MAMBO MUHIMU YA KUJUA WEWE KIJANA WA KIUME AMBAYE MTUMIAJI WA FB

13:17:00 Unknown 0 Comments



1. Sio kila binti anatekukubalia uwe rafiki hapa facebook basi kakupenda na anataka akakutanulie miguu yake, wengi wapo hapa fb kwa lengo la kuongeza marafiki na kubadilishana mawazo.
2. Sio kila binti atakaye like picha yako basi anataka usumbufu huko inbox, tulia na comment asante kisha endele ana kazi zako
3. Sio kila binti hapa facebook anataka kuchati masuala ya mapenzi huko inbox jaribu basi kuongelea hata masuala ya katiba mpya au maisha kwa ujumla na sio ngono tu
4. Sio kila ukimwona binti online hata kama ni saa tisa za usiku basi wewe unaanza kushusha maneno yako ambayo hayana upako …. Kuna wengine wanakamilisha majukumu yao ya siku iliyopita au wako na wenza wao
5. Binti akikuambia hapendi habari zako za inbox hana maana anataka ujenge nae beef, jaribu kuwa mwelewa
6. Kuna mabinti wengine wanatumia kwa pamoja na waume zao fb account zao, sasa hayo majina ya hello my love, wife, mpenzi nani kakutuma kuyapeleka. Wakiingia katika ungomvi utawasuluhisha? nyambafu kabisa
7. Kutagi watu mapicha ya ajabu wewe kijana hebu acha hizo mambo zako haraka bwana kuna wengine wana familia na wadogo zao huku fb
8. Kuinbox watu mapicha ya ngono pia uache
9. Kuchukua picha za mabinti wa watu hapa fb na kujifanya wake zako au kuwaweka kwenye profile yako acha kabisa
10. Kijana acha kufungua akaunti kwa majina ya kike ili udake mabinti huku fb
11. Mwisho sio unaamka tu una mashida yako unaanza kufungua magroup ya chati za upuuzi na kualika kila mtu kama vile kila mtu anaushabikia huo uzushi wako.

FB ina lengo la kuhabarisha, kufundishana tabia njema, kurahisisha biashara na sio danguro hili

You Might Also Like

0 comments: