WANAUME KUWENI MAKINI NA WANAWAKE WA AINA HII
1. Hamna hata wiki mbili tangu muwe wapenzi yeye ananza kuomba umkutanishe na dada zako au baadhi ya ndugu hata kuanza kuwasiliana nao mara kwa mara ----Jua anatengeneza mazingira ya ndoa
2. Binti mmeanza naye mahusiano kila akija kwako kukutembelea mara kakununulia sahani, vijiko na vitu vinginevyo-Jua anatengeneza mazingira ya ndoa
3. Mwanamke hamjakaa na kujadili suala la ndoa wala chochote lakini yeye kila mara anakusimulia juu ya marafiki zake wanavyoolewa kwa kasi--kaka Jua anatengeneza mazingira ya ndoa
4. Kila siku akija kwako mara ajifanye kusahau nguo, viatu, make-cup set yake na mengineyo --Braza braza Jua anatengeneza mazingira ya ndoa
5. Binti anakutambulisha kwa kasi kwa watu wengi hasa ndugu na marafiki na saa nyingine kukulazimisha uwapigie---Jua anatengeneza mazingira ya ndoa
6. Binti akipokea mshahara wake anaanza kukushirikisha matumizi yake na mna muda mchache tu tangu mfahamiane naye na kila hatua ya maisha yake anakuomba ushauri--- kaka kaka jua unamshauri mke mtarajiwa
0 comments: