazini kwake.

Katika hospitali moja ya bingwa kwa matibabu ya mifupa alionekana mgonjwa mmoja akifanyishwa mazoezi na hakuwa na kumbukumbu yoyote. Baada ya mazoezi alirudi chumbani na kulala lakini kuna picha kila akiiona kuna kumbukumbu zilitaka kumrudia lakini hakuna aliyeweza kujua picha hiyo ya binti huyo ilikuwa na maana gani kwa kijana huyo.

Jioni ya siku hiyo salha alikuwa akirudi kutoka kazini kwa kutumia usafiri wa bodaboda na wakati wanakaribia kuingia barabara iendayo kwao bodaboda ile iliacha njia na kuingia mtaroni.

Salha aliumia mguu ambao ulikatika na hivyo akakimbizwa haraka hospital  ambako alipewa matibabu ya awali na muda huo huo  alichukuliwa na kupelekwa hospital kubwa kwa ajili ya matibabu zaidi.

Taarifa zilimfikia samira na aunt amina wakiwa ofisini kwao na kwa mshtuko aunt amina alizimia na kuomba baadhi ya majirani kumsaidia na samira akachukua usafiri kwenda makao makuu ya mji huo alikopelekwa salha.

Alifika na kukuta matibabu yameanza lakini...............................................

Kisa hiki kitanendelea KESHO

Kwa wale wanaotaka kukisoma kisha hiki  kupitia whatsapp wasiliana nami kwa  namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini kuwa kupewa promo ya bidhaa zako kupiti hadithi hii

Kama umeipenda Jjisikie huru KU-SHARE Pia
*****************
Ili kutangaza Bure kupitia tovuti yetu fuata link hii karibumbeya.com/add-new/ au tuandikie kupitia: support@karibumbeya.com
Pia unaweza kupendekeza sehemu ya kuwepo tangazo lako katikka tovuti yetu ya karibumbeya.com kwa kutuandikia sales@karibumbeya.com au ukatupigia simu kupitia namba 0713317171

You Might Also Like

0 comments: