Mambo ambayo kama hutaanza kuyafanya wiki hii na kuendelea basi wewe utaishia kuwa maskini wa kufa
1.Usiwe mtu wa kulalamika kwa sababu hakuna mtu liye sahihi sana katika maisha haya.
2. Usimlaumu mtu hapa duniani kwani ulizaliwa peke yako na kila jukumu mbele yako ni lako wewe na utakufa peke yako.
3. Usijaribu kulazimisha watu wafikiri kama wewe au kuwahukumu watu kwa jinsi unavyofikiria wewe, jitahidi kuwa upande wa pili wa wao kabla ya maamuzi
4. Usiwe mtu wa kunung’unika kila wakati kwani hiyo hukupunguzia mori na ari ya kazi
5. Usijimilikishe mambo na majukumu makubwa ukidhani utaishi milele kuwa na kiasi nacho hakitapotea….
6. Usijisifie na kujipa ufahari mapema kumbuka bado tupo safarini na kunaweza kutokea lolote njiani
7. Usiwe na wivu mbaya kwani kila kitu ni matokeo ya mtu kujituma na Mungu kukamilishia mipango yake kwako.
8. Kamwe usitengeneze nafasi ya kisasi katika moyo wako kwani malipo yake huangamiza nafsi na moyo wako pia
9. Usijaribu kwa namna yoyote kumsababisha mtu akakosa riziki yake na familia yake kwa makusudi au bahati mbaya, dhambi hiyo huwa na doa lisilofutika na hukuandama kama laana
10. Kuwa mwepesi wa shukrani kwa kila jambo jema kwako hata kama ni dogo kiasi gani
11. Daima epuka: Unafiki, Umbea na majungu bali wewe kuwe mwenye busara kwa kila jambo
12.Tabasamu na kumtakia rafiki yako siku njema
0 comments: